Saturday, May 11, 2019
WAZAZI WA RC MWANZA WATIMIZA MIAKA 50 YA NDOA
Miaka 50 ya ndoa ya wazazi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John V.K. Mongella, Pichani ni wakiwa mbele ya madhabahu ni Bw. Silvin Ibengwe Mongella na mkewe Bi. Getrude Mongella aliyekuwa Rais wa Kwanza Bunge la Umoja wa Afrika, pia mbunge wa zamani Jimbo la Ukerewe mkoani Mwanza nchini Tanzania, ambapo mapema hii leo Ijumaa ya tarehe 10 Mei 2019 majira ya saa 12:30 asubuhi ibada Takatifu ya shukurani imefanyika katika Kanisa Katoliki kigango cha Kiseke wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Miaka 50 si mchezo hakika kuna kitu cha kujifunza toka kwao, Jeh wao wamesema nini? Sikiliza VIDEO HII INA KILA KITU.
BOKO WAUA WANANCHI SABA NDANI YA MWEZI MMOJA NA TEMBO WAFANYA UHARIBIFU MAZAO YA WANANCHI WA IRINGA
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Masunya wakati wa baraza la madiwani wakijadili kuhusu athari za wanyama Tembo na Boko
Madiwani na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wakiwa kwenye baraza kujadili athari zitikanazo na wanyama Tembo na Boko
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
JUMLA ya wananchi saba
wameuwawa na mnyama aina ya Boko ndani ya mwezi mmoja katika bwawa la Mtera
lililopo katika tarafa ya Ismani halmashauri ya wilaya ya Iringa huku pia
mnyama aina ya Tembo akiendelea kuharibu mazao ya wakulima wa halmashauri hiyo.
Akizungumza katika baraza la
madiwani ,diwani wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi kutoka katika
tarafa ya Ismani Yusta Kinyanga alisema kuwa mnyama aina ya Boko wamezaliana
kwa kasi kubwa na kuwa wengi katika bwawa la Mtera na kusababisha vifo vya
wananchi kutoka na wingi wao.
“Saizi Boko hao wapo wengi mno
katika bwawa hili la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi ambavyo havina tija
yoyote na kupunguza nguvu kazi za taifa kwa kuuwawa na book hao” alisema Kinyanga
Kinyanga alisema kuwa Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli aliagiza mamlaka
zinazohusika kuhakikisaha wanavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wavuvi
wanaofanya shughuli zake katika bwawa hilo.
“Alipokuwaja Rais hapa
nilimweleza juu ya swala hili la Boko na aliziagiza mamlaka husika
kushughulikia swala hilo lakini toka alipoondoka Rais hadi sasa wananchi saba
wameuuwawa kwa maana hiyo mamlaka husika zimepuuza tamko la Rais na kusababisha
vifo hivyo vya wananchi” alisema Kinyanga
Kinyanga ameiomba mamlaka
zinazohusika kuhakikisha wanawavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wananchi
vinavyosababisha kuacha wanawake wengi kuwa wajane kutokana na wanaume zao
kuuwa na viboko hao.
“Wanaofanya kazi ya uvuvi ni
wanaume ambao kwa asilimia kubwa wameshaoa na wanafamilia hivyo kuuwawa kwa wanaume hao kuwanawacha
wanawake kuishi bila wanaume zao hivyo kumpelekea mwanamke huyo kuwa mjane”
alisema Kinyanga
Naye diwani wa kata ya Ilolo
mpya,Fundi Mihayo amesema kuwa wanyama wa aina ya tembo wamefanya uharibifu wa
mazao wa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuwepo kwa kundi kubwa na Tembo
ambao wanafanya uharibifu wa mazao ya wananchi.
“Mwaka huu kundi kubwa hili la
tembo hatujui limetoka wapi na limekuja kuleta athari za mazao kwa wananchi wetu na mamlaka husika hakuna
jitihada yoyote ile ambayo wanaifanya kuhakikisha wanakabiliana na tembo hao”
alisema Mihayo
Mihayo alisema athari nyingine
ambayo imejitokezani kushindwa kwa wanafunzi kwenda shuleni kwa kuhofia
kudhuliwa na Tembo ambao wamekuwa wakitembea katika maeneo hao ambao wanafunzi
hao ndio njia kuu ya kuelekea shuleni.
