ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 18, 2014

HAWA JAMAA WAMEAHIDI KUMFUNIKA 'TI' LEO LEADERS JIJINI DAR KATIKA SERENGETI FIESTA 2014

Wakati Jiji la Dar es salaam likiongezeka joto kwa Tamasha la Serengeti Fiesta  2014 kumshusha mwanamuziki mkali wa Hip Hop kutoka nchini Marekani mwenye tuzo nyingi za Grammy, mtu mzima TI, tayari kuna wadau wa kuchana kitaani wameanza kutamba kuwa beat aliyoitumia msanii huyo katika wimbo wa No Midiocle, eti,,,,naongeza eti,,,,, hakuitendea haki, hivyo na wao wakaamua kutinga studio na kuifanyizia 'babakE'.

Jeh wamempiku, wamefanikiwa kumpindua, wamemfunika au wametokota?? 

SIKILIZA KWA KUBOFYA PLAY.


 Meneja wa Msanii wa Kimataifa T.I,  Jonson Geter wa kwanza kushoto akifafanua jambo kupitia moja ya maswali yaliyoulizwa na mmoja  wasanii walioshiriki kwenye semina ya fursa ndogo ya Wasanii na wadau wa muziki iliyofanyika kwenye ukumbi wa Litle Theather,jijini Dar, Pichani kulia ni Prodyuza  mahiri wa Muziki wa hapa nchini anayemiliki studio yake Bongo Records, P-Funk Majani.

TIGO SASA NI MKONO KWA MKONO NA BODABODA MWANZA

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya ziwa Ally Maswanya akizungumza na waendesha bodaboda mkoani Mwanza, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madereva wa Bodaboda na mpango wa Tigo kuwawezesha kukuza mtaji kwa kuwapa lita moja ya mafuta bure pindi wanaweka lita tatu au zaidi kwa kulipia kupitia Tigo Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza (RTO) Nuru Selemani.
Sehemu ya madereva wa bodaboda waliojitokeza katika viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza, kuingia kwenye mpango wa kuwezeshwa na Tigo kwa kupata ofa ya lita moja zaidi (bure) pindi wanaweka lita tatu au zaidi kwa kulipia kupitia Tigo Pesa. Jumla ya Madereva 300 wameandikishwa mkoani Mwanza katika mpango huo. 
Meneja wa Tigo kanda ya ziwa John Tungaraza (katikati) akitoa maelezo wakati wa kuwaandikisha madereva wa bodaboda mkoani Mwanza, ili waingie kwenye mpango wa kuwezeshwa na Tigo kwa kupata ofa ya lita moja zaidi (bure) pindi wanaweka lita tatu au zaidi kwa kulipia kupitia Tigo Pesa. Jumla ya Madereva 300 wameandikishwa mkoani Mwanza katika mpango huo.
Msafara wa madereva wa Bodaboda ukiranda katika barabara za jiji la Mwanza kuelekea moja kati ya vituo saba vya mafuta vilivyoainishwa kwaajili ya kuingia kwenye mpango wa kuwezeshwa na Tigo kwa kupata ofa ya lita moja zaidi (bure) pindi wanaweka lita tatu au zaidi kwa kulipia kupitia Tigo Pesa.
Zoezi hili la Tigo limekuja ikiwa ni mara baada ya shughuli za usafiri wa Bodaboda kurasimishwa nchini na kutambulika kama sehemu ya ajira rasmi kati ya vyombo vya usafiri rahisi.
Msafara ulipendeza 'kinyama'
Kuelekea moja kati ya vituo vya mafuta kwaajili ya kupata huduma ya ofa ya lita moja kwa kila dereva.
Kituo cha mafuta cha MOIL kilichopo Sabasaba ilemela jijini Mwanza ni moja kati ya vituo saba vilivyoainishwa kwaajili ya mpango wa Tigo kwa kupata ofa ya lita moja zaidi (bure) pindi madereva Bodaboda wakiweka lita tatu au zaidi kwa kulipia kupitia Tigo Pesa.
Mapozi ya washereheshaji.
Mashine za Tigo.
Mpaka kuleEEEeee!!
Kisha msafara ulielekea katikati ya jiji la Mwanza.
Tukio hili licha ya kuwa sehemu ya uchumi na biashara pia lilionekana kama utalii kwa wapita njia.
Aidha John Tungaraza ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa amesema kupitia mpango huu Kampuni yake ikishirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani, imeahidi kuandaa siku maalum kwa madereva hao wa Bodaboda mkoa wa Mwanza ambapo watapatiwa semina maalum itakayolenga kuboresha uendeshaji wao kuwa salama barabarani, kuwaepusha na ajali zinazozuilika, sambamba na kutoa leseni bure (zitakazo kuwa zimelipiwa na Tigo) kwa madereva watakao fuzu vyema mafunzo yatakayotolewa.

