ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 5, 2013

MWANZA YANYAKUA TENA TUZO YA USAFI KWA MARA YA 8 MFULULIZO.

Kwa mara ya nane mfululizo jiji la Mwanza limeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa jiji linaloongoza kwa Usafi Tanzania, kwa mujibu wa Mstahiki Meya Stanslaus Mabula hivi sasa aliyeko wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambako ndiko siku ya mazingira kitaifa inafanyika amesema kuwa Jiji lake liko kwenye mpango wa kushindana kimataifa kwa usafi..


Licha ya changamoto ya kuwa na barabara zinazohitaji ujenzi kiwango cha lami kwa mitaa mingi, Mkoa wa Mwanza umjikita katika kuanzisha utaratibu wa kufanya usafi wa kaya kwa kaya, ofisi kwa ofisi, mlango kwa mlango ambapo kila mwananchi anapaswa kushiriki suala la usafi.

Wafanyabiashara kwenye eneo karibu na soko kuu.

Wameitikia na suala la kuzibua mifereji... Ole wenu hamasa hii iwe zimamoto tutarudi..

Baadhi ya mitaa yenye miundo mbinu iliyokamilika na muonekano wake.

Ushindi haujaja hivi hivi kunasababu za ziada.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.