ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 16, 2019

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS WA AFRIKA KUSINI RAMAPHOSA WASHIRIKI MKUTANO WA WAFANYABIASHA WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (wa tatu kutoka kushoto) akipiga makofi. 
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kuhutubia kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam.
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.

MBUNGE MGIMWA AKERWA NA UBOVU WA BARABARA ZA KATA YA MAPANDA

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa  kijiji cha Chogo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihimbo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na wananchi kutofanya kazi kwa uhuru.

Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kata ya Mapanda Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amekiwa kuwa tatizo la ubovu wa miundombinu hiyo imekuwa kero na ameanza kuifanyia kazi ili kuzikarabati ziweze kupitika kirahisi.

“Nimebaini kuwepo kwa uchakavu wa barabara katika kata ya Mapanda ambazo zimekuwa zikififisha maendeleo ya jimbo langu hivyo natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha barabara hizi zinapitika” alisema Mgimwa

Mgimwa amesema kuwa amefaikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutengeza barabara zote korofi ili ziweze kupitika kwa urahisi.

“Nimefakisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia nane kuhakikisha tunakarabati barabara hii ambayo imekuwa inatumiwa na watu wengi kimaendeleo katika jimbo hili” alisema Mgimwa

Mgimwaalisema kuwa kuna barabara inayotoka kuanzia Kibengu,Kipanga,Ihimbo,Uhafiwa,Kisusa,Ukami hadi njia panda ya Mapanda inayokadiliwa kuwa na urefu wa kilometa sitini na moja imetengewa fedha kidogo tofauti na matengenezo yanayotakiwa kufanyika katika barabara hiyo.

“Nitakuja na viongozi wa TARURA huku kuhakikisha wanajionea ubo vu wa barabara hizi ili wanavyotenga fedha wajue wanakarabati wapi na wanaacha wapi haiwezekani barabara hii ikatengewa kiasi cha shilingi milioni thelethini tu” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa amewataka TANROAD na TARURA kuzikarabati  barabara zote korofi kipindi cha kiangazi  ili zipitike kirahisi na sio kipindi cha masika ambapo mara nyingi hutokea kero kwa wananchi.

Wakitoa kilio chao kwa mbunge huyo wanachi wa vijiji hivyo walimwambia hakuna maendeleo yanayoendelea katika vijiji hivyo kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Hakuna usafiri wa basi wala gari inayofika huku kutokana na ubovu wa barabara hizi hivyo tunakuomba uhakikishe unatusaidia kuzikarabati barabara hizo” walisema wananchi 

Thursday, August 15, 2019

WATUMIAJI WA MTANDAO WA INTERNET CHINA YAFIKIA MILIONI 830

Ripoti iliyotolewa na idara ya takwimu ya taifa ya China imesema, idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China imeongezeka kutoka laki 6.2 ya mwaka 1997 hadi milioni 830 ya mwaka 2018. Mwaka 2018 matumizi ya mtandao wa simu za mkononi yalifikia GB bilioni 71.1, ambayo ni mara 56.1 ya mwaka 2013.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA imetimiza maendeleo makubwa.

Hadi mwishoni mwa mwaka jana, idadi ya watumiaji wa mtandao wa mkonga wa mawasiliano imefikia milioni 368 na idadi ya watumiaji wa mtandao wa 4G imefikia bilioni 1.17. Idadi ya watumiaji wa simu kote nchini China imefikia bilioni 1.75 ambayo inashika nafasi ya kwanza duniani.

RAIS MAGUFULI ATAJA 'DAWA YA UMASIKINI AFRIKA'


Rais Magufuli, amesema hakuna uchaguzi mwingine katika kuhakikisha Afrika inaondokana na unyonge zaidi ya kuungana katika mapambano ya kiuchumi.

Amesema hayo akiwa na mgeni wake Rais  Cyril Ramaphosa wakati wa jukwa la baishara kati ya wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Kusini na Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo ambapo  amesisitiza  kuwa hakuna kinacheweza kuzuia  Afrika kuwa na maendeleo.

Rais Magufuli alisema, zaidia ya asilimia 70 ya uzalishaji katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) bidhaa zinakwenda Afrika Kusini. Alisisitiza, bidhaa nyingi zinakwenda Afrika Kusini ikiwemo mbogamboga na matunda, nafaka, vinywaji, mpira na huduma za usafiri.

