Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akishiriki Ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es Salaam
Saturday, July 5, 2025
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
· Hadi sasa vitongoji 33,657 vimefikishiwa umeme sawa na 52.3%
· Waliofikiwa wasisitizwa kutumia umeme kuibua fursa za kiuchumi
Imeelezwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote Tanzania Bara vitakuwa vimefikishiwa nishati ya umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu Julai 05, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
“Tayari tumefikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 Tanzania Bara sawa na asilimia 100 na sasa hivi ni zamu ya vitongoji, leo hii ninavyozungumza vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359 kote nchini vimefikishiwa umeme ambayo ni sawa na asilimia 52.3,” alisema Mhandisi Olotu.
Mhandisi Olotu aliweka bayana namna ambavyo Serikali imejizatiti katika kuhakikisha umeme unafika katika kila kona ya nchi kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa usimamizi wa REA ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Alisema kuwa vitongoji 30,702 havijafikiwa na umeme, hata hivyo alibainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kupitia miradi inayotekelezwa ya kuhakikisha umeme unafika katika vitongoji hivyo.
“Katika vitongoji ambavyo havijafikiwa; vitongoji 7,736 vipo katika miradi inayoendelea kutekelezwa na vitongoji 22,966 kati ya hivi tumetangaza zabuni kubwa ya kufikisha umeme kwenye vitongoji 9,009 hivyo tutabakiwa na vitongoji 13,957 ambavyo tunatarajia ndani ya miaka mitano navyo vitakuwa vimefikiwa kulingana na upatikanaji wa fedha,” alibainisha Mha. Olotu.
Mhandisi Olotu alitoa wito kwa wananchi katika maeneo yaliyofikiwa na umeme kutumia umeme kuboresha hali ya maisha yao kwa kubuni miradi inayotumia umeme ili kujiongezea vipato vyao badala ya kutumia umeme kwa ajili tu ya mwanga wakati wa usiku.
Amewasihi kuiga mfano wa baadhi ya wananchi ambao wamevumbua fursa katika maeneo yao baada ya kufikishiwa umeme jambo ambalo limeanza kuleta manufaa katika maisha yao ya kila siku.
“Baadhi ya wanufaika tumeshuhudia namna ambavyo wamechangamkia uwepo wa umeme kwenye maeneo yao, tumekuta wanatumia umeme kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo saluni, wamefungua kumbi za kuonyesha sinema na mpira, karakana za kuchomelea na wengine wamefungua biashara ya kuuza vinywaji baridi,” alisema.
Alisema kuwa katika maeneo mengi ya vijiji miji hali ya maisha imebadilika baada ya kufikishiwa umeme kwani fursa za ajira zimeongezeka kutokana na kuibuliwa kwa viwanda vidogo vidogo vingi vya kuchakata mazao.
Friday, July 4, 2025
WATANZANIA WATAKIWA KUACHANA NA DHANA POTOFU KWAMBA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI GHARAMA
Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mha. Jones Olotu (kushoto) akishuhudia upishi wa maandazi kwa kutumia nishati safi ya kupikia Julai 04, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewasihi Watanzania kote nchini kuachana na dhana ya kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni gharama ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.
Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu ametoa rai hiyo Julai 04, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
“Kumekuwepo na dhana kwamba kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo umeme ni gharama ikilinganishwa na kutumia kuni, dhana hii ni potofu haina ukweli kwani sasa hivi teknolojia imeboreshwa,” alisisitiza Mhandisi Olotu.
Alisema kuwa kwa sasa teknolojia imeboreshwa ikilinganishwa na hapo zamani na alisisitiza kuwa hivi sasa yapo majiko ya umeme ambayo yanatumia umeme kidogo.
Alitoa wito kwa wananchi kutembelea Banda la REA ili kushuhudia teknolojia hizo zilizoboreshwa na kujionea kwa vitendo namna ambavyo majiko hayo yanafanya kazi.
“Wananchi watembelee banda la REA kujionea namna ambavyo chakula kinapikwa kwa kutumia nishati Safi ya Kupikia, ladha haibadiliki na pia muda wa kupika ni mchache ikilinganishwa na chakula kinachopikwa kwa kuni ama mkaa,” alisema.
