ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 1, 2011

BURIANI SALUM KABUNDA 'NINJA'

Aliyekuwa beki wa zamani wa Dar es salaam Young Africans Salum Kabunda 'Ninja' amezikwa leo kwenye makaburi ya Kirumba jijini mwanza.Hayati Salum Kabunda 'Ninja'.

Salum kabunda aliaga dunia jana ijumaa majira ya usiku saa 2 na robo akiugulia nyumbani kwa mama yake mzazi mtaa wa Nela jijini hapa. Marehemu ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto wa 5 wa familia ya Mzee Hassan kimwaga ameacha mjane na watoto wanne akiwemo Hassan Kabunda ambaye yuko katika kambi ya michezo ya Kanali Kipingu.

Timu alizopitia ni pamoja na Dar es salaam Relwe, Waziri mkuu Dodoma ambako aliungana na akina Godwin Aswile kisha baadaye wakachukuliwa na tajiri mmoja na kuelekea Tukuyu Stars ya Mbeya ambako Yanga iliwanasa na kuwasajili.

Marehemu Salum Kabunda Ninja' aliisaidia timu ya Taifa iliyoitwa 'Kakakuona' kufika faina ya CECAFA Senior ambapo walipoteza mbele ya Uganda kwa kufungwa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kabla ya kuiwakilisha vyema Tanzania katika mchezo dhidi ya Zambia 'Chipolopolo'

Alitunukiwa jina Ninja kutokana na ufanisi wake kama beki kwa kuweza kuruka style mbalimbali kuondosha hatari langoni mwa timu yake ya Yanga akifananishwa na wacheza filamu maarufu ya miaka ya 90' 'Ninja'

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Amen

SHEREHE YA UZINDUZI WA MWACYA ILIVYOFANA

Mgeni rasmi bw. Yohana Mswahili ambaye pia ni Mkurugenzi wa Managing Patner-M S K Solution akihutubia wanachama wa MWACYA waliohudhulia sherehe hizo za uzinduzi wa chama hicho katika ukumbi wa Nyumbani Hotels Mwanza.

Mwenyekiti wa Mwanza city Youth Association (MWACYA) Faustine Msangira toka GVEP INTERNATION wakati akiwasilisha hotuba ya Ufunguzi.

Diwani wa kata ya Mkolani Mh. Mabula alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa hapa akisaini kitabu cha wageni.

Safu ya meza kuu ya uzinduzi wa MWACYA, chama chenye usajili wa kudumu wa no. CBO/NYG/117 toka wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.

Sehemu ya mashariki

Sambamba na uzinduzi pia ilifanyika harambee ili kutunisha mfuko wa chama hicho cha vijana wanaoishi na kufanya kazi katika jiji la Mwanza ambapo zaidi ya shilingi milioni kumi zimekusanywa kupitia harambee hiyo.

Wanachama wakijuliana hali, aliyekula suti ni bw. Godwin Kabago wa Nexus Associates Attorneys at law.

Mwonekano smati'

Kona ya wana Habari kutoka kushoto John Maduhu, Lavert Shuku, Ben Star na Fredrick Katulanda.

Mkurugenzi wa Managing Patner Solution ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo bw. Yohana Mswahili akiwasha fataki kama ishara ya uzinduzi.

Wakishuhudia mlipuko ni Mgeni rasmi na mh. diwani.

Mgeni rasmi bw. Yohana Mswahili akizindua Kitabu cha katiba ya Chama cha MWACYA.

Chiaaaazzzz.

Chiaaazzzz!!

Chiaaaazzz!!!!!

Mc Job aka Baba Paroko (shoto) aki show LUV na G. Sengo.

Ni wakati wa burudani...

Wanachama wakishiriki Dance la kwaito.

Part two.

Enjoy

Friday, September 30, 2011

METHALI MUHIMU ZA KISWAHILI...

