ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 21, 2015

KWAAJILI YAKO...

“A Hungry Man Is Always An Angry Man”….Bob Marley(1945-1983) 
Haya ni maneno ya kifalsafa yaliyowahi kutamkwa na gwiji wa muziki wa Reggae hayati Robert Nestar Marley maarufu kama Bob Marley nayaita maneno ya kifalsafa kwa sababu yalilenga kwenye Ulimwengu halisi aishio mwanadamu, kwa maana ya Kiswahili kauli hii yaweza kusemwa kuwa “mtu mwenye njaa mara zote huwa na hasira”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA KIGANGO CHA MT. DOMINIC SAVIO TEMEKE MIKOROSHINI, DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na kuongoza matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na kuongoza matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na mwakilishi wa Askofu Titus Mdoe, Padri Mushi (mwenye kanzu nyeupe) na baadhi ya viongozi wa Kanaisa wakati alipowasili eneo la mwisho wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Saa yenye picha yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya matembezi hayo, Paroko wa Parokia ya Chang’ombe, Benedict Mushi, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa na Msanii, Florian Ludovic (hayupo pichani) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya matembezi hayo, Paroko wa Parokia ya Chang’ombe, Benedict Mushi, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini,  matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.  Picha hiyo iliuzwa kwa mnada kiasi cha Sh. Milioni 2.5. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na kumpongeza, msanii aliyechora picha yake, Florian Ludovic, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Picha hiyo iliuzwa kwa mnada kiasi cha Sh. Milioni 2.5. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mzee Thomas Wambura Kyangombe (miaka 99) baada ya kushiriki matembezi hayo ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.  Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja yam zee Thomas Wambura Kyangombe (miaka 99) na mtoto mdogo kuliko wote walioshiriki matembezi hayo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo na wanakamati wa uchangiaji wa ujenzi huo. Picha na OMR 

'KING CLASS MAWE' APOTEZA MCHEZO WA KWANZA NAMIBIA

BONDIA IBRAHIMU CLASS ;King Class Mawe' mwenye rekodi ya namba moja nchini Tanzania na ni namba 216 kwa Dunia  amepoteza mpambano wake wa kwanza nchini namibia kwa kupigwa kwa pointi na bondia Julius Indongomwenye rekodi ya Namibia na namba moja na duiani ni namba 76 kwa ubora.
 Mpambano uho uliofanyika march 20 Windhoek Country Club Resort, Windhoek, Namibia
ulianza kwa kasi ya ajabu ambapo bondia Class alimkalisha chini Indongo na kuhesabiwa na mpambano kuendelea kwa mashambulizi ya zamu kwa zamu kila upande
hata hivyo mpaka mwisho wa mchezo Class alipoteza mpambano uho kwa point

Mpambano huu ni wa pili kwa Class kucheza nje ya nchi baada ya ule wa kwanza kupigana nchini Zambia mwaka jana na kurudi na ubingwa wa WPBF Africa

Kabla ya kuchaguliwa kwenda kupigana nchini Namibia Class alimdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa mkanda wa U.B.O Africa na kumfanya amiliki mikanda miwili ya Africa mpaka sasa 

Mpambano huu anaupoteza baada ya miaka mitano iliyopita kuwapiga mabondia mbalimbali Class anaenolewa na jopo la makocha linalongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro pamoja na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye umpa ushauli anapokuwa uringoni jinsi ya kukabiliana na mpinzani anaecheza nae

ANOTHER MAKAMUZI YA SUPER KAMANYOLA AT VILLA PARK MWANZA.

Weeee....!!
Safu ya mbele mabibi na mabwana.
Sistaz.
Sutumukaa.
Ngadu kwa ngudu....!!
Shika kamata.
Bass guitar.
Keyboardiste.
Vwaala
Kamata shikaaa.
Wow..na Super Kamanyola.
Kamatisha.
Burudani inaendelea toka stage la Villa Park Mwanza.
Meneja Rama UpoOOoo!!

KENYA AIRWAYS YAPUNGUZA SAFARI ZAKE TZ

CHANZO/BBC SWAHILI
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14.
Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo.
Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam

KA-UJUMBEzi'


IMETOSHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.

Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani. 

Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.

Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.

Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.

mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.

"Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia"amesma Mdimu.

Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.

Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika "Jhikoman".
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Thursday, March 19, 2015