Friday, June 7, 2013
ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.
Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Sash Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013 |
Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo. |
Taarifa kwa Wadau wote:
ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.
Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.
Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.
Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.
Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14
MAMBO YA UKEREWE
HII NI VIDEO YENYE WIMBO WA ROBERT MUGABE, JK NYERERE, AUGUSTINE NETO, NA MARAIS WENGINE MAARUFU WAASISI WA BARA LA AFRICA.
NGOMA HUSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA HUKO VISIWANI UKEREWE. CD ZA LIVE SHOW ZINAPTIKANA KISIWANI UK
JAFET KASEBA NA MMALAWI KUZIPIGA
Jafet Kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony Ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na ibrahim kamwe 'bigright' |
KASEBA KUZIPIGA NA RASCO CHIMWANZA KESHO
Bondia Jafet Kaseba leo amepima tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa Malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony ruta,ibrahim kamwe,pendo njau na doctor John Lugambila wa muhuimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.
Kwa upande wake jafet kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama juma fundi atazipiga na Hasan Kiwale (moro best), josef onyango toka kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro,huku Issa Omar-Peche boy atakapo mvaa bondia mkongwe Juma Seleman.
Mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa ddc magomeni kondoa.
Nae mkongwe Juma Seleman kushoto akitunishiana misuli na bondia chipukizi kulia ISSA OMAR,hili ni moja ya pambano la kusisimua kutokana na uwezo wa wawili hao na kupaniana |
Baadhi ya mabondia wengine watakao pigana jumamosi DDC Magomeni |
Katika hali ambayo si ya kawaida kwa vyama vya ngumi hapa nchini kuwa pamoja kikazi katika mapambano wanayoyasimamia, kwa pambano la jumamosi itakuwa tofauti kwa baadhi ya maofisa wa chini wa vyama vya ngumi kusimamia mapambano kwa pamoja na kuua tofauti zao, na kujirudi kuwa wao ni wamoja katika michezo.
Airtel yaongeza muda vifurushi vya Airtel Yatosha, sasa huduma masaa 25 kwa siku
Dar es Salaam Juni 5 2013 Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA nchini ambapo sasa wateja watafurahia Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25 kwa siku, hii itawawezesha watanzania kufurahia kupiga simu mtandao wowote kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel yatosha masaa 25 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” kuanzia sasa, huduma ya Airtel yatosha kwa siku itakua kwa masaaa 25 kuanzia pale mteja anapojiunga na huduma, yaani masaa 24 ya kuongea na kama vile haitoshi Airtel yatosha inakuongezea saa jingine moja la ziada. Sasa wateja wa Airtel watafurahi kupiga simu kwa gharama nafuu na kwa muda zaidi kuliko ilivyokuwa awali”.
“Hii ni ya kwanza na pekee kutoka Airtel, Airtel yatosha itaendelea kuwa suluhisho la mawasiliano ya huduma za simu kwa watuamiaji na wateja wa Airtel nchi nzima ”. aliongeza Mmbando
Airtel yatosha ni huduma iliyoanzishwa ili kuleta kuvunja mipaka kwa watanzania na kuwawezesha kuwasiliana ndani na nje ya mtandaa kwa gharama nafuu. Kujiunga na huduma hii piga *149*99# na atapata majibu papo hapo achague unataka Yatosha WIKI au Yatosha SIKU au Tosha ya Mwenzi.
TAFAKURI YA LEO.....!!!
Mwalimu kaingia class akiwa na daftari la nukuu, akafunua na kuanza kuandika ubaoni:
Unga sh. 26,000/-
Maharage sh. 15,000/-
Pango sh. 150,000/-
Karo sh. 250,000/-
Mafuta sh. 20,000/-
Mangi dukani sh. 30,000/-
SACCOS sh. 55,000/-
Mshahara sh. 244,000/-
Alipokaa tu akastuka, "Agg.rrr.. Nimeandika madeni badala ya zoezi, Mungu wangu".. Akaanza kufuta, watoto wakapga kelele.. "MWALIMU HATUJAMALIZAAA.