STAND UNITED TAYARI IPO BUKOBA KUUMANA NA KAGERA KAITABA LEO

PICHA na Faustine Ruta: Bukoba
JUMLA ya wachezaji wa Timu ya Stand United wametua Mjini Bukoba siku ya tatu leo kwa ajili ya Kipute cha Ligi kuu Vodacom msimu wa 2014-15 na Wenyeji wao Kagera Sugar jana asubuhi walifanya yao kwa mara ya kwanza wakiwa mkoani Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba. 

Wachezaji hao 26 wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na Viongozi wengine 6 wanaounda kikosi cha timu mpya iliyoionja ligi kuu ya Tanzania bara kwa mara ya kwanza baada ya kuwa miongoni mwa timu tatu zilizopanda ligi kwa msimu wa 2013-2014, wameahidi kuonyesha soka safi kwa mashabiki huku wakiahidi kuendelea kuonyesha maajabu kwa kung'oka na ushindi katika madimba ya ugenini.

Timu ya Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wa mchezo huo wanashika nafasi ya nane nyuma ya Stand United walio nafasi ya saba wakizidiwa magoli ya kufunga wao wameamua kujichimbia nje kabisa ya mji wa Bukoba.
BOFYA PLAY SIKILIZA TAARIFA ILIYORUKA LIVE JANA SPORTS XTRA CLOUDS FM.


Stand United.
Wachezaji wa Stand United wakifanya mazoezi 
Kocha Mkuu wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe (kushoto) akiwacheki Vijana wake Wakijifua kwenye Uwanja wa Kaitaba 

HIVI NDIVYO SKYLIGHT BAND HUFANYA

DSC_0088
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Digna Mbepera wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai Village.
DSC_0102
Skylight Band wakiserebuka na burudani yao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
DSC_0113
Unajua siri ni nani anayemfanya Aneth Kushaba AK 47 kung'ara katika mambo ya Make Up?? si mwingine mfollow Instagram @timelesstz ukapendeze kama AK47.
DSC_0319
Pale Mashabiki wanapokunwa na burudani ya Skylight Band.
DSC_0118
Vocal zikiendelea kuporomoshwa kwa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0027
NABOLINGOOOOO....! Binti mwenye kipaji cha pekee na sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera akitoa burudani kwa mashabiki wanaojumuika na Skylight Band kula bata kila siku za Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0178
Sam Mapenzi akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata kitu roho inapenda.
DSC_0214
Mmoja wa mashabiki wakubwa wa Skylight Band akishow love mbele ya camera yetu huku wengine wakijinafasi kwa raha zao pale kati.
DSC_0270
Raha zote hizi zinapatikana kila Ijumaa ndani ya Thai Village USIKOSE: Joniko Flower akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band walifurika kuianza week end yao na bendi ya kijanja ambayo ni habari ya mujini kwa sasa.
DSC_0265
Mashabiki wa Skylight Band wakijinafasi na mduara shurti wa nyuma aende mbele na wa mbele aende nyuma na mwenye kiuno kiti chamsubiri pale kati....!
DSC_0285
Wakinadada wakizungusha hizo nyonga zao. #MaunoYaKumwagaRadhi.
DSC_0289
TOPHY Bass akilicharaza gitaa huku Daudi Tumba akizichapa Tumba zake kwa ustadi kabisa.
DSC_0352
Calvin Michael a.k.a DJ-K'FLIP wa Jembe Beach Resort na Club Jembe anahusika kwenye moja na mbili kuendelea kuwapa bata mashabiki wa Skylight Band baada kumalizika kwa muziki wa Live ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0361
Kutoka kushoto ni Rais wa Wanamanyoya Family a.k.a #Sultan Gijegije, Eddievied na Luhano Lupogo wakiwakilisha #Wanamanyoya na ukodak.
DSC_0299
Mdau Andrew akishow love na warembooozzzz walipokuja kula bata na Skylight Band.
DSC_0298
Birthday Boy Professor Kingu (kushoto) akipata ukodak na mdau wa Skylight Band David.
DSC_0346
Birthday boy mwingine mratibu wa Skylight Band Lubea (kulia) akipata ukodak na Babu wa Kitaa na mdau.
DSC_0136
Man kushaba (kushoto) akishow love na marafiki.
DSC_0150
Mdau Faraja Fares (kushoto) akipata ukodak na marafiki.
DSC_0186
Divas wa Skylight Band wakipata ukodak.
DSC_0120
Wanamanyoya Family wakiwa na Rais wao Sultan Gijegije wa Oman.
DSC_0357
Sam Mapenzi wa Skylight Band akishow love na mashabiki wake.
DSC_0175
Blogger King Kif akishow love na wadau wa Skylight Band Ijumaa iliyopita.
DSC_0330
Hashim Donode na wadau wakubwa wa Skylight Band.

