GSENGOtV
"Wana siasa ni wanasiasa tu unakuta mtu anakwenda Magu lakini anaamua kupitia Misungwi sishangai" (PITIA jigrafia ya jiji la Mwanza utaelewa) Asema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Siasa mkoa wa Mwanza kujadili Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu, tangu Uchaguzi Mkuu Octoba 2015 hadi mwezi November 2018.
Katika muhtasari wake wa kufungua kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha VETA Mwanza, Dkt. Diallo amefunguka pia juu ya maneno yanayo sambaa kuhusu hali tete ya mahusiano baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, kwamba hawaivi chungu kimoja.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Siasa na huku akitizamana uso kwa uso na Mongella, Mhe. Diallo amesema "Huu mkoa wetu unaangaliwa na karibu kila mtu, kwa hiyo maneno hayawezi kukosekana, utaambiwa mkuu wa Mwenyekiti wa Chama mkoa haelewani na Mkuu wa Mkoa, Katibu haelewani na Mwenyekiti wako"....... "Hayo ni maneno tu na sisi kwakuwa tumeshayazoea kwenye siasa, tunayaelewa na wala hayatupi shida"
Aidha Katika mrejesho wanakamati kwa pamoja wameridhishwa na mwenendo wa ufuatiliaji, utendaji na usimamizi wa utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Fuatilia yaliyojiri ikiwa ni pamoja na utambulisho wa aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya CHADEMA na kutimkia CCM Joseph Michael Mkundi na pia utapata mrejesho mzima wa yale yaliyojadiliwa kwenye kikao toka kwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Mangelepa, vipi kuna mtu kawajibishwa?......
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.