Thursday, June 6, 2013
POLISI AVAMIA KAMBI YA ALBINO MISUNGWI, AMNG'OA MENO MLINZI
Matron wa kituo cha walemavu cha Mitindo Judith Mlolwa (mwenyekiti wa CCM wilaya ya Misungwi) |
KATIKA hali ya kushangaza, askari Polisi mmoja wa Kituo cha Misungwi, amevamia shule maalum ya walemavu wa ngozi (albino) na wenye mtindio ya ubongo akiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), kwa nia ya kumsaka mlezi wa wanafunzi hao, Judith Mlolwa na kuzua taftrani kubwa.
Askari huyo, ambaye alionekana kuwa na hasira kwa kile kinachodaiwa kumsaka Mlolwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi, alisababisha taharuki kubwa ya watoto kukimbia ovyo na kuumia vibaya.
Tukio hilo, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, saa 2 usiku shuleni hapo, ambapo askari huyo aliyefahamika kwa jina la Faraji mwenye namba G.3408 alipoamua kutumia nguvu kuingia shuleni hapo.
Katika purukushani hizo, askari huyo alimjeruhi mlinzi wa shule hiyo, Nyamizi Katemi kwa kutumia kitako cha bunduki.
Habari zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na afisa mmoja ndani ya jeshi la polisi, zimesema Faraji, alifanya tukio hilo akiwa kwenye lindo katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa habari hizo, Faraji alipofika shuleni hapo na kusema kuwa anamtafuta Mlolwa na alipojibiwa hayupo aligeuka mbogo na kuanza kutembeza kipigo.
Baada ya askari huyo kujibiwa hivyo, aliingia ndani ya uzio wa shule na kuanza kuwafukuza ovyo ovyo, pasipo na sababu za msingi.
Kutokana na Katemi kumsihi askari huyo, lakini hakumsikiliza ndipo alianza kumshambulia kwa kipigo na kumng’oa meno mawili.
Naye, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kulwa Ng’welo, alisema jana kuwa baada ya kuona vurugu hizo, alipiga simu polisi na askari wawili walifika shuleni hapo na kushindwa kumdhibiti askari mwenzao ambaye wakati huo tayari alikuwa akitamba na kudai kuwa lazima atimize dhamira yake.
“Baada ya taarifa walikuja bila silaha na kushindwa kumdhibiti hata kumsogelea Faraji.
Ofisa mmoja wa polisi, akielezea tukio hilo jana, alidai suala hilo limewaacha mdomo wazi askari wa Misungwi, lakini hakuwa tayari kulielezea zaidi kwa madai kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo.
“Leo (jana) nimefika kwa Kamanda wa Polisi Mkoa na kukutana naye ambapo nimemuelezea kila kitu na alinieleza kuwa alikuwa bado hajapata taarifa za tukio hilo, aliniahidi kuwa nirudi Misungwi na atalifuatilia kwa hatua zote,” alisema Matron Judith.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipotakiwa kuelezea tukio hilo, alisema hajapata taarifa na aliahidi kulifuatilia
.
Tukio hilo, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, saa 2 usiku shuleni hapo, ambapo askari huyo aliyefahamika kwa jina la Faraji mwenye namba G.3408 alipoamua kutumia nguvu kuingia shuleni hapo.
Katika purukushani hizo, askari huyo alimjeruhi mlinzi wa shule hiyo, Nyamizi Katemi kwa kutumia kitako cha bunduki.
Habari zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na afisa mmoja ndani ya jeshi la polisi, zimesema Faraji, alifanya tukio hilo akiwa kwenye lindo katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa habari hizo, Faraji alipofika shuleni hapo na kusema kuwa anamtafuta Mlolwa na alipojibiwa hayupo aligeuka mbogo na kuanza kutembeza kipigo.
Baada ya askari huyo kujibiwa hivyo, aliingia ndani ya uzio wa shule na kuanza kuwafukuza ovyo ovyo, pasipo na sababu za msingi.
Kutokana na Katemi kumsihi askari huyo, lakini hakumsikiliza ndipo alianza kumshambulia kwa kipigo na kumng’oa meno mawili.
Naye, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kulwa Ng’welo, alisema jana kuwa baada ya kuona vurugu hizo, alipiga simu polisi na askari wawili walifika shuleni hapo na kushindwa kumdhibiti askari mwenzao ambaye wakati huo tayari alikuwa akitamba na kudai kuwa lazima atimize dhamira yake.