KUMENOGA...!!!


Thursday, October 16, 2014

MPINA KUENZI UTAMADUNI WA WASUKUMA.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.

Mpina alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.

Hata hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.

Akizungumza mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.

Naye Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.

Pambano hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

Mpina aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI


Wachezaji wa ngoma toka kundi la Malogi Hamsini ambaye ni Mgika wakifanya yao.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa mpambano wa ngoma asili kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagika, Malogi Hamsini (kulia) akiwa amesimama barabara kuuanza mpambano ambapo alizidiwa nguvu ya uchawi na Mpinzani wake Magise Jilunga ambaye Mgalu.
Wachezaji wa kundi la Malogi Hamsini wakionyesha kazi.
Mara baada ya kuona ameshindwa katika nguvu za kichawi Malogi Hamsini alipandwa na hasira ampazo alizielekeza kweye tunguli zake.
Na hapo ndipo alipo amua kuziteketeza kwa kuzifumua kwa mateke..... PwachAaA!!
Wingi wa watu ndiyo pointi za ushindi watu walihama toka kwa Malogi Hamsini na kuelekea kwa Magise Jilunga ambapo kila mmoja alikuwa akipiga ngoma kwa wakati mmoja (yaani kulia na kushoto wapi pananoga?).
Wananchi wakiwa wameizunguka himaya ya Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga wa pili kutoka kushoto akiwa tayari kulianzisha kwenye mpambano kati yake na Malogi Hamsini ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina.
Hatari kama anaporomoka vile...
Malogi Hamsini alituma nyoka kuja kuharibu ngoma ya Magise Jilunga lakini hakufua dafu.
Mapanga dizaini....
Akinamama wakiingia kwenye lango kuu kushuhudia mpambano.
Michezo ya hatari balaa ni mwendo kugalagala kwenye moto.
Silaha ya ushindi kwa Magise Jilunga ilikuwa ni kubadilika badilika.
Si kubadilika tu bali alikuwa na vionjo kama kuoga moto mchana kweupe na kunywa mafuta ya dizeli...tobA!
Ni balaa mwanawane!!!
Jamaa aliamua kukizika kichwa kwa dakika kadhaa kiasi cha kusisimua mashabiki!!
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga akipiga ngoma kuusaka ushindi.
Viongozi wa kada mbalimbali nao wamo.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Maelfu waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na Mhe. Mbunge, ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Ni wakati wa jaji Mkuu kutangaza matokeo rasmi:- Mpambano wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
 Malogi Hamsini (kushoto) akimpongeza kiroho safi Magise Jilunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi....
Full m-banano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaaga wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumalizika mpambano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaamezungukwa na maelfu ya wananchi waliofika eneo la uwanja wa kusanyiko.