Akizungumzia kuhusiana na uhamasishaji na uwezeshwaji kwa waendelezaji wa teknojia za Nishati safi ya Kupikia, Mhandisi Olotu alisema lengo ni kuwawezesha Watanzania kutumia nishati safi kuepuka madhara ya afya ikiwemo changamoto kwenye mifumo ya upumuaji sambamba na kulinda mazingira.
Alifafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya; kwa mwaka mmoja takriban watu 33,000 hupoteza maisha kutokana na matumizi ya nishati isiyo salama na kwamba REA ni miongoni mwa washika dau wa kuhakikisha idadi ya vifo vinavyosababishwa na athari ya moshi ya kuni na mkaa inapungua.
“Tunataka kuachana kabisa na matumizi ya kuni na mkaa lakini jambo hili linafanyika kwa utaratibu kwani ni ngumu kumbadilisha kila mtu mara moja; inachukua muda na ni hatua kwa baadhi ya maeneo na ndio maana kuna majiko tunasambaza yanayotumia kuni ama mkaa kwa kiwango kidogo,” alisema.
Alisema kwa kuanzia REA ilianza na mpango wa kugawa majiko ya gesi ya kilo sita ambapo mitungi 3,255 na vichomeo vyake yalitolewa kwa kila Wilaya Tanzania Bara kwa bei ya ruzuku ya 50% na kwamba zoezi hili linaendelea.
“Lengo ni kumhamasisha kila mwananchi kuhama kutoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa kuja huku kwenye nishati safi ya kupikia na kwa wale ambao tunaona inachukua muda kubadilika tumewaletea teknolojia inayotumia mkaa kidogo tukitaraji taratibu watahama,” alisema.
Vilevile alibainisha kuwa REA inatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza taasisi zinazolisha Zaidi ya watu mia kutumia nishati safi ya kupikia.
“Tunatekeleza agizo hili la Mhe. Rais tumeanza kuhamasisha na kuwezesha hizi taasisi kuhama ikiwemo Jeshi la Magereza ambapo maeneo 211 yakiwemo magereza 129, kambi za magereza 47, ofisi za mikoa za Magereza 26, nyumba za watumishi wa Magereza, vyuo, shule na hospitali zinasambaziwa nishati safi mbalimbali za kupikia,” alisema.
Alizitaja nishati zilizosambazwa katika taasisi hizo kuwa ni pamoja na mifumo ya bayogesi, mifumo ya gesi ya mitungi (LPG), mifumo ya gesi asilia, mkaa unaotokana na makaa ya mawe na mashine za kutengenezea mkaa mbadala.
Aidha, alisema wakala vilevile unawajengea uwezo Maafisa wa Magereza wapatao 280 kuhusu suala zima la nishati safi ya kupikia.
KIPA WA ZAMANI WA NIGERIA, PETER RUFAI AFARIKI DUNIA
NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, kipa Peter Rufai amefariki dunia leo, Alhamisi ya Julai 3, 2025 akiwa ana umri wa miaka 61.
Hakuna taarifa zaidi juu ya chanzo cha kifo chake, ingawa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limepost taarifa ya kuthibitisha msiba huo na kumuenzi; “Ataishi milele mioyoni mwetu, urithi unaendelea kati ya vijiti na zaidi,”.
Taarifa ya kifo chake Rufai inakuja baada ya kifo cha mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota, aliyefariki mapema leo kwa ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 28.
Alizaliwa Agosti 24, mwaka 1963 Jijini Lagos na aliibukia katika klabu ya Maduka Stationary mwaka 1980 ambako alicheza hadi 1985 alipohamia Femo Scorpions zote za Nigeria.
Mwaka 1986 alikwenda kujiunga na AS Dragons ya Benin iliyomfungulia milango ya kucheza Ulaya baada ya kununuliwa na KSC Lokeren ya Ubelgiji mwaka 1987 ambako alicheza hadi mwaka 1992 akahamia KSK Beveren.

Mwaka 1993 aliondoka Ubelgiji kwenda kujiunga na Go Ahead Eagles ya Uholanzi ambako alicheza msimu mmoja na kuhamia SC Farance ya Ureno hadi 1997 alipokwenda Hispania alikochezea klabu za Hércules Alicante hadi 1999 na Deportivo La Coruña hadi mwaka 2000 akarejea Ureno kudakia Gil Vicente FC.