“Saizi wanafunzi wanaogopa hata
kwenda shule maana njia zote ambazo wanafunzi huwa wanapita kwenda shule ndio
njia ambazo kwa sasa tembo ndio maeneo ambayo wanashinda kutafuta chakula na
wameweka makazi yao” alisema Mihayo
Kwa ujumla mwaka huu hadi hivi
sasa Tembo hao wameshafanya uharibifu wa mazao katika kata ya Ilolo Mpya,Nzihi
na kata ya Kiwele na kuwaacha wananchi wasijue cha kufanya kutokana na kuwepo
kwa Tembo hao.
Kwa upande afisa maliasilia wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Evidence Machenje alisema kuwa serikali
imejipanga kuhakikisha wanawavuna Boko kutokana na taratibu na sheria za
wanyama pori hivyo tayarai wamewasilisha taarifa hizo kwa wizara na wanasubiri
majibu kutoka wizarani.
“Ni kweli tunataarifa za athari
zinazotokana na Boko hao hivyo sisi kama halmashauri hatuna mamlaka ya kuwavuna
wanyama hao hivyo ni lazima tuwasiliane na mamlaka husika ili waje wafanyae
utalamu wao ndipo lije swala la uvunaji wa Boko hao” alisema Machenje
Aidha Machenje amekili kuwa Tembo
na Boko wamefanya uharibifu mkubwa na kuleta madhara makubwa kwa wananchi
lakini kila kitu kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo
wananchi wanatakiwa kuwa na subira muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa tayari kimefanyiwa
kazi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya wanyama hao yanatafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya wananchi
Hata mimi ni mwadhirika kwenye kata yangu kwa Tembo kuaribu mazao ya wananchi hiki kitendo kinakera hivyo wataalam naombeni fanye haraka kuwasiliana na mamlaka husika kutatua tatizo hilo
Thursday, May 9, 2019
DHAHABU ILIYOUZWA SIKU 4 YAIZIDI ILIYOUZWA MWAKA MZIMA - SOKO LA MADINI LABAINI
SOKO jipya la Madini jijini Mwanza tayari limekwisha zinduliwa, naye Waziri wa Madini Dotto Biteko ndiye aliyesimamia hafla fupi iliyofanyika katika jengo maarufu la kibiashara Afrika Mashariki Rock City Mall ambapo tayari ametangaza kufutwa kwa kodi zilizokuwa kandamizi kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiasha wa madini.
Akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza (John Mongella ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) Waziri Biteko, amesema athari za faida za masoko ya madini tayari zimeanza kuonekana nchini kwani katika kipindi kifupi mathalani wilaya ya Chunya ambayo ilikuwa inaongoza kwa utoroshaji wa madini ya dhahabu ndani ya siku 4 tangu soko lake kuanzishwa imeuza Kilogram 22 ambazo hapo awali zilikuwa hazifikiwi hata kwa mauzo yake ya mwaka. Kwani hapo awali kwa mwaka, Chunya ilikuwa inauza kilogramu 12 tu ....ambazo zilikuwa zikipita katika mfumo wa uuzaji wa Serikali ........ Faida moja wapo Yya masoko hayo ya madini ni pamoja na kuzuia uuzwaji wa madini kiholela na kwa njia ya magendo, ambapo awali watu walikuwa wakichimba na kuvuna madini mbalimbali nchini Tanzania na kisha kuyakimbizia nchini za jirani kama vile Kenya ama Uganda nako ndiko walikuwa waki yaboresha katika thamani na kuyatambulisha kana kwamba yametoka kwenye nchihizo hali ambayo ilikuwa ikiishusha Tanzania kwenye takwimu za soko la madini la dunia.....
DKT. APUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE
Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi umezikwa katika makaburi ya familia yao yaliyopo nyumbani kwa wazazi wake, Nkuu, Machame, wilayani hai mkoani Kilimanjaro, leo Alhamisi, Mei 9, 2019.
Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuhudhuria ibada hiyo, polisi walilazimika kufunga barabara zote ambazo zinaelekea kwenye kanisa hilo.
Safu ya waombolezaji imeongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la nchi hiyo Job Ndugai.