“Baada ya taarifa walikuja bila silaha na kushindwa kumdhibiti hata kumsogelea Faraji.
Ofisa mmoja wa polisi, akielezea tukio hilo jana, alidai suala hilo limewaacha mdomo wazi askari wa Misungwi, lakini hakuwa tayari kulielezea zaidi kwa madai kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo.
“Leo (jana) nimefika kwa Kamanda wa Polisi Mkoa na kukutana naye ambapo nimemuelezea kila kitu na alinieleza kuwa alikuwa bado hajapata taarifa za tukio hilo, aliniahidi kuwa nirudi Misungwi na atalifuatilia kwa hatua zote,” alisema Matron Judith.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipotakiwa kuelezea tukio hilo, alisema hajapata taarifa na aliahidi kulifuatilia
.
VIJANA WENGI WAJITOKEZA USAJILI AIRTEL RISING STARS
Vijana wengi wajitokeza kwenye usaliji wa Airtel Rising Stars
USAJILI wa timu za mikoa inayoshiriki mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu umekuwa na mwitikio mkubwa miongoni mwa vijana wa umri huo katika mikoa ya Temeke, Ilala, Kinondoni na Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti makatibu wa mikoa hiyo ambao ndiyo wanaoratibu zoezi hilo la usajili wamesema kuwa vijana wengi wamejitokeza kiasi cha kulazimika kufanya mchujo ili kupata timu sita zinazotakiwa kushiriki Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa.
Katibu wa mkoa wa kisoka wa Temeke, Mbarouk Mohamed alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa kumekuwa na mwitikio wa ajabu ambapo zaidi ya timu mia zimejitokeza na kuwalazimu kuanza kufanya mchujo kwa kuzingatia vipaji ili kupata idadi ya timu sita zinazohitajika kushiriki.
“Kwa kweli ni vijana wengi mno wanaotaka kushiriki mashindano haya ya Airtel Rising Stars na tunaamini kuwa kujitokeza kwao kwa wingi kunatupa wigo mpana wa kupata wachezaji wazuri watakao tuwezesha kutetea ubingwa wetu katika fainali za ARS Taifa”
Naye Katibu wa Mkoa wa Ilala, Kanuti Daudi alisema kuwa mchakato usajili unaendelea vizuri na vijana wengi kujitokeza kwenda kujisajili. “Kutokana mwitikio huu tunatarajiza kumaliza usajili mapema kabla ya muda wa mwisho uliowekwa ambao ni Juni 11, 2013”, alisema Daudi.
Kwa upande wake Katibu wa Mkoa wa kisoka wa Kinondoni, Isack Mazwile alisema kuwa wameanza rasmi zoezi la usajili Jumapili iliyopita na kulingana na mwitikio wa vijana wengi wanatarajia kukamilisha zoezi hilo wiki hii. “Tutalazimika kufanya mchujo ili kupata vijana wenye vipaji vya soka wataounda timu sita za mkoa wetu”
Mkoa wa Tanga unaoshirikisha timu za wasichana pekee umeanza kuendesha ligi ambayo ndiyo inayotumika kubaini wachezaji wenye vipaji na hatimaye kuunda timu sita kwa ajili ya Airtel Rising Stars mkoani humo.
“Sisi huku tumeshaanza mchakato wa kutafuta timu kwa upande wa wasichana , na kwakweli nimefurahi kuona mwitikio wa timu umekuwa mkubwa na hapa tunajiandaa kuzichuja ili tuweze kupata timu bora, “ alisema katibu wa soka mkoa wa Tanga Beatrice Shabani.
Mbali na mkoa wa Tanga mikoa mingine inayoshirikisha wasichana pekee ni Kigoma na Ruvuma wakati mikoa ya kisoka ya Kinondoni, Ilala na Temeke inashirikisha wavulana na wasichana huku Morogoro, Mwanza na Mbeya ikijumuisha wavulana pekee.
Mikoa ya Morogoro, Mwanza, Kigoma, Ruvuma na Mbeya pia imeshaanza usajili na inatarajia kukamilisha zoezi hilo kabla ya siku ya mwisho Juni 11.