Ameidakia timu ya taifa ya Nigeria kuanzia mwaka 1981 hadi 1998 baada ya Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Ufaransa akidaka jumla ya mechi 66 na kufunga bao moja.
Mungu ampumzishe kwa amani. Amiin.
LIVERPOOL YAPOTEZA MCHEZAJI KWA AJALI HISPANIA
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Diogo José Teixeira da Silva ‘Diogo Jota’ (28)amefariki dunia Alhamisi ya tarehe 3 June 2025 katika ajali ya gari kaskazini mwa Hispania akiwa safarini na nduguye, Andre (26), ambaye pia ni mwanasoka.Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya A-52, njia muhimu inayotumiwa na madereva kutoka kaskazini mwa Ureno katika jimbo la Zamora.
Jota anafariki dunia wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni, Rute Cardoso mama wa watoto wao watatu, ambaye hivi karibuni katika mahojiano wana habari alimuelezea Jota kama mwanaume mwenye bahati zaidi duniani.
“Tulipokea simu kadhaa katika kituo cha 1-1-2 Castilla y León zikieleza kuwa kulitokea ajali ya gari katika kilomita ya 65 ya barabara ya A-52, katika Manispaa ya Cernadilla, Zamora. Gari liliripotiwa kuhusika katika ajali na lilikuwa likiteketea,” taarifa ilieleza.
“1-1-2 iliarifu Polisi wa Barabara wa Zamora, Kikosi cha Zimamoto cha Baraza la Jimbo la Zamora, na Kituo cha Kuratibu Dharura cha Sacyl (CCU) kuhusu ajali hiyo.
“Kutoka hapo, Kitengo cha Matibabu ya Dharura (UME) na Wahudumu wa Afya kutoka Kituo cha Afya cha Mombuey walitumwa eneo la ajali na wakathibitisha vifo vya watu wawili.”
Habari hii ya kusikitisha inakuja wiki mbili tu baada ya Jota kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Rute Cardoso, katika mji wa Porto.

𝙅𝙤𝙩𝙖 atabaki kwenye mioyo ya wana-Liverpool kwa mchango wake mkubwa kuisaidia timu hiyo kunyakuwa kombe la Ligi kuu ya Uingereza msimu ulioisha 2024-2025 akiisaidia pia timu ya taifa lake Ureno kuisulubu katika fainali Hispania na kutwaa kombe la mataifa ya Ulaya mnamo mwezi 𝙅𝙪𝙣𝙚.
NAIBU WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGHARAMIA MAZISHI WALIOFARIKI SAME
Na Mwandishi Wetu - KILIMANJARO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa kugharamia mazishi ya miili 42 ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali iliyotokea Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.
![]() |
Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.
![]() |
Amesema Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.
Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua sampuli za miili hiyo (DNA) kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.
Hata hivyo Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao.
Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.
Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.
BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO YA DHAHABU YA KIMATAIFA YA UWEKEZAJI KATIKA JAMII KUPITIA CRDB MARATHON
Thursday, July 3, 2025
REA YATOA MKOPO WA KUJENGA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI
Afisa Upimaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Hussein Shamdas akielezea miradi ya Wakala kwa mwananchi aliyetembelea Banda la REA, katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam Julai 03, 2025
REA YAJA NA MPANGO KABAMBE WA KUWEZESHA UJENZI WA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI
· Mkopo wa hadi Shilingi Milioni 133 kwa riba ya 5%-7% kutolewa
· Marejesho ni ndani ya Miaka 7
· Lengo ni kuhakikisha bidhaa za mafuta zinapatikana kwa gharama nafuu
· Wananchi watakiwa kuchangamkia fursa
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mpango wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petrol na dizeli) maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.
Hayo yamebainishwa Julai 3, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Afisa Upimaji wa REA, Hussein Shamdas.
“Katika kuhakikisha nishati bora na salama inapatikana maeneo ya vijijini REA imeendelea kutekeleza majukumu yake ikihakikisha inaandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo mradi huu wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vidogo vya bidhaa za mafuta maeneo ya vijijini,” alisema Shamdas.
Alitaja baadhi ya kadhia inayowakumbuka wakazi wa maeneo ya vijijini kufuatia kutokuwepo kwa vituo vya bidhaa za petrol na dizeli katika maeneo yao kuwa ni pamoja na gharama kubwa za upatikanaji wa bidhaa hizo tofauti na bei elekezi ya Serikali.
