ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 9, 2022

MLINZI WA CHUO AIBA GARI KWENYE MAEGESHO YA CHUO.

 

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 kwa kuiba gari aina ya raum rangi ya Grey yenye namba za usajili T 702 DFV mali ya Gasper Abraham mwenye umri wa miaka 34 aliloiba katika eneo lake la kazi

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa wamemkamata kijana huyo baada ya taarifa za kuibiwa kwa gari hilo kutolewa na hivyo kupelekea jeshi la polisi kufanya doria ya kutosha na kuikuta wilaya ya kilolo mkoani hapa

“Tunamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 mlinzi wa RUCU aliiba gari hiyo ikiwa kwenye maegesho lakini mmiliki alitoa taarifa kwenye jeshi la polisi na ndipo utaratibu wa kumtafuta ukaanza ndipo ilipokutwa kwa mtuhumiwa akiitumia wilaya ya kilolo “

Pamoja na hayo Allan Bukumbi alisema  kuwa  miongoni wa waharifu waliofanikiwa kuwakamata katika  msako walioufanya  walifanikiwa kumkamata ndugu Boni Kipalile kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu moja ikiwa chemba huku wakimshikilia benadetha kipago umri wa miaka 61 akiwa na meno ya tembo na kiboko

“Ndugu waandishi wa habari kutokana na taarifa za siri kijiji cha kiponzero wilaya ya mkoa wa Iringa tulifanikiwa kumkamata boni kipalile mkulima mkazi wa igangidungu anayetuhumiwa kujihisuisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akizwa na silaha moja aina ya shortgun namba za usajili 14949na risasi tatu moja ikiwa chemba pamoja na hilo tunamshikilia benedetha kipago kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na meno mawili ya kiboko “

Aidha kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Iringa amewataka wananchi kujitokeza na kutambua mali zilizokamatwa kwa watuhumiwa Emmanuel Mnyeke (28) na Alfred Mkanula (25) ambao walikamatwa na mali za wizi ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina ya sanlg ,boxer na honda

Katika kushighulikia changamoto mbalimbali jeshi la polisi mkoani iringa lilifanikiwa kumkamata Sebastian Mahuwili (42) aliyehukumiwa kwa kesi ya kubaka mtoto wa miaka 6 na hivyo kupelekea Kufungwa miaka 30 jela kutokana na ushahidi kukamilika.

Thursday, December 8, 2022

HAPPY BIRTHDAY BOBWHITE PAMBA 'MMOJA TU DUNIA NZIMA'


Tarehe 9 December siku ya Maadhimisho ndio kazaliwa mnyamwenga mwenyewe, mbishi town, wakuitwa 'Kichwa cha Burudani' aka BOB WHITE PAMBA.

Sifa ni nyingi muda mchache jamani.

#Mwanza

KAMA NI MASSAGE UKIWA JIJINI DODOMA JIBU NI - THE CAPITAL PARK BARBER SHOP

 Mwambie rafiki awaambie marafiki, Huduma hapa ni full kiwango mwanawane, 'HUTOJUTIA PESA YAKO'

#dodoma #jijiniDodoma #massagetherapy

MAMA NA BINTI YAKE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTOA MIMBA.

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye nyumba ya huyo mama kwa ajili ya kujiridhisha taarifa za tuhuma za kutoa mimba kwa binti wa mama huyo

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye nyumba ya huyo mama kwa ajili ya kujiridhisha taarifa za tuhuma za kutoa mimba kwa binti wa mama huyo
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye nyumba ya huyo mama kwa ajili ya kujiridhisha taarifa za tuhuma za kutoa mimba kwa binti wa mama huyo


Na Fredy Mgunda, Iringa.

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Egria Ngalawa kwa tuhuma za kumtoa mimba binti yake mwenye umri wa miaka 17 na kufukia kichanga Kwenye banda la kufugia nguruwe lililopo nyuma ya nyumba yao katika mtaa wa Bomba mbili kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa.

 

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo anasadikika kutenda kosa hilo wiki moja iliyopita kwa mujibu wa taarifa alizopokea kutoka kwa raia wema.

 

Moyo alisema kuwa jeshi la polisi wilaya ya Iringa pia linamshikilia kwa mahojiano binti anayesadikiwa kutoa mimba hiyo  na kushrikiana na mama yake kufukia kichanga hicho Kwenye banda la kufugia nguruwe.

 

Kiongozi huyo wa kamati ya ulinzi na usalama Iringa akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kwa mujibu wa mahojiano Kati ya jeshi la polisi na watuhumiwa hao,inaelezwa kuwa mama wa binti huyo aliwahi kuitwa shuleni alipokuwa akisoma binti huyo nakutaalifiwa mwanae ni mjamzito.

 

Hata hivyo mama huyo amekana kuhusika kumtoa mimba binti yake na kufukia kichanga,akieleza kuwa Amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara ya binti yake kujihusisha kimapenzi na na wanaume za watu mtaani hapo.

 

Kwa upande wake binti huyo amekana kutoa mimba na kueleza kuwa hakuwahi kuwa na ujauzito wowote kwa kipindi hicho.

 

Aidha kulingana na maelezo hayo jeshi la polisi kwa kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii limeanzisha uchunguzi wa kisayansi ili kubaini kama binti huyo anakuwa na ujauzito za siku za hivi karibuni na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitafuata.

 

Tukio hilo limeibuliwa ikiwa Leo ni siku ya kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatilii ambapo mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametumia jukwaa la maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Ikuvilo kukemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea wilaya humo huku akiwataka wananchi kupaza sauti kuwafichua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichuliwe dhidi yao.

 

Moyo aliwaoonya viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata kuacha tabia za kumaliza kiholela kesi za ukatilii ikiwemo ubakaji na ulawiti huku akisisitiza yeyeto atakayebainika kufanya hivyo anafunguliwa mashtaka na serikali.

MAFIA WAFANYA KWELI WAADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU KWA KISHINDO KWA KUPANDA MITI NA MAKONGAMANO.

Na Victor Masangu,Pwani 

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhandisi Martin Ntemo ameongoza wananchi kuamua kuadhimisha sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kupanda miti na kushiriki kwenye Kongamano ambalo lilikuwa maalum kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili walimu wanawake pindi wanapotekeleza majukumu yao.


Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba Kongamano hilo limefanyikia katika ukumbi wal CARITAS na kuratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Action Aid ambapo pia kulifanyika zoezi la kupanda miti katika eneo kinapojengwa Chuo cha VETA. 

Ailisema kuwa katika zoezi la upandaji miti lilihitimishwa katika eneo inapojengwa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Ndagoni kisiwani Mafia lengo ikiwa ni kuboresha mazingira katika shule hiyo.


Akizungumza  katika kongamano hili mkuu huyo wa Wilaya  alieleza kuwa ratiba hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mikoa na wilaya zote kuadhimisha sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kuandaa makongamano.

"Tumepokea maagizo ya Rais wetu ya kuadhimisha sherehe za miaka 61 ya uhuru katika kuandaa makongamano lakini pia kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii na sisi katika Wilaya ya mafia tumetekeleza hilo,"alisema Ntemo.

Picha za matukio mbali mbali ya baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mafia wakifanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo kupanda miti na kufanya kongamano ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru.

Akifafanua zàidi alisema kwamba ratiba hiyo ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara itaendelea kwa mashindano ya mashule kwa upande wa mashairi na ngonjera lakini pia itahusisha mashindano ya michezo mbali mbali kabla ya siku ya kilele ambayo ni tarehe 9 Desemba mwaka huu.


Katika hatua nyingine alibainishwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Mkunguni kwa ajili ya kukutana na wananchi,wadau wa maendeleo ili kujadili mambo mbali mbali.

Tuesday, December 6, 2022

YESU HAKUTAFUTA WATU WAZURI; YESU ALITAFUTA UZURI NDANI YA WATU WABAYA

 


Yesu Hakutafuta Watu Wazuri; Yesu Alitafuta Uzuri Ndani ya Watu Wabaya: Mbinu ya 13 Aliyoitumia Kutoboa.


Denis Mpagaze

_________

Yesu alifanikiwa sana kwa sababu hiyo! Alishughulika na uzuri ulio ndani ya mtu bila kujali mtu huyo ni mzuri au mbaya maana watu wana yote; mabaya na mazuri. 


Katika hili Yesu anatufundisha kushughulika na mazuri yao, mabaya waachie wenyewe.


Sisi tunapoteza muda mwingi kutafuta watu wazuri na kuwakimbia wabaya. Utasikia ukitaka kufanikiwa katika biashara, elimu, ndoa, na ajira Find Good People! Ignore Bad People. Akina hopeless guys!