Mapema asubuhi saa tatu kanisa lilikuwa limejaa, na nje pia kulikuwa pamefurika. Baadhi ya waombolezaji walipata nafasi ya kuaga mwili ndani ya kanisa lakini ilifika mahala hatua hiyo ilisitishwa ili ibada na hotuba zitolewe.
Mwili ulitolewa kanisani kwa safari ya mwisho ya makaburini saa tisa na nusu. Na shughuli za mazishi zilikamilika saa 11 na nusu.
ASKOFU SHOO AWAONYA VIONGOZI
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Mkuu Dk. Ferdinand Shoo amewaonya viongozi wa Tanzania na kuwataka watumie nafasi zao kuwasaidia wengine hasa wale wenye uhitaji.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa mahubiri kwenye ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP, Dkt. Reginald Mengi iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi mjini.
Amesema kuna watu wakipata vyeo ama utajiri kidogo tu, wanatumia nafasi zao kunyanyasa wengine na akaonya Watanzania wasie wepesi wa kuhukumu, kunyanyasa wengine au kubagua wengine.
Katika mahubiri yake, Dk. Shoo amesema kama kuna dhambi ambayo binadamu anapaswa kuifanyia toba ni ile ya kubaguana na kama Watanzania wanahitaji Taifa lipokee baraka kutoka kwa Mungu, ni vema wakaacha kufanya hivyo. Amesema dhambi nyingine inayopaswa kufanyiwa toba ni ile ya watu wenye nafasi kuwakanyaga wengine.
“Ndugu zangu tukiwa na cheo, tukiwa matajiri, tukiwa na uwezo tuvitumie kuwasaidia wengine, tuache ubinafsi, tuache kiburi, tuache kujitutumua hasa kwa viongozi wa umri mdogomdogo. Kuna mahali mmefika mnajitutumua kama chatu, acheni kabisa. Naomba tuwe unyenyekevu ndugu zangu.”
Ameendelea kwa kusema, “Wale wanaopata utajiri, acheni kukumbatia mali zenu, toeni na kuwasaidia wenye uhitaji kwani mnapata satisfaction kwa kufanya hivyo. Huu ni ujumbe kwetu sote na Mungu atusaidie tulishike hili. Muendelee kuiombea familia na yale mazuri mengi tuliyojifunza kwake tukayatende tukayatende, tuyaenzi,” amesema.
DHAHABU ILIYOUZWA SIKU 4 YAIZIDI ILIYOUZWA MWAKA MZIMA - SOKO LA MADINI LABAINI
VIDEO YAJA HIVI PUNDE
Soko la Madini jijini Mwanza tayari limekwisha zinduliwa mkoani Mwanza, naye Waziri wa Madini Dotto Biteko ndiye aliyesimamia hafla fupi iliyofanyika katika jengo maarufu la kibiashara Afrika Mashariki Rock City Mall ambapo amengaza kufutwa kwa kodi zilizokuwa kandamizi kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiasha wa madini.
Kwa mujibu wa Biteko, faida za masoko ya madini zimeanza kuonekana kwani katika kipindi kifupi mathalani wilaya ya Chunya ambayo ilikuwa inaongoza kwa utoroshaji wa madini ya dhahabu nchini ndani ya siku 4 tangu soko lianzishwe imeuza Kilogram 22 ambazo hapo awali zilikuwa hazifikiwa hata kwa mauzo mwaka.
Kwani hapo awali kwa mwaka ilikuwa inauza kilogramu 12 tu ....ambazo zilikuwa zikipita katika mfumo wa uuzaji wa Serikali tizama wizi huo. Audio ndani ya mail.
Faida moja wapo ni kuzuia uuzwaji wa madini kiholela...watu walikuwa wakichimba Tz na kuyakimbizia Kenya na Uganda nako ndiko walikuwa wakiyabrand kwamba yametoka kwao hivyo kuishusha Tz kwenye takwimu za soko la madini la dunia.....
Soko la Madini jijini Mwanza tayari limekwisha zinduliwa mkoani Mwanza, naye Waziri wa Madini Dotto Biteko ndiye aliyesimamia hafla fupi iliyofanyika katika jengo maarufu la kibiashara Afrika Mashariki Rock City Mall ambapo amengaza kufutwa kwa kodi zilizokuwa kandamizi kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiasha wa madini.