Mbali na suala la gharama, Shamdas alisema wakati mwingine bidhaa hizo zimekuwa zikiadimika maeneo ya vijijini kutokana na umbali uliopo kutoka kwenye vituo vya mafuta pamoja na gharama kubwa za usafiri.“Kwa sasa uuzaji na uhifadhi wa bidhaa hizi za mafuta ya petroli na dizeli kwa vijijini sio safi na salama maana wengi wanahifadhi mapipa na madumu ya plastiki ndani ya nyumba jambo ambalo ni hatari linaweza kusababisha mlipuko na kugharimu maisha ya wananchi lakini pia sio salama kwa vyombo vya moto vinavyotumia bidhaa hizo,” alisema Shamdas
Madhara mengine ambayo Shamdas aliyataja ni pamoja na athari za kiafya kutokana na kuvuta hewa isiyo safi na salama kutokana na kuhifadhi bidhaa hizo ndani ya nyumba pamoja, athari za kimazingira zinazotokana na kumwagika kwa kwa mafuta maeneo mbalimbali pamoja na kuikosesha Serikali mapato kwa kuwa wauzaji wengi wa bidhaa hizo vijijini hawalipi kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
“Kwa kutambua athari hizi na kwa kuzingatia malengo ya Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015, ni wajibu wa Wakala kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa nishati na kwa bei nafuu katika maeneo yote ya nchi kwa njia iliyo salama,” alibainisha.Shamdas alitoa wito kwa wananchi kote Tanzania Bara kuchangamkia fursa ya kuomba mkopo huo ili kuweza kujenga na kuendesha vituo vya mafuta ambapo alisema mwananchi atapaswa kujaza fomu maalum na hatua zingine zitaendelea na kwamba mwongozo wa uombaji wa mkopo huo unapatikana kwenye tovuti ya wakaa ambayo ni www.rea.go.tz na pia kwa sasa mwananchi anaweza kutembelea banda la REA na kupatiwa mwongozo.
KADA WA CCM AMIRI MKUFYA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA MLALO
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Amiri Mkufya maarufu kama AMESCO, ni miongoni mwa watia nia Jimbo la Mlalo, ambaye naye amechukua fomu kwa ajili ya kumkabi li Mbunge wa sasa Rashid Shangazi.
Pamoja na kuwa kada, Mkufya pia ni mshindi wa tuzo za Young CEO Round table Africa, Mchumi na msomi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Wednesday, July 2, 2025
MAJALIWA AAMUA KUPUMZIKA UBUNGE "ASANTENI WANA RUANGWA"
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa na Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumuunga mkono wakati wote ambao amekuwa mbunge wa jimbo hilo.
"Imefika wakati kwa mshikamano tulioujenga sasa ni wakati wa kutoa fursa kwa Wana-Ruangwa wengine wapenda maendeleo waweze kuunganisha nguvu hizi ili Kauli mbiu yetu ya Ruangwa kwa maendeleo inawezekana iweze kusonga mbele zaidi."
Aidha, ametoa wito wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya kuwapa ushirikiano wagombea wote wenye nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewasihi Wana-Ruangwa kuendelea kushikamana na itakapofika siku ya uchaguzi waweze kuchagua wagombea wote watakaowakilisha chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo.
"viongozi wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza Dkt. Nchimbi watakapokuja tujitokeze kwa wingi kwenye mikutano tusikilize sera, lakini siku ya kupiga kura tuwapigie kura nyingi za kutosha."
Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Viongozi wakuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumuamini na kumpa fursa ya kuwatumikia wana Ruangwa.
Mheshimwa Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mwaka 2010 na amehudumu kwa kipindi cha miaka 15.
LISSU APINGA SHAURI KUAHIRISHWA TENA, AKUMBUSHIA KESI YA KINA BIBI TITI.
Julai 01, 2025, kesi mbili zinazomkabili Tundu Lissu mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ziliendelea katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam kesi hizo ni ile ya Uhaini na nyingine ya uchochezi ambazo zote zimesikilizwa katika mahakama hiyo.