Rais Magufuli amebainisha kuwa , Afrika Kusini ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini ambapo kwa mwaka jana 2018 mauzo katika biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 5.3,” alisema.

“Afrika Kusini ni ya 13 kwa uwekezaji nchini, takwimu zinaonyesha uhusiano wetu katika uchumi ni mkubwa, maendeleo haya yanaonyesha urafiki wetu wa kibiashara, kiuchumi, kijamii na kisiasa unaimarisha uwekezaji huu," alisema.

“Tanzania ni ya pili kwa idadi ya mifugo baada ya Ethiopia barani Afrika, tunahitaji kutumia vema fursa hii kuchakata mazao ya mifugo, vilevile kutumia bidhaa zitokanazo na samaki kutoka kwenye bahari, mito na mabwawa. Lengo la msingi ni kuwa na bidhaa zetu na kuacha kusafirisha bidhaa ghafi ambapo pia tutakuwa tunasafirisha ajira.”

Naye Rais Ramaphosa amesema “Mlitufunza, mlituunga mkono kwa njia nyingi na kutusaidia kiasi kikubwa, tunashukuru kwa dhati. Hii ndio sababu muunganiko wetu si wa kihistoria tu bali wa damu. Kujitoa kwenu muhanga na kutuunga mkono katika mapambano ndio maana leo Afrika Kusini imekuwa huru,” alisema.

Rais Cyril Ramaphosa alisema ameongeza kuwa Tanzania na Afrika Kusini ina urafiki wa miaka mingi, hakuna maneno ya kueleza kwa namna ilivyowasaidia wakati wa kuhangaika, wakati wa kipindi kigumu.

NAIBU WAZIRI MAZINGIRA - MADHARA MAKUBWA ZEBAKI INAPOTUMIKA KAMA SABUNI KUFUA DHAHABU



DALILI zinazoashiria ugonjwa wa saratani zimejitokeza miongoni mwa wachenjuaji wa dhahabu katika mgodi wa Kebaga, kata ya Kenyamanyori Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kutokana na matumizi makubwa ya kemikali aina ya zebaki (mercury).

Lakini cha kushangaza baadhi ya wachenjuaji wa maeneo hayo hawana hofu na hali hiyo wakisema kuwa ni sehemu ya maisha yao ingawa wataalamu wanasema ni hatari kwao.

Uchunguzi umebaini kuwa watu hao hutumia zebaki kuchenjua dhahabu kwa mikono jambo ambalo limewaathiri baadhi yao kubadilika rangi ya asili ya mwili ikiwa ni dalili mbaya.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima pamoja na kulizungumzia hili na kutanabaisha juhudi za Serikali ya Awamu ya 5 pamoja na mipango mikakati ya baadaye pia amefunguka juu ya kile kinachoendelea kupitia kampeni iliyo fanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99% 'KAMPENI YA KUDHIBITI MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI'
Fuatilia yale yaliyojiri kupitia mahojiano yake aliyoyafanya mnamo tarehe na JEMBE FM Radio Mwanza katika ziara yake Kanda ya Ziwa..

SUPER CUP: LIVERPOOL YAILAZA CHELSEA NA KUWA MABINGWA.

Adrian alikuwa shujaa alipozuia penalti ya Tammy Abraham


Liverpool ilishinda kombe la Super Cup kwa mara ya nne katika historia kwa kuilaza Chelsea 5-4 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2 mjini Istanbul.
Kipa Adrian alizuia penalti iliopigwa na mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham kuwapatia ushindi mabingwa hao wa kombe la mabingwa Ulaya.
Chelsea ilikua imechukua uongozi katika kipindi cha kwanza kupitia Olivier Giroud lakini Sadio Mane alifunga mara mbili kuipatia uongozi Liverpool.
Penalti ya Jorginho ilisababisha mikwaju ye penlati kupigwa ambapo Liverpool iliibuka washindi.
Ushindi huo unajiri miezi miwili tu baada ya Jurgen Klopp kushinda taji lake la kwanza kama mkufunzi wa Liverpool wakati alipoiongoza Reds kuishinda Tottenham katika fainali ya kombe la mabingwa (UEFA Champions League).

