Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiongoza Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Aliyesimama ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee akizungumza wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Wanja Mtawazo akizungumza mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku akimpitisha katika randama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Jeshi la Magereza nchini limedhamiria kuanzisha Kiwanda cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga ili kwenda sambamba ya dhana ya Viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa leo Machi,20 na Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku wakati akiwasilisha maelezo ya Randama kuhusu Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo kwa mwaka 2020/2021 mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
“Katika mpango wa bajeti wa mwaka 2020/2021 Jeshi limeweka vipaumbele katika maeneo ya ajira na maendeleo ya watumishi, utawala wa magereza, uboreshaji miundombinu ya majengo ya magereza, kuimarisha shughuli za kilimo ili kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha shughuli za Shirika la Magereza na kuimarisha shughuli za Viwanda ikiwepo Ujengaji wa Kiwanda cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga kilichopo jijini Dar es Salaam” alisema SACP Kitiku
Akizungumza wakati akichangia hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene aliwataka Jeshi la Magereza pindi mradi huo utakapoanza watengeneze mkate bora wakizingatia suala nzima la masoko, teknolojia bora ikiwepo ladha ya mkate huo, vifungashio vyake ili waweze kwenda sambamba na hitajio la mtumiaji wa mwisho
“Ni wazo zuri kwa mlichopanga kwani mtakapofanikiwa mtakua mmeongeza kipato na ile dhana ya jeshi la magereza kujitegemea itakua sasa imeingia kwenye utekelezaji sambamba na kujitosheleza kwa chakula cha kulisha wafungwa, lakini katika mpango huo lazima baadhi ya mambo muyafanyie utafiti ikiwepo soko linataka nini, teknolojia mtakayotumia muhakikishe ni nzuri itakayowafanya mpate bidhaa yenye ladha nzuri sambamba na kifungashio cha bidhaa hiyo, ni vizuri mmeliweka wazo wazi mapema nadhani mtapata michango ya kuliboresha” alisema Simbachawene
Jeshi la Magereza limeomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 201,251.298,000/- katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo huku likiweka lengo la kukusanya maduhuli ya Shilingi 2,000,000.000/- kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.