Yale Masuala Ya Mtihani Wa Kiswahili, Pamoja Na Majawabu Yake Sahihi........
KIJANA WA KIDOSI BAADA YA KUMALIZA TUITION YA KISWAHILI, ANAJIBU IFUATAVYO:


(1) Mfa maji? Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole? Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ? Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua? Uliza google.
(5) Mbio za utelezini? Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga? Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea? iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika? Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa? Takosa guo ya sikukuu...
(10) Kila ndege .....? Hutua Airport
(11) Bandu bandu ....? Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ....? Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya .....? Kama sio gonjwa basi haina njaa
(14) Aisifuye mvua ....? Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ....? Ongeza mwendo au tachelewa fika
(16) Mlanawe hafi nawe ila .....? Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ....? Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ....? Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ....? Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ....? Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ....? Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ....? Taenda Chadema
(23) Bendera ....? Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ....? Peleka Bombay Lakini sio kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ..? Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi? ........ Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua

Thursday, September 29, 2011

DIAMOND, H BABA, DJ CHOKA, DJ MAKEY, GADNA MIMI NA WEWE KUZINDUA NEW STONE CLUB MWANZA IJUMAA HII YA 30.sept.2011

Ile Club maarufu jijini Mwanza, Stone.....baada ya kufungwa miezi kadhaa ambapo ngoma zikivurumishwa katika mjengo wa Mwanza Hotel, Sasa club hiyo mara vuuup!... kisha Bwaaa!!! Ndani ya Eneo Jingine Jipyaaaaa!! Tivol Opoziti na Nyamagana Stadium.

Ijumaa hii ndo mpango mzima.

Ukisha kata tiketi yako basi unakibali cha kula good time.

Sasa unaingia New Stone Club.

Kuchimba dawa: Lady's First...

Kuchimba dawa: Wavuvi Mupooooo!!!!


Ze Dansing Flow.

Wednesday, September 28, 2011

SUTUMUKA NA NGWASUMA LA FM AKADEMIA

Ilikuwa ni ijumaa ya tarehe 23sept2011 ndani ya ukumbi wa Golden Crest PPF Building Mwanza ni Burudani tosha na style mupya toka kwa wazee wa 'ngwasuma balaaa'.

MISS TOURISM DODOMA WABUNGE NDANI....!!!!

MISS UTALII DODOMA 2011/2012 KUSHUDIWA NA WABUNGE, WAKUU WA WILAYA NA MKUU WA MKOA DODOMA
Waheshimiwa wabunge wote wa Majimbo ya mkoa wa Dodoma, wakuu wa Wilaya zote na mkuu wa mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa wageni mashuhuri walio alikwa kuhudhuria shindano la kumpata mrembo wa utalii wa mkoa wa Dodoma 22-10-2011. Shindano hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya New Dodoma hoteli, na kushirikisha jumla ya warembo kumi na tano toka wilaya zote za mkoa wa Dodoma, ambao hivi sasa wana endelea na kambi ya mazoezi katika Hoteli hiyo ya New Dodoma Hotel chini ya mkufunzi wao Neema Isdory (Miss Utalii Njombe 2010/2011) na Tabia Msuta (Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kati 2010/2011.

Shindano hilo ambalo linaandaliwa na Miss Tourism Tanzania Organisation mkoa wa Dodoma, linatarajiwa kuvuta hisia za wakazi wengi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla, kutokana na ubora wa warembo waliojitokeza kuwania Taji hilo kubwa na la pekee la Utalii mkoani Dodoma na ushindani mkubwa uliopo miongoni mwa washiriki. Pia hamasa ya kila Mbunge, mkuu wa wilaya na wananchi kutaka mrembo wa jimbo lake na wilaya yake kushinda taji hilo inachochea ushindani na mvuto zaidi wa shindano hilo na kusababisha karibu kila mkazi na mpenzi wa sanaa ya urembo mkoani humo kutaka kuhudhuria na kushudia balozi wa Utalii wa mkoa huo akipatikana hiyo tarehe 22-10-2011.

