ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 4, 2025

LIVERPOOL YAPOTEZA MCHEZAJI KWA AJALI HISPANIA

 


MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Diogo José Teixeira da Silva ‘Diogo Jota’ (28)amefariki dunia Alhamisi ya tarehe 3 June 2025 katika ajali ya gari kaskazini mwa Hispania akiwa safarini na nduguye, Andre (26), ambaye pia ni mwanasoka.

Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya A-52, njia muhimu inayotumiwa na madereva kutoka kaskazini mwa Ureno katika jimbo la Zamora.

Jota anafariki dunia wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni, Rute Cardoso mama wa watoto wao watatu, ambaye hivi karibuni katika mahojiano wana habari alimuelezea Jota kama mwanaume mwenye bahati zaidi duniani.


“Tulipokea simu kadhaa katika kituo cha 1-1-2 Castilla y León zikieleza kuwa kulitokea ajali ya gari katika kilomita ya 65 ya barabara ya A-52, katika Manispaa ya Cernadilla, Zamora. Gari liliripotiwa kuhusika katika ajali na lilikuwa likiteketea,” taarifa ilieleza.

“1-1-2 iliarifu Polisi wa Barabara wa Zamora, Kikosi cha Zimamoto cha Baraza la Jimbo la Zamora, na Kituo cha Kuratibu Dharura cha Sacyl (CCU) kuhusu ajali hiyo.
“Kutoka hapo, Kitengo cha Matibabu ya Dharura (UME) na Wahudumu wa Afya kutoka Kituo cha Afya cha Mombuey walitumwa eneo la ajali na wakathibitisha vifo vya watu wawili.”

Habari hii ya kusikitisha inakuja wiki mbili tu baada ya Jota kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Rute Cardoso, katika mji wa Porto.

Moja kati ya posti zake za mwisho katika Instagram zilionesha baadhi ya matukio muhimu ya sherehe yake ya harusi iliyofanyika Tarehe 22 𝙅𝙪𝙣𝙚 2025

𝙅𝙤𝙩𝙖 atabaki kwenye mioyo ya wana-Liverpool kwa mchango wake mkubwa kuisaidia timu hiyo kunyakuwa kombe la Ligi kuu ya Uingereza msimu ulioisha 2024-2025 akiisaidia pia timu ya taifa lake Ureno kuisulubu katika fainali Hispania na kutwaa kombe la mataifa ya Ulaya mnamo mwezi 𝙅𝙪𝙣𝙚.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment