Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia
David Richard mwenye umri wa miaka 23 kwa kuiba gari aina ya raum rangi ya Grey
yenye namba za usajili T 702 DFV mali ya Gasper Abraham mwenye umri wa miaka 34
aliloiba katika eneo lake la kazi
Akizungumza na waandishi wa
habari mkoani Iringa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa
wamemkamata kijana huyo baada ya taarifa za kuibiwa kwa gari hilo kutolewa na
hivyo kupelekea jeshi la polisi kufanya doria ya kutosha na kuikuta wilaya ya
kilolo mkoani hapa
“Tunamshikilia David Richard
mwenye umri wa miaka 23 mlinzi wa RUCU aliiba gari hiyo ikiwa kwenye maegesho
lakini mmiliki alitoa taarifa kwenye jeshi la polisi na ndipo utaratibu wa
kumtafuta ukaanza ndipo ilipokutwa kwa mtuhumiwa akiitumia wilaya ya kilolo “
Pamoja na hayo Allan Bukumbi
alisema kuwa miongoni wa waharifu waliofanikiwa kuwakamata
katika msako walioufanya walifanikiwa kumkamata ndugu Boni Kipalile kwa
kosa la kukutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu moja
ikiwa chemba huku wakimshikilia benadetha kipago umri wa miaka 61 akiwa na meno
ya tembo na kiboko
“Ndugu waandishi wa habari
kutokana na taarifa za siri kijiji cha kiponzero wilaya ya mkoa wa Iringa tulifanikiwa
kumkamata boni kipalile mkulima mkazi wa igangidungu anayetuhumiwa kujihisuisha
na matukio mbalimbali ya kihalifu akizwa na silaha moja aina ya shortgun namba
za usajili 14949na risasi tatu moja ikiwa chemba pamoja na hilo tunamshikilia
benedetha kipago kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na meno mawili ya kiboko
“
Aidha kamanda wa Jeshi la
polisi mkoani Iringa amewataka wananchi kujitokeza na kutambua mali
zilizokamatwa kwa watuhumiwa Emmanuel Mnyeke (28) na Alfred Mkanula (25) ambao
walikamatwa na mali za wizi ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina ya sanlg ,boxer
na honda
Katika kushighulikia changamoto
mbalimbali jeshi la polisi mkoani iringa lilifanikiwa kumkamata Sebastian
Mahuwili (42) aliyehukumiwa kwa kesi ya kubaka mtoto wa miaka 6 na hivyo
kupelekea Kufungwa miaka 30 jela kutokana na ushahidi kukamilika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.