ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 20, 2020

RAIA 51 WA KIGENI WANASWA KICHAKANI WILAYANI BAGAMOYO MKOANI PWANI

 Baadhi ya wahamiaji haramu 51 ambao ni raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kwa kos ala kuingia nchini bila ya kibali wakiwa wamekamatwa wakiwa wamejificha katika kichaka ambacho kipo karibu na pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya hindi(Picha na Victor Masangu)

Baadhi ya wahamiaji haramu 51 ambao ni raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kwa kos ala kuingia nchini bila ya kibali wakiwa wamekamatwa wakiwa wamejificha katika kichaka ambacho kipo karibu na pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya hindi(Picha na Victor Masangu)

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Zainabu Kawawa akiwa ananawa mikono baada ya kutoka kuwaangalia wahamiaji haramu  wapatao 51 ambao wamekamatwa kwa kuingia nchini bila ya kuwa na kibali maalumu katika maeneo ya kichaka kimoja kilichopo ufukweni mwa bahari ,(Picha na Victor Masangu)
 Baadhi ya wahamiaji haramu raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kutokana na kuingia  nchini bila ya kuwa na kibali wakiwa katika moja ya kituo cha afya kwa ajili ya kuangaliwa afya zao ikiwemo kuwapima kama wanamaambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.(Picha na Victor Masangu)
 Mwonekano wa basi ambalo limewabeba wahamiaji hao haramu wapatao 51 ambao wamekamatwa kwa kosa la kuingia nchini bila ya kuwa na kibali ambao serikali ya Wilaya ya Bagamoyo chini ya Mwenyekiti wake Zainabu Kawawa imeamua kuwapeleka katika eneo maalumu ili kuepukana kama watakuwa na maambukizi wa ugonjwa wa Corona.(PICHA Victor Masangu)
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata Wahamiaji haramu 51 walioingia nchini kupitia bandari bubu ya ya Makurunge Tarafa ya Yombo Wilayani Bagamoyo Mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani  Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alisema wahamiaji hao walikamatwa  majira ya saa 11 alfajiri Mach 19.

Wankyo alisema, watuhumiwa hao walikabidhiwa kwa vyombo vingine vya dola kwa taratibu za kisheria  waweze kuchukuliwa hatua.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa alisema, wahamiaji hao wamekutwa katika pori wakiwa katika harakati za kutafuta usafiri kuelekea Mikoa ya Nyanda za juu Kusini ili waweze kuendelea  na safari yao hadi Afrika Kusini.

Kawawa lisema, Wahamiaji hao walikuwa wanaotokea nchini Ethiopia, ambao katika mahojiano ya awali walikiri kuingia Nchini kwa kupitia Pwani ya Bagamoyo, wakitumia majahazi. 

Alisema, Wahamiaji hao walichukuliwa hadi katika kituo cha Afya Matimbwa (Bagamoyo) ili kupimwa kama Wana maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kituo hicho kilichotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Corona wanaoweza kujitokeza siku za usoni, .

Wahamiaji hao, wamefikishwa katika kituo hicho ili kufanyiwa vipimo vya awali kujiridhisha kama hawana maambukizi ya ugonjwa wa Corona,  kabla ya kupelekwa katika gereza la Kigongoni  Wilayani Bagamoyo wakisubiri kusomewa mashtaka yao ya kuingia Nchini bila kibali


Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji na kufukia mwili wa marehemu..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alisema, watuhumiwa hao walikamatwa Machi 19 huko Kibindu Wilaya ya Bagamoyo wakituhumiwa kuua na kuzika mwili wa marehemu (jina linahifadhiwa)katika shamba la mahindi.

Wankyo alisema, Machi 3, majira ya saa nane mchana huko Kibindu mtuhumiwa Chacha Machangu (27) alimfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine .

Kamanda alisema, Machangu alimshambulia mke wake kwa kumkata na panga maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo.

Wankyo alisema, Machangu kwa kushirikiana na ndugu zake Emmanuel Machangu (19) na Hamis Machangu (22 walichimba shimo kwenye shamba la mahindi na kufukia mwili wa marehemu.

Kamanda alibainisha kuwa, Machi 19 Jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu ambao walionyesha shimo lilipo na lilipofukuliwa mwili wa marehemu ulipatikana.

Alisema, mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kufanyiwa mazishi kwa kufuata taratibu.

Jeshi hilo limesema, bado linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushiriki katika tukio hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.