ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 18, 2010

MAUAJI YA MARA SERIKALI YAONESHA MAKUCHA YAKE.

MIILI YA WATU WALIOUAWA KIKATILI KIJIJI CHA BUHARE NJE KIDOGO YA MKOA WA MARA.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH. LAWRANCE MASHA LEO MCHANA AMETEMBELEA ENEO YALIPO TOKEA MAUAJI YA KUTISHA YA WATU 17 WA FAMILIA MOJA KTK KIJIJI CHA BUHARE MKOANI MARA. PICHANI NI SEHEMU YA KIJIJI CHA BUHARE YALIPOTOKEA MAUAJI.
PAMOJA NA KUWAPA POLE WAFIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIFIKA ENEO LA MAKABURI NA KUWEKA SHADA LA MAUA KAMA HESHIMA KWA WATU WALIOUAWA.
MH. MASHA AMEWATAKA WANAUKOO HUO KUTOLIPIZA KISASI KWANI KWA KUFANYA HIVYO WATAENDELEZA WIMBI LA MAUAJI SAMBAMBA NA WAO KUTAMBULIWA KAMA WAUAJI.
WAZIRI AMESEMA JESHI LAKE HALITOLALA, LITATUMIA MBINU ZOTE KUWASAKA POPOTE PALE WALIPO WALIOFANYA MAUAJI HAYO NA KUWATIA NGUVUNI ILISHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Wednesday, February 17, 2010

ETI KAMIS KETU KIMEO?


TUKIO LA MISS TANZANIA 2009 2010 MIRIAM GELARD KUKAMATWA, KUPANDISHWA KIZIMBANI KISHA FASTA FASTA KUPELEKWA RUMANDE KWENYE GEREZA LA SEGEREA DAR ES SALAAM NA HATIMAYE KUACHIWA KWA DHAMANA. SUALA HILI LIMEPOKEWA KWA UZITO MKUBWA, LIKITIZAMWA KWA MAUMIVU MAKALI NA MASWALI MENGI TOKA KWA WAKAZI WA KANDA YA ZIWA HUSUSANI MKOA WA MWANZA ALIKOTOKA. KAMA MDAU WA HABARI NIMETUMIWA SMS NYINGI KAMA MASWALI NA NYINGINE KAMA MAJIBU VILE, NAMI NAZIMWAGA KAMA ZILIVYO...

>>>TATIZO MAMOU\MIRIAM AKIPENDA ANAPENDA KWELI MPAKA ANASAHAU MJUKUMU YAKE KWA TAIFA.
>>>MISS HUYU ANAHISI DUNIA KAIMALIZA KABISA KUMBE HAKO NI KATAITO TU.
>>>NASHAURI ANGEBAKI NA BOY FREND WAKE WA ZAMANI PAUL ALIYEKUWA MSHAURI MZURI KWAKE.
>>>TABIA YA UGOMVI, KIBURI NA UONGO KWA MIRIAM TANGU ZAMANI, UNAKUMBUKA ALIPOMSINGIZIA BOY FRIEND WAKE WA ZAMANI KUWA ALIFIKA KAMBINI MZ AKIWA NA BASTOLA NA KUMFANYIA FUJO ASISHIRIKI MASHINDANO YA MAMISS?
>>>MWONGO ALIDAI NI MWANAFUNZI WA CBE MWANZA NA BADO ANASOMA MBONA HATUMJUI NA MBONA HAJARUDI SHULE KUENDELEA NA MASOMO?
>>>KAMATI YA MISS TZ YOTE KIMEO KUANZIA JUU MPAKA KWA WADHAMINI, SIUNAJUWA WANACHOKITAKA? MIRIAM ALIBANA KUTOA KWA MDAU MMOJA NDO MANA YOTE HAYA YAMEMKUTA TIME IMEFIKA KUWAUMBUA.
>>>OH 'NITAWASAIDIA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU' KWA HALI HII.. MISS TANZANIA KIINI MACHO AKA SANAA TUPU.
>>>DUU EBANA KAKA NIMEJARIBU SANA KUGOOGLE JINA LA HUYU MTOTO WA MAHINA NECTA TENEDU ILI KUPATA MATOKEA YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA SITA BUT SIJAPATA JINA KANA HILO, SASA HAPA SIJUI IMEKAA VIPI? NINA MASHAKA HAJAMALIZA HATA O LEVEL.

NAAHIDI KUZIPITIA SMS ZAKO KIKAMILIFU KISHA KUZIANIKA HAPA....... LAKINI PLIZ TUSIHUKUMU KABLA YA KUHAKIKI.....NITUMIE MAONI YAKO KUPITIA albertgsengo@yahoo.com NAMI NITAFIKISHA.

Monday, February 15, 2010

KWA KHERI BABU CHARLES JEREMIAH.

1933 KUZALIWA KWAKE MZEE CHARLES JEREMIAH (BABU MZAA MAMA) HADI KIFO KILIPOTUTENGA NAYE TRH 9FEB 2010. HAPA NI NDANI YA KANISA LA AICT MALAMPAKA KATIKA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU.
BAADHI YA WAJUKUU WAKE KUTOKA KUSHOTO JEREMIAH MASASI, CELIA KULWA, NA CHARLES MANOTA.
SEHEMU YA UMATI ULIOFURIKA KUHUDHURIA IBADA YA MAZISHI ILIYOFANYIKA KANISA LA AICT MALAMPAKA MASWA SHINYANGA TAREHE 11FEB2010.
FAMILIA INATOA SHUKURANI KWA WALE WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA KUIFANIKISHA SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA MZEE CHARLES JEREMIAH, AKSANTENI KWA SALA.
KUTOKA WILAYA ZA MIKOA YA KANDA YA ZIWA PICHANI NI WAKUU WA ELIMU NGAZI MBALIMBALI.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
WAKIWEKA MASHADA YA MAUA KUTOKA KUSHOTO MR. JULIUS MANOTA, MTOTO WA MAREHEMU SALOME CHARLES *MAMA YANGU MZAZI* NA UNCLE MESHACK.
MIE.