|
Mkurungezi wa spanco Tanzania bw Chandrashekhar Narayanan akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo Airtel imesherehekea na wateja wake kwa kuwashukuru kwa kutumia huduma Zake, Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel bi Adrianna Lyamba na kulia ni Meneja uendeshaji Amit Arora. |
|
Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor akiongea na waandishi wa habari wakati wa maathimisho ya wiki ya ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo Airtel imesherehekea na wateja wake kwa kuwashukuru kwa kutumia huduma Zake
|
Airtel yaadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja, yaahidi kuendelea kutoa huduma za kisasa
· Kauli mbiu “Ni mimi wa kukupa huduma bora “ Airtel inadhihirisha mteja ni muhimu
· Airtel yawaahidi wateja huduma bora na za kisasa nchini
Dar es salaam, 4 Oktoba 2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja duniani kwa kutoa na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake hapa nchini.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Bw. Sam Elangalloor leo Jijini dar ikiwa ni katikati ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bw Sam Elangalloor alisema “Airtel imejipanga kutoa huduma bora na za kimataifa kwa kuwa tumewekeza kikamilifu katika vitendea kazi vya kisasa na pia tunashirikiana kikamilifu na wadau wetu wataalam wa huduma kwa wateja SPANCO RAPS –Tanzania Limited ili kumpatia mteja huduma yenye ubora zaidi kila wakati, tunawatoa huduma zaidi ya 650 wakitoa huduma masaa 24 siku 7 za wiki. Airtel tutaendelea na dhamira yetu hii ya kutoa huduma bora na ya kisasa ili kuendelea kuvutia wateja wengi kutumia mtandao wa Airtel pamoja na kutimiza malengo yao mbalimbali.”
Sam aliendelea kwa kusema” tumewekeza kwa kiasi kikubwa kupanua wigo wa mawasiliano hasa vijijini na hivyo tumekuwa na ongezeko kubwa la wateja wanaojiunga kwenye huduma zetu. Leo asilimia 97 za simu zinazopigwa kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja ni zakutaka ufafanuzi wa namna ya kutumia huduma zetu za Internet, meseji, namna ya kutumia simu, Airtel money na nyingine zinazofanana na hizo
Vileviele Airtel tumewekeza kikamilifu katika mfumo wetu wa ndani na nje wa mawasiliano kwa kuweka miundombinu ya kisasa kwa lengo la kuwahudumia wateja kwa haraka na urahisi zaidi. Airtel tunaushirikiano mkubwa na IBM wataalam wakubwa katika teknolojia ya mwasiliano duniani ikiwa ni muendelezo wa kutimiza dhamira yetu kuhakikisha tunatoa mawasiliano bora na nafuu kwa kumfaidisha mteja wetu wakati wote atumiapo huduma za Airtel” aliongeza bw Elangalloor
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba alisema” tunao wafanyakazi waliopata mafunzo na wanaoendelea kupewa mafunzo mbalimbali ili kwenda na mabadiliko mbalimbali ya technologia za kisasa. Hivi karibuni tulizindua Mafunzo ya muda mrefu yajulikanayo kama Airtel Service Academy ili kuwawezesha wafanyakazi wetu kuongeza ufanisi kwa kupitia mafunzo haya”.
Sambamba na hilo tumewekeza kwenye technolojia za kisasa ili kuwawezesha wateja wetu kutufikia kirahisi kupitia call center zetu. Leo tunayofuraha kuweza kuwasiliana na wateja wetu nchi nzima kupitia mawakala au kwa kupiga namba 0784001001 bila malipo na kuweza kupata taarifa mbalimbali zikiwemo ofa kabambe, huduma za internet, kupiga na kutuma ujumbe mfupi na nyingine nyingi”
Airtel call center inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki, na tunapokea simu zaidi ya laki moja kwa siku hii ni kutokana na wateja wetu wengi kutumia huduma za simu na internet mara ya kwanza,
Maduka yetu yanafunguliwa kuanzia saa 2 hadi saa moja usiku, ili kuweza mteja wetu ili kuwasiliana nasi tafadhali piga namba 100 bure au piga +255 78 4105 400, +255 78 4104 800 ikiwa unatumia namba ya mtando mwengine na utatozwa gharama ya kupiga simu ya kawaida, vilevile unaweza kutupata kwa kupitia barua pepe Email info@tz.airtel.com.” aliongeza Lyamba
Nae Mkurugenzi wa Spanco Tanzania Chandrashekhar Narayanan alisema” tunayofuraha kushirikiana na Airtel katika kutoa huduma bora kwa wateja Tanzania. Tunaamini huduma bora tunayoitoa inafanikisha lengo la Airtel la kuwa mtandao unaopendwa na watanzania nchini. Tunauzoefu wa kutoa huduma kwa wateja katika nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na kupokea simu za wateja zaidi ya 400000 kwa siku”
Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa tarehe mosi hadi tano ya mwezi October Duniani kote na hapa nchini kampuni ya Airtel yenye wateja zaidi ya milioni 8 inafanya maadhimisho hayo kwa shughuli mbalimbali huku kauli mbiu yao ikiwa ni “ Ni mimi wa kukupa huduma bora “ Airtel inadhihirisha mteja ni muhimu
Airtel ni mtandao wenye gharama nafuu na wenye mtandao mpana ulioenea zaidi kwa utoa huduma kama vile Airtel money ambayo imewezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kirahisa kwa gharama mahali popote nchini.