Wednesday, August 14, 2019

WAZIRI MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar, kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Kamishna Mwandamizi Msaidizi, Fortunatus Musilimu, akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Hamza Kasongo akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Henry Bantu akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Tuesday, August 13, 2019

KWA MARA YA KWANZA MKUU WA MKOA WA MWANZA KUPIGA KURA AKIWA MWANZA.


KWA mara ya kwanza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella atakwenda kupiga kura mkoani pake ni kupitia mabadiliko aliyoyafanya hii leo kupitia daftari la kudumu la wapiga kura.

Mapema leo asubuhi mara baada ya kuzindua rasmi zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani hapa, Mongella amekuwa mtu wa kwanza kuboresha taarifa zake katika kituo cha Polisi eneo la Wazi Mtaa wa Kiseke PPF Kata ya Kiseke Manispaa ya Ilemela anakoishi.
.
.
Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mongella alipiga kura kata ya Miembeni mtaa wa Pwani Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera mahala alipojiandikishia. Hivyo hii inaashiria kua ameepuka kulazimika kusafiri hadi mjini Bukoba kwaajili ya kupiga kura 2019.
.
.
 Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la kudumu la wapiga kura mkoani Mwanza litadumu kwa siku saba kuanzia Agosti 13-19, 2019 katika Wilaya za Ukerewe, Magu, Ilemela, Nyamagana, Sengerema na Misungwi ambapo kwa Wilaya ya Kwimba litaanza Agosti 26, 2019 hadi Septemba 01, 2019.







MAONESHO YA NANE NANE MWANZA 2019 YAMEKUWA KAMA KITAIFA


MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ameipongeza kamati yake ya maandalizi ya maonesho ya KILIMO NANENANE 2019 kwa kufanikisha zoezi la uhamasishaji, ushiriki kwa makampuni na mashirika binafsi, sanjari na mahudhurio ya watazamaji kitendo ambacho kimeyafanya maonesho hayo kuonekana kuwa na taswira ya kipekee.

"Unapohudhuria maonesho haya na kupita kwenye mabanda mbalimbali hakikisha kuwa unatoka na kitu cha kujifunza, kitu cha kufanyia kazi katika mapinduzi yako ya maendelea hususani uwekezaji wako. Wapo wataalamu wakutosha na wawekezaji wengi wenye weredi na tija katika masuala mazima  ya ujasiliamali" Mongella ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameyasema hayo katika maadhimisho ya maonesho ya Nanenane yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja  vya Nyamhongolo jijini Mwanza na kupata mahudurio makubwa licha ya mikoa mingine shiriki kama Mara, Shinya na Simiyu kumegwa nao kuwa na maonesho yao .

Sanjari na hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane 2019 katika Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, Emil Kasagala ametoa taarifa ya Maonesho hayo inayoonesha mafanikio makubwa.

Monday, August 12, 2019

MAJINA YA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA MOROGORO.


Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwatembelea na kuwapa pole majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambao wameungua moto katika ajali iliyotokea jana asubuhi Mjini Morogoro baada ya mafuta yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye lori lililopinduka kulipuka moto. Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 71 mpaka sasa.
Majeruhi 46 wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbi kwa magari ya wagonjwa na helkopta na majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu Mkoani Morogoro. Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa horodha kamili ya majina ya majeruhi hao 43 na watatu waliofariki.

Manchester United YATEMBEZA BAKORA KWA CHELSEA 4-0


Hiki ndicho kilichomkuta Chelsea.

Si kila aliyehusika katika ajali hii alikwenda kuchota mafuta - Rais Magufuli


Rais John Pombe Magufuli amewataka raia nchini kutowahukumu waathirika wa mkasa wa moto uliosababisha vifo vya watu 69 mjini Morogoro siku ya jana. Amesema kwamba huu sio muda wa kulaumiana na badala yake akawashukuru baadhi ya Watanzania waliojitolea kuokoa maisha ya watu.

Akizungumza baada ya kuwasili katika hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuwajulia hali majeruhi, Magufuli amesema kuwa baadhi ya walioathirika na mkasa huo walikuwa wamekwenda eneo la tukio ili kutoa msaada huku wengine wakiwa wapita njia.