Kwa mujibu wa Biteko, faida za masoko ya madini zimeanza kuonekana kwani katika kipindi kifupi mathalani wilaya ya Chunya ambayo ilikuwa inaongoza kwa utoroshaji wa madini ya dhahabu nchini ndani ya siku 4 tangu soko lianzishwe imeuza Kilogram 22 ambazo hapo awali zilikuwa hazifikiwa hata kwa mauzo mwaka.
Kwani hapo awali kwa mwaka ilikuwa inauza kilogramu 12 tu ....ambazo zilikuwa zikipita katika mfumo wa uuzaji wa Serikali tizama wizi huo. Audio ndani ya mail.
Faida moja wapo ni kuzuia uuzwaji wa madini kiholela...watu walikuwa wakichimba Tz na kuyakimbizia Kenya na Uganda nako ndiko walikuwa wakiyabrand kwamba yametoka kwao hivyo kuishusha Tz kwenye takwimu za soko la madini la dunia.....
Wednesday, May 8, 2019
PICHA: MUONEKANO WA MJENGO WA DKT. MENGI MJINI MACHAME.
Muonekano wa makazi ya Dkt. Reginald A. Mengi katika Kijiji cha Nkweseko, Machame mkoani Kilimanjaro. Mwili wa Dk Mengi utalala hapa leo, na kesho ibada ya mazishi itafanyika Usharika wa KKKT, Moshi Mjini, na kisha utazikwa kwenye makaburi ya familia Kisereni, Machame.
HIVI NDIVYO LIVERPOOL ILIVYOISHANGAZA BARCELONA
Liverpool ilionyesha mchezo mzuri katika historia yake baada ya kutoka nyuma na kuilaza Barcelona kwa jumla ya magoli 4-3
Baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 katika uwanja wa Nou camp , Liverpool ililipiza kisasi wakati Divock Origi alipoiweka kifua mbele timu hiyo.
Georginio Wijnaldum alifunga magoli mawili katika dakika mbili ili kusawazisha.
Origi baadaye alifunga goli lake la pili na la nne kwa upande wa Liverpool kutokana na kona iliopigwa kwa haraka ili kukamilisha ushindi mkubwa.
Liverpooll sasa huenda ikacheza dhidi ya Ajax ama Tottenham katika fainali ya kombe la vilabu bingwa mjini Madrid mnamo tarehe mosi mwezi Juni.
Ilikuwa mazingaombwe kwa Barcelona ambao walicharazwa 3-0 na Roma katika mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kutokana na goli la ugenini , baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1.
Lakini kwa Liverpool ilikuwa kumbukumbu nyengine ya matokeo mazuri ya Ulaya ambayo yanafananishwa na ushindi wao dhidi ya AC Milan katika fainali ya 2005 na ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Borussia Dortmund katika uwanja wa Anfield miaka mitatu iliopita.
Ni mara ya kwanza tangu 1986-wakati Barcelona ilipoilaza Gothenburg katika kombe la Ulaya-ambapo timu ilitoka nyuma kwa magoli matatu kushinda nusu fainali ya michuano hiyo.
Baada ya magoli hayo manne mashabiki wa nyumbani walisimama wakiishabikia timu yao katika dakika za mwisho huku wachezaji wa Barca walioshangazwa wakishindwa kujibu mashambulizi ya Liverpool.
Kipenga cha mwisho kilipopulizwa kilileta sherehe kubwa ndani ya uwanja na katija maeneo ya mashabiki.
Liverpool imefanikiwa kutoka nyuma na kushinda katika siku za nyuma , hususana wakati waliposhinda taji lao la tano mjini Istanbul lakini ushindi huu dhidi ya barcelona ndio mkuybwa katika historia ya klkabu hiyo wanapojiandaa kucheza dhidi katika fainali mji Madrid.
Sio mara ya kwanza kwa Barcelona kuadhibiwa kwa kiwango hiki, baada ya kufungwa 3-0 na Roma katika robo fainali mwaka uliopita baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1 hivyobasi wataendelea kusubiri kutinga fainali tangu 2015.