Mwisho wa siku kila mtu mzuri utakayempata utakuta ana mabaya yake yatakayokunyima hamu ya kushiriki naye katika mapenzi, biashara na kazi.🤭🤭


Unapata mume mwema, mwaminifu lakini hana hela na kumbuka kuna mambo yataendelea kuwa magumu hadi utakapopata hela.


Unapata mwenye pesa, uaminifu sifuri. Haya maisha yanavurugu nyingi!


Unapata fundi mzuri lakini mwizi wa vifaa; unapata fundi mwanifu lakini mbabaishaji.

Katika hali kama hii ni bora kufanya kazi na mtaalam mwizi unaweza kumdhibiti kuliko kufanya kazi na mbabaishaji mwaminifu!


Yesu alijua kabisa Petro atamkana lakini bado hakumny'ang'anya zile funguo za Ufalme wa mbinguni wa kufungia au kufungulia chochete (Matayo 16:13-19). 


Yesu aliona ni upuuzi kupoteza akili kubwa ya msaliti Petro kwa mambo madogomadogo. 


Yesu angekuwa Mzee Athumani, Petro angetumbuliwa siku ileile alipomkana Yesu kwa mara ya kwanza. 


Sisi kumpoteza mtu mwenye akili nyingi kwa sababu ametukosea adabu ni rahisi kama kumsukuma mlevi.


Sikiliza, ni nadra sana kumpata mtu akili na adabu kwa wakati mmoja. Kwakweli ni nadra mno. Mara nyingi watu wenye akili nyingi hawanaga adabu na wale wenye adabu sana ni zero brain. 


Nimesema ni nadra. Nadra haina maana hawapo. Wapo lakini wachache. Labda hoja hapa ni kujiuliza wewe uko kundi gani...


......inaendelea.....vipi una Sh 5,000 ya fasta nikurushie e-book ya Ukombozi wa Fikra Mpesa 0753665484!


Cheers

Mwl. Denis Mpagaze

Muhenga wa Karne ya 21!

Monday, December 5, 2022

MWANA WA OSAMA BIN LADEN AFICHUA MAMBO KUMHUSU BABAKE

Kushoto  Omar Bin Laden na kushoto Osama Bin Laden,
 

Omar Bin Laden mwanawe mwasisi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Osama bin Laden, amefichua taarifa za kushangaza kumhusu baba yake. 


Akizungumza katika mahojiano na gazeti la The Sun, Omar Bin Laden alikiri kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo baba yake alifanya yaliyomkera zaidi. 

Miongoni mwa mambo ambayo alifichua hayakumfurahisha ni kwamba baba yake alifuga mbwa ambao kulingana na dini ya Kiislamu huchukuliwa kama uchafu. 

Omar Bin Laden alisema kuwa babake Osama Bin Laden alifanyia majaribio mbwa wake silaha za kemikali. 


"Niliona (vipimo vya silaha za kemikali vikifanyiwa mbwa, sikufurahia jambo hilo. Nilijaribu kusahau kumbukumbu hizo zote mbaya kuhusu tukio hilo.

 Ni vigumu lakini baada ya muda, utasahau," alisema Omar Bin Laden. 

Kitabu kilichoandikwa kuhusu Osama Bin Laden kinasema kwamba mbwa huyo alikufa ghafla lakini hakuna anayejua kwa nini alikufa. 

Osama bin Laden aliuawa katika operesheni iliofanywa na wanajeshi wa Marekani mjini Abbottabad, Pakistan na mwili wake ulirushwa katika Ziwa la Arabian kutoka kwenye ndege ya Amerika saa kadhaa baada ya kifo chake, ili kuzuia kuundwa kwa kituo cha hija ardhini. 

Hata hivyo, Omar bin Laden ambaye sasa ana umri wa miaka 41, anasema haamini kuwa Marekani ilizika mwili wa babake Osama bin Laden baharini. 

Omar aliishi nchini Sudan na baba yake Osama Bin Laden kuanzia mwaka 1991 hadi 1996 kabla yao kutengana akikiri kwamba alipata mafunzo ya matumizi ya silaha katika kambi za mafunzo za al-Qaeda. 

 Katika kilichoandikwa kuhusu Osama Bin Laden, Omar alisema haikubaliki kwa baba yake kuua raia, na ndiyo maana aliondoka Al-Qaeda. 