Kesi ya kwanza iliyoanza ilikuwa ya uhaiani ambayo inamkabili Tundu Lissu na baadaye kesi ya uchochezi ikasikilizwa.BENKI YA CRDB YAANDIKA HISTORIA KUORODHESHA KIJANI BOND SOKO LA HISA LA LUXEMBOURG
Luxembourg, 1 Julai 2025 – Benki ya CRDB imeweka historia kwa kuorodhesha rasmi hatifungani yake ya kwanza ya kijani maarufu kama ‘Kijani Bond’ katika Soko la Hisa la Luxembourg (LuxSE). Hatua hii inaifanya Benki ya CRDB kuwa miongoni mwa benki za kwanza za biashara Kusini mwa Jangwa la Sahara kuorodhesha hatifungani ya kijani iliyotolewa nchini katika soko hilo la kimataifa na pia kuonekana katika Soko la Hisa la Kijani la Luxembourg (LGX), jukwaa linaloongoza duniani kwa masuala ya fedha endelevu.Kijani Bond ilizinduliwa kwa mafanikio nchini Tanzania ikivutia wawekezaji wengi na kukusanya zaidi kwa thamani ya Shilingi Bilioni 171.8 (sawa na Dola za Marekani Milioni 65.7). Kuorodheshwa kwake katika orodha rasmi ya Dhamana za Soko la Hisa la Luxembourg (LuxSE SOL) ni ushuhuda wa kuongezeka kwa mahitaji na uwezo wa Afrika kuwekeza katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi huku ikivutia masoko ya mitaji ya kimataifa.
Hafala ya kuorodheshwa kwa hatifungani hiyo imefanyika katika kwenye makao makuu ya LuxSE, ikihudhuriwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Luxembourg, Bw. Juma Ali Salum, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, Afisa Mkuu wa Biashara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya LuxSE, Arnaud Delestienne, pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Benki ya CRDB, LuxSE na Orbit Securities Tanzania mawakala wa uuzaji wa dhamana hiyo ambayo pia imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema: “Kuorodheshwa kwa Kijani Bond si tu hitimisho la mchakato wa kifedha, bali ni mwanzo wa ushirikiano mpya kati ya Afrika na Ulaya katika kufadhili uchumi wa kijani. Tuna fahari kuwa waanzilishi katika nyanja hii kwa kufanikisha ukusanyaji wa zaidi ya Dola Milioni 65.7 kupitia dhamana yetu ya kwanza ya kijani, ambayo ilispata mafanikio ya zaidi ya asilimia 429. Leo, tunaipeleka safari yetu ya uendelevu katika jukwaa la kimataifa, si kwa ajili ya kupata fedha pekee, bali pia kuinua viwango vyetu vya ufadhili endelevu. Huu ni ujumbe kwa dunia: Afrika ipo tayari kuongoza katika ufadhili endelevu kwa ubunifu, uadilifu, na dhamira ya kweli.”
Kijani Bond ni hatifungani ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania na miongoni mwa kubwa zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa wakati wa kutolewa. Fedha zilizopatikana kupitia dhamana hii tayari zinaelekezwa katika sekta mbalimbali zenye mchango mkubwa kwa maendeleo endelevu ikiwemo: Nishati mbadala, Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, Nishati safi ya kupikia, Majengo rafiki kwa mazingira, Usafiri wa kijani, Maji safi na huduma bora za usafi wa mazingira, pamoja na miradi mingine inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake, Arnaud Delestienne, Afisa Mkuu wa Biashara wa LuxSE, alisema: “Tunafurahia kuikaribisha Benki ya CRDB na hatifungani yake ya kijani katika soko letu. Huu ni ushahidi wa namna masoko ya mitaji ya kimataifa yanavyoweza kusaidia kupata fedha kwa ajili ya huduma muhimu na kuchochea mabadiliko ya kijani barani Afrika. Pia ni uthibitisho wa nafasi ya Afrika kama mshirika muhimu katika maendeleo ya fedha endelevu duniani.”Akitoa salamu kutoka kwa Serikali ya Tanzania, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Luxembourg, Juma Ali Salum, alieleza:
“Tukio hili ni la kujivunia kwa taifa letu na ni kielelezo cha dhamira ya Tanzania katika kushiriki kikamilifu katika ajenda ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kijani Bond ya Benki ya CRDB inaonyesha dhamira ya nchi yetu kuwa mfano wa maendeleo jumuishi na yanayozingatia mabadiliko ya tabianchi.”Benki ya CRDB ikiwa ni taasisi iliyoidhinishwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UN-GCF), inaendelea kujijengea nafasi thabiti kama kiongozi wa ufadhili endelevu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kuorodheshwa kwa Kijani Bond katika Soko la Hisa la Luxembourg kunaiwezesha benki kupanua wigo wake wa kupata mitaji ya kimataifa huku ikiimarisha mchango wake katika kusaidia jitihada za serikali kukuza uchumi wa kijani.