Walichezewa katika kila safu na ijapokuwa walipata fursa kadhaa hawawezi kudai kwamba walihitaji kushinda.
Kulikuwa na kipindi kifupi katika kipindi cha kwanza , wakati mabingwa hao wa La Liga walipoamka na kuanza mchezo wao mzuri na katika kipindi cha dakika tano kipa Allison alimnyima Messi na Phillipe Coutinho huku Jordi Alba akilazimika kutoa pasi wakati ambapo alikuwa amesalia na kipa huyo kucheka na wavu.
Messi ambaye alikuwa mchezaji mwenye kasi kubwa wiki moja iliopita alishindwa kutawala hususan katika kipindi cha pili wakati magoli ya Wijnaldum yalioposawazisha.
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez pia alipotea huku mchango wake ukionekana wakati ambapo alizomwa mara kwa mara na mashabiki ambao walizoea kumuabudu.
Alikuwa na fursa nzuri katika kipindi cha pili , wakati Messi alipompatia pasi nzuri huku Liverpool ikiwa 1-0 usiku huo lakini Allison alikuwa macho na hiyo ndio iliokuwa nafasi ya mwisho wageni hao kutekeleza tishio lolote.
Tuesday, May 7, 2019
AL MANUSURA WATU WAUANE BUSARA ZA MONGELLA ZASEVU SOO LA MEI MOSI.
Sherehe za Mei Mosi kwa mwaka 2019 mkoani Mwanza zilifanyika wilayani Magu, ambako licha ya kuwa na shamrashamra za kupendeza toka kwa watumbuizaji wa vikundi mbalimbali vya sanaa pia burudani nyingine ilitoka kwa fanyakazi wenyewe.
Ilifikia mahala ambapo wafanyakazi nusura watoane roho kisa na mkasa......chungulia kichupa.....
Monday, May 6, 2019
WATENDAJI WATAFUNA MKWANJA WA VITAMBULISHO VYA MACHINGA MWANZA
SERIKALI Mkoani Mwanza Imebaini kuwepo kwa baadhi ya watendaji wa kata na mitaa ambao wameshindwa kufanya uadilifu katika zoezi la kuuza vitambusho vya wafanyabisahara wadogo vilivyotolewa na Rais Magufuli, wakidaiwa kutumia fedha za vitambulisho hivyo kwa matumizi binafsi.
Chanzo cha kubaini mchezo huo mchafu ni kufuatia taarifa za kushtua kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kushika mkia kimkoa katika mauzo ya vitambulisho kwa kukusanya asilimia 20.87 tu ya fedha, licha ya kutajwa kuwa moja kati ya wilaya zenye idadi kubwa ya wafanyabiashara hao wadogo na miundombinu ya kutosha.
Nayo Halmashauri ya wilaya ya Sengerema imeshika nafasi ya saba kwa makusanyo ya asilimia 22.52, Nafasi ya sita imeshikwa na Magu iliyokusanya asilimia 37.05, wakifuatiwa na Buchosa yenye asilimia 44.42.
Nafasi ya nne imekwenda kwa wilaya ya Ukerewe ambayo mpaka sasa imekusanya asilimia 47.88, Kwimba ni ya tatu yenye asilimia 54.28, Halmashauri ya wilaya ya Nyamagana ambayo ndiyo jiji la Mwanza imekamata nafasi ya pili kwa kukusanya asilimia 67.72, wakati Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ikitajwa kuwa ndiyo inayoongoza kwani tayari imekusanya asilimia 80.40 za fedha za vitambulisho hivyo awamu ya pili.
Akiwa ameambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama mkoa, John Mongella ni mkuu wa mkoa wa Mwanza na hapa anaamua kulivalia njuga suala hilo katika kikao hiki kilichofanyika kuanzia majira ya saa moja usiku na kwenda hadi usiku wa manane kikibaini baadhi ya watendaji wa halmashauri kuzifanyia matumizi mengine binafsi fedha hizo za vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vilivyotolewa na Rais Dokta John Pombe Magufuli awamu ya pili...
HII HAPA BEI MPYA YA PAMBA.