Hata hivyo, baba yake hakufurahishwa na uamuzi wake alirejea Saudi Arabia na kuanza biashara mwaka 2006 na baadaye alikwenda Ulaya. 

Osama Mwongo mmoja tangu alipowindwa na kuuawa, Osama bin Laden, bado ana ushawishi mkubwa kwa wanamgambo wa kiislamu hata katika maeneo yenye michafuko ya wapiganaji wa kiislamu. Uso wa Bin Laden bado huwekwa katika T-shirt, jina lake huandikwa nyuma ya magari na vinyago vyake hutumiwa wakati wa maandamano. 

BENKI YA CRDB, VISA WATAMBA KOMBE LA DUNIA.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwa uwanjani kushuhudia mechi ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Poland ikiwa ni sehemu ya mwaliko kutoka Visa International, washirika rasmi wa malipo wa FIFA. Benki ya CRDB imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Visa kupitia mifumo yake ya malipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela (katikati) akiwa na Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (kushoto), na Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa wakati wa mkutano maalum uliondaliwa na kampuni ya Visa International nchini Qatar kujadili ushirikiano katika mifumo mipya ya malipo.
Mwakilishi wa Visa nchini Qatar akielezea juu ya mwenendo wa huduma za malipo na biashara kote duniani katika kipindi cha mwaka 2022

Kampuni ya Visa ambayo ndio mwezeshaji mkuu wa malipo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa), imeikaribisha Benki ya CRDB kushuhudia maboresho ya huduma zake kwenye michuano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Qatar.

Ili kurahisisha malipo kwa mashabiki na washiriki waliohudhuria michuano hiyo, Visa imefanya maboresho kadhaa kuondoa usumbufu kwa wateja wake.

Maboresho yaliyofanyika yanamruhusu mteja anaweza kuidhinisha malipo kwa kutumia sura yake bila kulazimika kutumia kadi au simu baada ya kukamilisha usajili, kutumia kadi za kidijitali pamoja na kulipia teksi kidijitali.

Katika kusherehekea mafanikio hayo, Visa imezialika benki kubwa inazoshirikiana nazo kutoka kila pembe ya dunia huku Tanzania ikiwakilishwa na Benki ya CRDB.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema mashabiki wa mpira nchini ambao wameenda kujionea michukuano hiyo wanaweza kulipia huduma na bidhaa wanazozitaka iwe hotelini, dukani au katika chombo cha usafiri. 

“Michuano hii ya kombe la dunia ni fursa kwa Benki ya CRDB na Visa kuonyesha na kudhihirisha ubora wa huduma zetu za malipo. 

 Kadi zetu za TemboCard Visa zinatumiwa na Watanzania wengi wlaiokuja kushuhudia michuano inayoendelea hapa Qatar,” amesema Nsekela.

Ushirikiano wa Benki ya CRDB na Visa umekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha Watanzania kupata huduma bora za benki hata kushiriki kwenye uchumi wa kidijitali.

Tangu mwaka 2014 ulipoanza kwa kuitambulisha Tembocard Visa, ushirikiano huo umewawezesha Watanzania kupata huduma za fedha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

"Benki ya CRDB inajisikia fahari kuwa mbia wa Visa kuwawezesha mashabiki wa mpira wa miguu kufurahia mchezo huku wakilipa kwa namna rafiki kwa kutumia kadi zetu za TemboCard Classic, Gold, Platinum, na Infinite zenye huduma zinazokidhi mahitaji ya mteja,” amesema Abdulmajid Nsekela. 

Wakati wote, Nsekela amesema benki imekuwa ikitumia juhudi kubwa, kwa kushirikiana na Visa, kuboresha na kuongeza ujumuishaji wa wananchi kwenye huduma za fedha. 

Kutokana na uwezo wake, Nsekela amesema  TemboCard Visa zinaweza kutumiwa kwenye mashine za kutolea fedha (ATM), vituo vya mauzo hata majukwaa ya mtandaoni yanayomruhusu mteja kufanikisha muamala akiwa mahali popote duniani.

"Mpaka sasa tuna zaidi ya wateja milioni 4 wanaotumia huduma kupitia kadi zetu, wengi wanamiliki TemboCard Visa. Malengo yetu ni kuhakikisha mteja anaweza kupata huduma aitakayo kutoka popote alipo na wakati wowote anaoihitaji. 