''Ninasisitiza, tusiwe majaji, tusiwe wepesi kutoa hukumu, si kila aliyehusika katika ajali hii alikwenda kuchota mafuta, wengine walikuwa wanapita tu, wengine walikwenda kuokoa, wengine walikuwa na shughuli zao. Mwingine alikuwa safarini kuelekea Mtwara, akazuiliwa na moto ulipolipuka ukamkuta'', alisema Rais Magufuli..

Hatua hiyo inajiri baada ya Jukwaa la Wahariri nchini kusema kwamba vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya miongoni mwa watu wanaochukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu ilioanza katika miaka ya hivi karibuni.

TANZANIA YATWAA KOMBE LA COSAFA U201 WANAWAKE.


Timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Zambia leo Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.

Mabao ya Tanzania inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime anayesaidiwa na Edna Lema yamefungwa na Opa Clement dakika ya 24 na Protasia Mbunde dakika ya 87.

Ushindi huo pia ni sawa na kulipa kisasi kwa Tanzanite baada ya kufungwa mabao 2-1 pia na Zambia katika mchezo wa awali, kwenye Kundi B. Ikumbukwe Tanzania iliingia fainali baada ya kuwafunga wenyeji, Afrika Kusini Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.

Sunday, August 11, 2019

SABABU YA KUPANDA BEI YA MAJI JIJINI MWANZA YAELEZWA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko mapya ya ankra za maji huku ikitumia fursa hiyo kuwaelekeza wafanyabiashara wa maji kwamba bei elekezi kwa ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 tu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga alitoa ufafanuzi huo Agosti 09, 2019 kwenye ziara ya waandishi wa habari mkoani Mwanza kutembelea miradi mbalimbali ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza utendaji kazi wake.

Meza kuu:- Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (chini pichani)  kuhusu miradi ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo pamoja na ongezeko la bei mpya ya maji.
Wanahabari ndani ya kusanyiko.
Yanayojiri ubaoni.

Kabla ya MWAUWASA kuwasilisha EWURA mapendekezo ya kufanya mabadiliko ya bei, ilipewa kibali na Wizara ya Maji cha kuendelea na hatua za kuwasilisha EWURA maombi ya kuongeza bei za huduma ya majisafi na usafi wa mazingira

Mara baada ya kupewa kibali na Wizara, mnamo Tarehe 15/01/2019, MWAUWASA iliitisha kikao cha Wennyeviti wa Serikali za mitaa Jijini Mwanza, Baraza la Watumiaji wa huduma za maji (EWURA CCC) na Makundi mbalimbali ya wateja wanaotumia huduma za majisafi na usafi wa mazingira. Wadau hawa walielezwa bayana nia, umuhimu na uhalisia wa kufanya mabadiliko ya bei za maji iliyolenga kuboresha huduma hiyo, ambapo wadau wote walioalikwa waliridhia na kukubaliana na mpango wa MWAUWASA kufanya mabadiliko ya bei za maji.
 Ziara imeanzia katika maabara ya Kituo cha Chanzo cha Maji Capripoint wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.
 Wanahabari pia walitembelea mradi mpya wa maji Nyahiti wilayani Misungwi na kushuhudia kwa mara ya kwanza mashine za kusukuma maji zikiwashwa kwenye mradi huo.


Ziara hii iliratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) ikilenga pia kuimarisha mahusiano na MWAUWASA.

 Mwanahabari George Binagi akichukuwa matirio katika Kituo Cha Mradi wa Maji Nyahiti, wilayani Misungwi.
 Muonekano wa Ziwa Victoria toka chanzo cha Maji na Kituo Cha Tiba ya Maji Capripoint. 
 Eneo kubwa la jiji la Mwanza ni Mabonde na milima.

Baadhi ya Maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji ambayo MWAUWASA imekusiudia kuboresha huduma hii ni pamoja na Kisesa, Bujora, Buhongwa, Kiseke, Nyasaka Islamic, Nyaaka Riverside, Ibanda, Buswelu, Nyamhongolo, Kishiri, Nyagezi Kalifonia, Ihila, Mwashi, Shadi, Biugarika, Nyakurunduma, Mabumbani, Mahina, Tambuka Reli na Maeneo mengine yaliyo kwenye miinuko Jijini Mwanza.
Wanahabari ziarani Misungwi. Hii ni taswira toka juu ya a Kituo Cha Mradi wa Maji Nyahiti, wilayani humo.