Msimu mpya wa ununuzi wa Pamba umezinduliwa rasmi, huku Serikali ikitangaza bei mpya ya shilingi 1200 kwa kilo moja ya zao hilo ikiwa ni ongezeko la shilingi 100 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya shililingi 1100 msimu uliopita.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi bwana Amosi Makala, amesema Serikali imekusudia kuongeza bajeti ya sekta ya kilimo ili kuwahakikishia wakulima kunakuwa na upatikanaji mzuri wa pembejeo na huduma ya ugani kwa lengo la kuongeza tija na mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba(TCB), Marko Mtunga amesema bodi hiyo inatekeleza mikakati ya kuongeza tija kutoka kuzalisha kilo 300 kwa hekari hadi kfikia kilo zaidi ya 1,000.
Amesema licha ya changamoto kadhaa za uzalishaji wa pamba nchini, msimu huu unatarajiwa kuongeza hadi zaidi ya tani 400,000 kutoka zaidi ya tani 200,000 za msimu uliopita.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi bwana Amosi Makala, amesema Serikali imekusudia kuongeza bajeti ya sekta ya kilimo ili kuwahakikishia wakulima kunakuwa na upatikanaji mzuri wa pembejeo na huduma ya ugani kwa lengo la kuongeza tija na mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba(TCB), Marko Mtunga amesema bodi hiyo inatekeleza mikakati ya kuongeza tija kutoka kuzalisha kilo 300 kwa hekari hadi kfikia kilo zaidi ya 1,000.
Amesema licha ya changamoto kadhaa za uzalishaji wa pamba nchini, msimu huu unatarajiwa kuongeza hadi zaidi ya tani 400,000 kutoka zaidi ya tani 200,000 za msimu uliopita.
MWILI WA MENGI WAWASILI NCHINI, MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi umewasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere Dar es salaam kutoka Dubai ambapo alifikwa na umauti Jumatano iliyopita.
Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo amesema mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Tanzania utahifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo baada ya kuwasili.
Siku ya Jumanne, marehemu ataagwa katika viwanja vya Karimjee.
LIPULI YAILIPUA YANGA
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema kuwa malengo ya kuchukua ubingwa wa FA yalikuja katikati ya msimu, kutokana na hali ya timu yao walikuwa wakipambana wasimalize chini ya nafasi ya 10 katika ligi kuu.
Ametoa kauli hiyo mara baada ya kikosi chake kufungwa goli 2-0 na Lipuli FC na kutolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
"Tulipaswa kumaliza Ligi nafasi ya sita au ya saba kutokana na hali ya timu, tukasema tufanye nguvu tusimalize chini ya 10 na hdi leo tunaongoza Ligi" amesema.
Ameendelea kwa kusema, "FA ilikuja katikati ya Ligi, ndio tukasema sio mbaya tunaweza kubeba kikombe cha FA tukaaza kutia nguvu".
MSOLA NDIYE MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA SC.
Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Jana kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es salaam, Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.
MWENGE WA UHURU KUANZA KUIMULIKA MWANZA MEI 14/2019
KWA mara ya kwanza Mwenge wa Uhuru uliwashwa Tanganyika Desemba 9 mwaka 1961. Alexander Nyirenda ndiye aliyepandisha Mwenge juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ishara ya Uhuru na Mwanga.
Mwenge uliwashwa kama ishara ya kuangaza ndani na nje ya nchi kuleta matumaini pale yalipopotea, kuleta upendo kwenye uadui na kuleta heshima kwenye chuki.
Tangu kuasisiwa kwa Mwenge wa Uhuru umekuwa ni utamaduni wa kukimbiza mwenge kila mwaka katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania.
Safari hii mbio za mwenge kwa mkoa wa Mwanza zitaanza tarehe 14 Mei 2019 ambapo Misungwi ndiyo wametunukiwa hadhi ya kuulaki.
Swali linabaki pale tulipoishia....Jeh safari hii ukimulika, atapona mtu?
Sunday, May 5, 2019
BARCELONA YAPATA PIGO...KUELEKEA MCHEZO LIGI YA MABINGWA
Klabu ya Barcelona ipo kwenye wasiwasi wa kuweza kumtumia mshambuliaji wake Ousmane Dembele baada ya kuumia katika mchezo wa La Liga dhidi ya Celta Vigo.