Mwanzon wateja hawakuwa tayari kufungua akaunti kutokana na ulazima wa kwenda kwenye tawi la benki watakapohitaji kuzitumia fedha zao lakini ushirikiano wetu na Visa umeondoa ulazima huo,” amesema Nsekela akisistiza kuwapo kwa CRDB Wakala nako kumeongeza maeneo ambako wateja wa benki wanaweza kupata huduma.

Kwa sasa kuna zaidi ya CRDB Wakala 25,000 wanaosaidia kufikisha huduma hata maeneo yasiyona tawi huku mifumo ya kidijitali ya benki ikiongeza fursa za kulipia bili za Serikali kwani imezijumuisha zaidi ya taasisi 4,000 za umma. 

Huduma za kidijitali ni kati ya vipaumbele vya Visa hata Benki ya CRDB kwani teknolojia hiyo siyo tu imerahisisha miamala ya wateja bali ukusanyaji mapato kwa mamlaka za serikali. 

Katika kampeni iliyoizindua mapema mwaka huu kuhamasisha uchumi wa kidijiti, wateja wanne wa Benki ya CRDB wanaotumia TemboCard Visa walilipiwa nauli ya ndege na tiketi za kuingia uwanjani kushuhudia mechi za kombe la dunia, visa ya kuingia Qatar pamoja na malazi ili kuwapa nafasi ya kufurahia michuano hiyo inayoendelea kutokana na matumizi ya kadi zao.

Ujumbe wa Benki ya CRDB ulioenda Qatar ulipata fursa ya kutembelea vituo vya ubunifu kama sehemu ya mwaliko wa kuhudhuria michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.

 Vilevile, ulishuhudia mtanange wa makundi uliozihusisha Argentina na Poland, pamoja na ule wa Japan na Hispania.

Sunday, December 4, 2022

RC MALIMA AFURAHISHWA NA BENKI YA NMB KUJIHUSISHA NA KILIMO.


NA ALBERT GSENGO/ MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima ametoa rai kwa benki ya NMB kuendelea kuchangia maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi nchini kupitia huduma za kifedha wanazotoa.

Akizungumza na Viongozi na Mameneja wa benki hiyo waliotoka kanda zote nchini leo Jijini Mwanza, Mhe. Malima amewapongeza kwa kubuni huduma mpya bora za kiushindani wanazozitoa kwa jamii kama zinazowanufaisha wajasiliamali wadogo.

Aidha, Mhe. Malima ameipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma zao kwenda kwenye mifumo ya kidigiti siku hadi siku kwani kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia jambo hilo haliepukiki kutokana na ushindani wa kibenki.

"Faraja yangu kubwa kwenu ni kuona mnajihusisha na Sekta ya Kilimo tena katika nyanja zote za mifugo, uvuvi na ufugaji wa Nyuki sehemu ambazo wananchi wengi wanaendesha maisha yao huko" Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Vilevile, ametoa wito kwa benki hiyo kuborsha huduma za mikopo kwa wajasiliamali na vikundi vya wananchi wanaojihusisha na shughuli ndogondogo za kujitafutia kipato kwa kuweka masharti mepesi kwani wananchi wengi wa kipato cha chini lakini wamekua wakikosa mitaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede amesema Benki hiyo ina mikakati ya kuwafikia wananchi kupitia uwajibikaji wao kwa jamii kwa kuwa sehemu ya Maendeleo yao kwa kuiunga Mkono Serikali kusaidia kwenye utoaji wa huduma mbalimbali kwa kusaidia vifaa kwenye Sekta ya Maji, Elimu na Afya.


"Benki yetu ilianzishwa mwaka 1997 na wakati huo tulikua na Matawi 97 tu nchini lakini sasa tumefikisha 228, tulikua hatuna mifumo ya digitali lakini hivi sasa tuna mifumo mbalimbali na tunashukuru sana Serikali, Wadau na Wateja wetu kwani wametupa faida kubwa hadi kufikia Bilioni 321 baada ya kodi ndani ya robo tatu tu za Mwaka." Kaimu Mtendaji Mkuu NMB,  Filbert Mponzi.

Mkutano huo wa Benki ya NMB umewakutanisha Viongozi na Mameneja zaidi ya 250 kutoka kanda zote nchini wakisherehekea kwa pamoja kuwa na tuzo 18 ndani ya mwaka mmoja kwa utoaji wa huduma mbalimbali kwa ubora mkubwa kutokana na kufanya Biasha kwa ufanisi.