|
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Sebastian Maganga (kulia) akifafanua jambo leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari, kuhusiana na Tamasha hilo litakalo funguliwa rasmi mwaka huu jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba jumamosi hii. |
Baada ya kupatikana kwa mshindi wa Super Nyota na washindi wa Dance la Fiesta ambao wote walipatikana jana kwenye ukumbi wa Jembe ni Jembe Beach Resort leo wasanii mbalimbali wameongea na waandishi wa habari.
Wasanii hao ni wale ambao wataperfoam kesho waliofika ni pamoja na Ney wa Mitego,Young D,Mr.blue,Barakah Da Prince,Chegge na Temba,Madee,Makomando,Stamina,Young Killer,Vanessa Mdee na wengine kibao.
Miongoni mwa wasemaji wa mkutano huu na waandishi wa habari ni pamoja na Mwenyekiti wa shamrashamara za Serengeti Fiesta Sebastian Maganga ambaye amesema kuwa sababu ya kuanza kwa Serengeti Fiesta kwa mkoa wa mwanza ni kama watu wana kumbukumbu mwaka 2004 Serengeti Fiesta ya kwanza kutoka nje ya Dar ilikua ni ndani ya jiji la Dar ambayo ilikua na kauli mbiu ya Utamaduni unaendelea.
Kwa miaka 10 hii kwa sasa wameweza kushuhudia namna ilivyosambaza upendo ambayo imewajumuisha wasanii wadogo na wakubwa na safari hii Serengeti fiesta imeongeza miji na itakuwa miji 18 badala ya 14 ya mwaka jana.
Hizi ni baadhi ya picha za mkutano huo.