MALKIA WA TAARAB HADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE
Jafari Ally enzi za uhai wake akiwa na mkewe Malkia wa Mipasho nchini Tanzania, Khadija Omar Kopa wakifuatilia onesho la Mshauzi Classic ndani ya Mango Garden. |
Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina la Jafari Ally, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua.
Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini.
Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa maeneo ya Chalinze au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
CHANZO: FATHER KIDEVU
Wednesday, June 5, 2013
MWANZA YANYAKUA TENA TUZO YA USAFI KWA MARA YA 8 MFULULIZO.
Wednesday, June 05, 2013
No comments
Wafanyabiashara kwenye eneo karibu na soko kuu. |
Wameitikia na suala la kuzibua mifereji... Ole wenu hamasa hii iwe zimamoto tutarudi.. |
Baadhi ya mitaa yenye miundo mbinu iliyokamilika na muonekano wake. |
Ushindi haujaja hivi hivi kunasababu za ziada. |
"KWA HERI ALBERT MANGWEA"
Msanii Wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond akipita kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea. |
Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Wa Kwanza Kabisa ni Mkoloni akifuatiwa na Madee ambaye ni wa Tatu kutoka Mbele wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Albert Mangwea |
Msanii wa Muziki Keisha (aliyejifunga kiremba Cheupe) akifuatiwa na Noora wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakipita kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho leo katika viwanja vya leaders |
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho |
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Albert Mangwea likiwa juu ya meza tayari kwa Wakazi wa Jiji la Dar Kuanza kutoa Heshima Zao za Mwisho katika Viwanja Vya Leaders leo. |
Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, utamaduni na Michezo Bi Lilian Bereko akitoa Salamu za Rambirambi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo katika viwanja vya leaders kabla ya Wakazi wa Jiji la Dar hawajaanza kutoa heshima zao za mwisho |
Mmoja kati ya watu wa karibu wa Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni msanii wa muziki wa Kizazi kipya kutoka Katika Kundi aliloanzisha Marehemu Albert Mangwea Mez B akitoa historia fupi ya Kundi la Chamber Squade katika viwanja vya leaders leo |
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake wakiwa wamekaa tayari kwa kusubiria shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders |
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa na Nyuso Za Huzuni wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja vya Leaders |
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho pamoja na kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja Vya Leaders |
Askari Polisi wakijaribu kuweka mambo sawa ili kusudi wakazi wa Jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake kuweza kuingia kwaajili ya kutoa heshima zao kwa utaratibu mzuri na kuepusha vurugu |
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiwa wanatoka kutoa heshima zao za Mwisho |
PICHA ZOTE NA LUKAZA BLOG
MWANZA ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI HII LEO
Ujumbe wa mwaka huu juu ya siku ya mazingira. |
Shughuli mbalimbali za utoaji elimu kwa wilaya za Nyamagana na Ilemela zimefanyika leo katika viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza. |
Hili ni banda la Wizara ya maji mradi wa hifadhi ya mazingira ya ziwa Victoria (LVEMP) ambapo kulikuwa na huduma za utolewaji ufafanuzi sambamba na elimu ya utunzaji mazingira. |
Muonekano zaidi. |
Glory Munhambo wa banda la Bodi ya Utalii Tz mkoa wa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliodhuru banda lake. |
Bidhaa zizalishwazo na Donna African Fashion. |
Ni bidhaa ambazo miaka ya sasa zatajwa kuvaliwa na wengi kama sehemu ya kuitikia wito wa kuthamini bidhaa za nyumbani. |
Vinogesho asili ndani ya Donna African Fashion. |
Tuhamie hapa sasa..... |
Mdau na wateja wake. |
Dagaa na bidhaa za nafaka... |
BHARTI AIRTEL YASAIDIA KUONDOA UMASKINI KUPITIA MRADI WA MILLENIUM VILLAGE
Bharti Airtel yasaidia kuondoa umaskini kupitia mradi wa Millenium
Village
* Mradi huo kutoa elimu kwa wafanyakazi wa afya kwa kupitia huduma za mawasiliano
* Yawawezesha wafanyakazi 240 kuwasiliana kwa gharama nafuu za pekee.