Katika mchezo huo Celta Vigo imeweza kuitandika Barcelona mabao 2-0 kwa magoli ya Maxi Gomez na Iago Aspas.
Kumkosa Dembele ni pigo kwa Barcelona katika kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool.
YANGA MOTO UPAMBIRE'
Yanga SC leo Mei 5 wanaandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya ambao wataiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.
Leo zoezi hilo linafanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi ambapo wagombea kwa nafasi zote walipata fursa ya kuzungumza sera zao na wanachama kupata fursa ya kuuliza maswali.
Nafasi ambazo zinagombewa ni ngazi tatu ya kwanza ni ngazi ya Mwenyekiti, ngazi ya pili ni ya Makamu Mwenyekiti na ngazi ya tatu ni ya Ujumbe wa Kamati Tendaji ndani ya Yanga.
ACT Wazalendo wajivunia kuwa na wanachama wapya laki mbili ndani ya miezi miwili
Na Thabit Hamidu, Zanzibar.
Chama Cha ACT Wazalendo kimesema kinajivunia kupokea wanachama wapya Zaidi ya laki mbili kutoka vyama vya CUF na CCM ndani ya miezi miwili.
Chama hicho kimesema wanachama hao wametoka katika maeneo mbali mbali Tanzania bara na Visiwani tangu kuanzishwa kwa kampeni Shushatanga Pandisha Tanga mnamo Machi 18 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu kiongozi wa Chama hicho Juma Duni Haji wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho katika Maadhimisho ya miaka mitano tangu kuasisiwa kwa Chama hicho.
Duni Haji alisema hatua hiyo ni nzuri na dalili njema ya kufanya vizuri kwa Chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa bara na Kuelekea katika Uchaguzi Mkuu 2020.
“Kwa wale waliojiunga na Chama chetu nachukua fursa hii kuwakaribisha wapenzi wote wa demokrasia na siasa safi kujiunga na chama chetu, karibuni tujenge mwelekeo wa kiasiasa”
Pia alisema dhamira kuu walikuwa nao chama hicho ni kujenga siasa ambazo zenye kufuata misingi ya utu, uzalendona uadilifu na kupinga rushwa na ufiusadi.
“Tumedhamiria kuona rasilimali za Nchi zinatumika vizuri kutokkomeza umasikini na kujenga taifa linalojitengegemea na kufanya siasa za uadilifu.
Alisema Chama hicho kinawajibu mkubwa wa kihistoria wa kuitoa ccm madarakani ifikapo 2020 kwa upande wa Zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Duni alifahamisha kuwa Chama cha ACT Wazalendo kimeazima kuchukua dola kutokana na CCM kushindwa kuendesha Nchi kutokana kuongoza kwa Mabavu na siasa mbovu.
Hata hivyo aliwashukuru wanachama wa Chama hicho kuwa nao katika kipindi cha miaka mitano tangu kuasisiwa kwa chama hicho.
“Ni kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwa ACT Wazalendo ambapo lengo lake lilikuwa kulete siasa safi zilizojikita kwenye kuwakomboa wananchiwate” Alisema Duni Haji.
Aidha aliongeza kuwa ACT Wazalendo haikuzaliwa kwa bahati mbaya wala kuongeza idadi ya vyama vya siasa bali kimeanzishwa kwa malengo binafsi.
SAA ZAHESABIKA MILANGO YA SOKO LA MADINI MWANZA KUFUNGULIWA
JUMATANO ya Tarehe 8 Mei 2019 Uzinduzi wa soko la madini kwa mkoa wa Mwanza unafanyika rasmi.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella Jumamosi ya tarehe 04 mwezi Mei 2019 imezuru katika eneo hili maarufu la kibiashara na lenye biashara mbalimbali, Rock City Mall jijini hapa kujiridhisha na kukagua mazingira ya mahala palipotengwa kwaajili ya soko hilo.
Licha ya soko hilo kutumika kama nyenzo ya kukuza uchumi wa taifa pia linatarajiwa kufungua fursa za kiuchumi kwa mkoa, likihusisha wadau wote walio kwenye mnyororo wa biashara ya madini wakiwemo Wanunuzi, Wauzaji, TRA, Tume ya Madini, Benki na Mamlaka ya Serikali za mitaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)