Kupitia dhamana hiyo, Benki ya CRDB tayari imefanikiwa kuwezesha maelfu ya wanawake na vijana kuanzisha na kukuza biashara zao, kusaidia wakulima kutumia mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuboresha maisha ya watu katika jamii mbalimbali nchini Tanzania Kwa taarifa zaidi kuhusu Dhamana ya Kijani ya CRDB Bank, tafadhali tembelea: 🔗 https://www.luxse.com/security/TZ1996105155/416649
Tuesday, July 1, 2025
JOHN NZILANYINGI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA
Tarehe 28 Juni 2025 ILIKUWA siku ya kwanza ya uchukuaji fomu za kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani.
Asubuhi tu ya siku hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Ndg John Nzilanyingi alifika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana na kuchukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama kuwania ubunge Jimbo la Nyamagana kwa uchaguzi Mkuu wa baadaye Octoba mwaka huu.
ENDELEA KUTUFUATILIA TUKIKUPA DATA MBALIMBLI KUELEKEA UCHAGUZI HUO.
MCHAFU ATUA KUCHUKUA FOMU KUTETEA KITI CHA UBUNGE VITI MAALUMU PWANI
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
KADA WA CCM MACRINA AJITOSA UBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA TANGA
KADA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Macrina Clemens (kulia ) akikabidhiwa fomu na Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Anastazia Aman
Na Mwandishi Wetu,TANGA.
KADA wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Macrina Clemens amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge wa viti Maalumu Mkoa huku akihaidi kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu alisema ameamua kuchukua fomu ili kuweza kutoa mchango wake kwa wananchi hususani Jumuiya wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Tanga.
Zoezi la kuchukua fomu limeanza katika ofisi za Chama cha Mapinduzi linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.
Monday, June 30, 2025
MIAKA MITANO MFULULIZO PAREDI LA YANGA LIMEKUWA LIKIPITA MSIMBAZI NA KOMBE
Ni miaka mitano sasa tena mfululizo, klabu ya Yanga imeendelea kuwatesa watani zao Simba kwa kunyakuwa idadi kubwa ya mataji, ambapo msimu wa 2024-2025 ndiyo imekuwa kufuru zaidi, baada ya kufanikiwa kuvitia kibindoni vikombe vyote.
Mapema hii leo klabu hiyo ya Jangwani paredi la kihistoria lililo wang'aoa mashabiki wake wa viunga mbalimbali kujumika nao kila hatua walizosonga.
Katika msafara huo wa Yanga, bodaboda wamepata fursa ya kubeba mashabiki kwa kujipatia kipato, kutoka kwa mashabiki ambao wamechoka kutembea na kuamua kutumia usafiri huo.
Kutokana na msafara kuwa na magari mengi yanayotembea taratibu, kumekuwa na foleni, inayosababisha bei kuchangamka.
Pamoja na bei wanazotajiwa haionekani kuwasumbua mashabiki waliojawa na shangwe ya kusherehekea ubingwa wa msimu huu, ukiwa wa mara 31 tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.
Haijafahamika ni kiasi gani wanatoa kukodi usafiri huo ambao umetawaka kwenye msafara wa sherehe za ubingwa wa Yanga.
Yanga inatembeza mataji matano iliyotwaa ndani ya msimu wa 2024-2025 likiwamo Kombe la Toyota ililotwaa Afrika Kusini, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ililotwaa usiku wa jana Jumapili kwa kuifunga Singida Black Stars kwa mabao 2-0.
Katika fainali hiyo ikliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Dube Abuya na Clement Mzize na kuipa Yanga taji la nne mfululizo la michuano hiyo na la tisa kwa ujumla tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1967.































.jpeg)
.jpeg)



.jpg)