* Airtel unasaidiana na mradi huu wa millennium village katika nchi 6 za Afrika
Dar es Salaam Juni 04 2013: Kampuni ya Bharti ("Airtel") inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika ndani ya nchi 20 barani Afrika na Asia, leo imethihirisha thamira yake ya kufikia malengo ya Millenium kwa kushirikiana na kampuni ya Erickson katika mradi maalum ujulikanao kama Millenum village inayoendeshwa katika nchi 6 za Afrika ikiweko Tanzania.
Mradi huo umeundwa na taasisi ya Earth Institute kwa dhamira ya kutimiza baadhi ya malengo ya Milenia kwa kuelekeza ufumbuzi wa kiubunifu zaidi katika maeneo ya vijijini huku ikishirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni ya simu za mkononi Airtel barani Afrika Airtel imesaidia mradi wa millennium village katika mkoa wa Tabora kwa kutoa huduma za mawasiliano zitakazowawezesha watu kupata elimu kuhusu maswala ya afya kwa urahisi. Airtel imetoa namba ya dharura itakayopigwa bila kutozwa gharama yoyote na kuwawezesha watoa huduma za afya na wagonjwa kuwasiliana kiurahisi zaidi.
Mradi wa millennium Vilage unasaidiwa na Airtel katika nchi 6 ambazo Airtel inafanya biashara zake. Nchini Tanzania mradi wa millinium village umeanzishwa katika eneo la Mbola mkoani Tabora na kusambaa katika maeneo mengi na kufikia zaidi ya vijiji 20 vilivyopo katika eneo lenye mita za mraba 700msq likiwa na wakazi 30,0000 waishio katika wilaya ya Uyui Tabora.
Mpaka sasa mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa, zaidi ya watu 500,000 katika nchi 11 zilizoko kusini mwa jagwa la sahara Afrika wamefaidika ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2011 asiliimia 90 ya vijiji vilikuwa vimesha unganishwa na mtandao wa simu Vile vile ndani ya mradi huu kuna kipengele cha Connect to Learn, chenye ushirikiano baina ya Earth Institute Chuo kikuu cha Columbia , Ericsson and Bharti Airtel Africa, ulioanzishwa katika shule zilizopo ndani ya mradi wa millennium village na kuwafikia walimu na wanafunzi zaidi ya 5,000 katika nchi za Ghana, Tanzania, Uganda na Kenya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema" Airtel ina dhamira ya kugusa maisha ya watu si tu kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu lakini pia kuwazifikia jamii za chini zenye uhitaji wa technologia katika kuendeleza na kukuza maisha yao, ambayo ndio lengo lililotufanya kushirikiana na Earth Institute pamoja na Erickson kusaidia mradi huu wa millennium village.
Ushirikiano huu unatupelekea kufikia malengo ya mradi wa millennium village ya kushughulikia changamoto za umasikini katika maeneo mengi ikiwemo Kilimo, elimu, afya, miundo mbinu, usawa katika jinsia na kukua kwa Biashara. Tunafurahi kuwa sehemu ya mabadiliko na tunaahidi kuisaidia jamii nchini Tanzania.
Akiongea wakati wa halfa ya kupanua mradi wa millennium village katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora, Meneja Huduma Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi alisema" tunafurahi kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu katika vijiji mbalimbali Tanzania .
leo tunaonyesha kwa
vitendo dhamira yetu na kuwapatia wafanyakazi 240 huduma za mawasiliano
ili kuuendesha mradi huu wa millennium village kirahisi. Airtel pia
imetoa namba ya dharura ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo
huduma za dharura na elimu ya afya katika kijiji cha Mbola"
"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii" aliongeza Bayumi
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii kupita mitandao na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule."
"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii" aliongeza Bayumi
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii kupita mitandao na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule."
Mbali na mradi wa Millennium Villages , Airtel Tanzania iko mstari wa mbele katika kusaidia shule za secondari nchini kwa kuwapati nyenzo za kufundishia ikiwemo vitabu. Tangu kuanzishwa kwa mradi wa 'Airtel Shule Yetu' zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na kupata vitabu kutoka Airtel.
Subscribe to:
Posts (Atom)