ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 6, 2012

MWANZA NA AJIRA.

     Hivi majuzi katika ziara ya Mh. Waziri mkuu Mizengo K. Pinda alitoa wito kwa wakazi wa jimbo la Nyamagana kuhakikisha kuwa wanafanya uvuvi endelevu ili kunusuru zao la samaki na wimbi la uvuvi haramu linalotishia biashara hiyo kuanguka lengo la kauli hiyo ni kuboresha sekta hiyo iendelee kuchangia pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mji wa Mwanza umejengwa na uvuvi. Eneo la jimbo la Nyamagana lina kilomitaza mraba ya nchi kavu 185 na wakazi wanaokadiriwa kuwa 300,000 na 3% ni wazawa na 8% ni wageni kutoka mikoa jirani.

     Kwakuzingatia binadamu hana urafiki na Nyoka basi kabila la Wasukuma limezidi kumudu maisha na kuchangia uchumi wa familia na taifa kadhalika kujipatia sifa maradufu kitaifa na kimataifa baada ya kucheza ngoma zao na Nyoka na kuwa kivutio kwa watu. Ieleweke bayana kuwa 80% ya Nyoka wote hawana sumu. 

Swali la kujiuliza Unautumiaje utamaduni wako katika kuchangia pato lako binafsi na pato la Taifa ikiwa ni mkakati wa kupunguza umaskini na kuongeza kipato cha mtu kwa kuongeza ajira kwa vijana ambapo 60% ya vijana hawana ajira?

     Kazi ni kazi ‘bhana’… Asilimia 60% ya vijana nchini hawana ajira.

     Tinga Tinga ni mapambo yaliyobuniwa kutoka mkoa wa Iringa nchini Tanzania na kuhimili soko la kitaifa na kimataifa. Chakustaajabisha biashara hii nje ya mipaka ya Tanzania inasadikika kujulikana kama ni mapambo asili ya Kenya hivyo Kenya imekuwa ikipata fedha zakigeni maradufu na watanzania wakiambulia patupu. Mjane Magreth Jaffy Mollel mmiliki wa Tinga Tinga arts Gallery ambaye marehemu mumewake

Swala la ajira nchini Tanzania limekuwa mtambuka na kuwezesha sector binafsi kufikia 35% isiyo rasmi ambapo sheria za nchi imeziainisha na kuweka utaratibu unaomuwezesha mtu kufanya biashara kulingana na mtaji wake. Miongoni mwa ajira hiyo Boda boda kuchangia vijana kujiajiri japo kama Boda Boda wa jiji la Mwanza hawana Bima ya ajari.

 Hofu kubwa ni uendeshaji usiozingatia sheria na taratibu ikiwa na leseni na umakini kazini. Taasis watu binafsi mnashiriki vipi kuwezesha ajira35% isiyo lasmi iweze kuwa rasmi na kupunguza 60% ya vijana ambao hawana ajira? Japo kama umakini ktk uendeshaji wa boda boda unahitajika ili kuepusha ajari

Wahenga waronga:- mtaji wa masikini ni nguvu zake. Na dunia ya leo inasema ili uwe mfanya biashara uliyefanikiwa na unayetaka kufanikiwa kwa haraka na kwa wepesi basi 
1. nilazima ufanye biashara ya mtandao tofauti na kuchukua mzigo na kukaa na kusubiri mteja akufuate hapo ulipo.

2 Ujue mshindani wako katika biashara. 

3. Uatambue mteja wako. 

4. Uwe mbunifu na kutambua fursailiyopo inayoweza kupelekea ukawa tofauti na wafanya biashara wanaokuzunguka. Wewe unaonaje katika bisahara yako?    

Camera inaweza kutumiwa kama chombo cha kuchukua kumbukumbu lakini kwa Alex Nyoni Enhard kijana mwenye umri wa miaka 25 mwenyeji kutoka mkoa wa Mbeya ni ajira inayomuwezesha kumudu maisha yake kila siku na kumsaidia kupata 8000 kwa siku mpaka 150000 mara 3 kwa mwezi. Kwakua yeye ni mtoto wa kwanza ktk familia yake basi biashara hii isiyokuwa na bima au mkopo ameweza kuimudu kwa miaka mitatu na kumwezesha kuwa na familia ya watu watatu na kusomesha wadogo zake wawilili.

 Japo kama ana account bank kipato chote anachokipata kinaishia kinywani na kwenye mzunguko wa mahitaji ya familia. Mafanikio makuu ambayo ameyapata katika biashara hii ni pamoja na kuimarisha mahusiano na watu na kufanhamika.
   

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.