Rais Magufuli, amesema hakuna uchaguzi mwingine katika kuhakikisha Afrika inaondokana na unyonge zaidi ya kuungana katika mapambano ya kiuchumi.
Amesema hayo akiwa na mgeni wake Rais Cyril Ramaphosa wakati wa jukwa la baishara kati ya wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Kusini na Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo ambapo amesisitiza kuwa hakuna kinacheweza kuzuia Afrika kuwa na maendeleo.
Rais Magufuli alisema, zaidia ya asilimia 70 ya uzalishaji katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) bidhaa zinakwenda Afrika Kusini. Alisisitiza, bidhaa nyingi zinakwenda Afrika Kusini ikiwemo mbogamboga na matunda, nafaka, vinywaji, mpira na huduma za usafiri.
Rais Magufuli amebainisha kuwa , Afrika Kusini ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini ambapo kwa mwaka jana 2018 mauzo katika biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 5.3,” alisema.
“Afrika Kusini ni ya 13 kwa uwekezaji nchini, takwimu zinaonyesha uhusiano wetu katika uchumi ni mkubwa, maendeleo haya yanaonyesha urafiki wetu wa kibiashara, kiuchumi, kijamii na kisiasa unaimarisha uwekezaji huu," alisema.
“Tanzania ni ya pili kwa idadi ya mifugo baada ya Ethiopia barani Afrika, tunahitaji kutumia vema fursa hii kuchakata mazao ya mifugo, vilevile kutumia bidhaa zitokanazo na samaki kutoka kwenye bahari, mito na mabwawa. Lengo la msingi ni kuwa na bidhaa zetu na kuacha kusafirisha bidhaa ghafi ambapo pia tutakuwa tunasafirisha ajira.”
Naye Rais Ramaphosa amesema “Mlitufunza, mlituunga mkono kwa njia nyingi na kutusaidia kiasi kikubwa, tunashukuru kwa dhati. Hii ndio sababu muunganiko wetu si wa kihistoria tu bali wa damu. Kujitoa kwenu muhanga na kutuunga mkono katika mapambano ndio maana leo Afrika Kusini imekuwa huru,” alisema.
Rais Cyril Ramaphosa alisema ameongeza kuwa Tanzania na Afrika Kusini ina urafiki wa miaka mingi, hakuna maneno ya kueleza kwa namna ilivyowasaidia wakati wa kuhangaika, wakati wa kipindi kigumu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.