ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 5, 2019

ACT Wazalendo wajivunia kuwa na wanachama wapya laki mbili ndani ya miezi miwili




Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Chama Cha ACT Wazalendo kimesema kinajivunia kupokea wanachama wapya Zaidi ya laki mbili kutoka vyama vya CUF na CCM ndani ya miezi miwili.

Chama hicho kimesema wanachama hao wametoka katika maeneo mbali mbali Tanzania bara na Visiwani tangu kuanzishwa kwa kampeni Shushatanga Pandisha Tanga mnamo Machi 18 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu kiongozi wa Chama hicho Juma Duni Haji wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho katika Maadhimisho ya miaka mitano tangu kuasisiwa kwa Chama hicho.

Duni Haji alisema hatua hiyo ni nzuri na dalili njema ya kufanya vizuri kwa Chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa bara na Kuelekea katika Uchaguzi Mkuu 2020.

“Kwa wale waliojiunga na Chama chetu nachukua fursa hii kuwakaribisha wapenzi wote wa demokrasia na siasa safi kujiunga na chama chetu, karibuni tujenge mwelekeo wa kiasiasa”

Pia alisema dhamira kuu walikuwa nao chama hicho ni kujenga siasa ambazo zenye kufuata misingi ya utu, uzalendona uadilifu na kupinga rushwa na ufiusadi.

“Tumedhamiria kuona rasilimali za Nchi zinatumika vizuri kutokkomeza umasikini na kujenga taifa linalojitengegemea na kufanya siasa za uadilifu.

Alisema Chama hicho kinawajibu mkubwa wa kihistoria wa kuitoa ccm madarakani ifikapo 2020 kwa upande wa Zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Duni alifahamisha kuwa Chama cha ACT Wazalendo kimeazima kuchukua dola kutokana na CCM kushindwa kuendesha Nchi kutokana kuongoza kwa Mabavu na siasa mbovu.

Hata hivyo aliwashukuru wanachama wa Chama hicho kuwa nao katika kipindi cha miaka mitano tangu kuasisiwa kwa chama hicho.

“Ni kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwa ACT Wazalendo ambapo lengo lake lilikuwa kulete siasa safi zilizojikita kwenye kuwakomboa wananchiwate” Alisema Duni Haji.

Aidha aliongeza kuwa ACT Wazalendo haikuzaliwa kwa bahati mbaya wala kuongeza idadi ya vyama vya siasa bali kimeanzishwa kwa malengo binafsi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.