Mkurugenzi wa Miss Tourism Organisation Mkoa wa Dodoma Bwana Charles Gabriel amewataka wakazi wa Dodoma na Maeneo ya Jirani kujitokeza kwa wingi katika kushuhudia Mabinti Utalii wa mkoa huo wakionyesha na kutangaza Utamaduni, Utalii, Mitindo na mianya ya uwekezaji ya mkoa wa Dodoma, na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza ngoma na nyimbo za asili ya Dodoma, jukwaani na nje ya jukwaa huku wakitangaza Utalii na Utamaduni wa Majimbo na wilaya zao.

“…….Maandalizi yana endelea vizuri tunaomba wadhamini wajitokeze zaidi kusaidia shindano hili ambalo ndio pekee Alama ya Urithi wa Mkoa wa Dodoma na linalotoa fulsa kwa makampuni, wafanyabiashara na watu binafsi kujitangaza na kutangaza bidhaa zao, kimkoa, kitaifa na hata kimataifa kupitia matangazo ya ukumbini, redioni, magazetini, Televisheni ,Mabango ya Barabarani, Mitaani na katika mitandao ya Tovuti za kitaifa na kimataifa” alisema Charles Gabriel ambaye pia ni Mratibu mkuu wa shindano hilo.

Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Octoba 2011,lakini kutokana na mabadiliko ya kalenda ya mashindano yaliyo fanywa na Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania sasa litafanyika 22/10/2011.

Akithibitisha mabadiliko hayo ya kalenda Rais wa mashindano hayo nchini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bara la Afrika wa Miss Utalii Dunia na Miss Umoja wa Mataifa Gideon Chipungahelo alifafanua kuwa mabadiliko hayo ya kalenda ya kitaifa ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania, pamoja na kulenga kuboresha zaidi mashindano na maandalizi ya fainali za kanda na mikoa ikiwemo kutoa muda na fulsa zaidi kwa waandaaji kpata wadhamini na wadhamini kujitokeza na kujiandaa, pia yamechangiwa pia na mabadiliko ya kalenda ya mashindano ya Dunia na kimataifa, fainali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Kanda maalum za Vyuo Vikuu zitaanza Oktoba 7, 2011 na kukamilika mwanzoni mwa Februari 2012, huku fainali za Taifa zikifanyika kati ya Machi na Aprili 2012 katika mkoa utakao tangazwa katika uzinduzi rasmi wa kauli mbiu na msimu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2011/2012 utakao fanyika sambamba na Fainali za Miss Utalii Dodoma 2011/2012.

Mikoa na kanda karibu zote nchini wapo katika maandalizi ya fainali za mikoa na kanda zao, ikiwemo mikoa ya na tarehe za mashindano yao katika mabano Mara (7-10-2011),Shinyanga (29-10-2011), Njombe ( 26-11-2011), Iringa (28-10-2011),Kanda ya Kusini ( 2-12-2011),Kanda ya Kaskazini ( 3-12-2011),Dodoma ( 22-10-2011),Vyuo Vikuu Kanda ya Kati (8-12-2011),Kanda ya Magharibi (11-12-2011),,Kanda ya Mashariki (4-2-2012),Dar Es Salaam (28-1-2012), Kinondoni (9-12-2011),Temeke (31-12-2012),Ilala (24-12-2011),Pwani (25-12-2011), Kanda ya Ziwa (26-11-2011), Vyuo Vikuu Kanda ya Magharibi (21-1-2012),Morogoro (24-12-2011),Tabora (29-10-2011), aidha kalenda na tarehe kwa fainali za mikoa yote na kanda zote itatangazwa rasmi 5-10-2011 katika mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.

Fainali za mwaka huu katika ngazi zote zinalenga, kuhamasisha na kutilia mkazo zaidi katika kuhamasisha Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Uzalendo kwa taifa na utumiaji wa Bidhaa za Tanzania, vita dhidi ya uharibifu wa Mazingira, Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu ,.Mila Kongwe, Mila Potofu, na vita dhidi ya Ujinga, Umasikini na Maradhi kupitia Utalii.

Wadhamini waliojitokeza ni pamoja na Asante Water, Kifimbo Radio, New Dodoma Hotel, Ngoto Funiture, Royal Vilage, Clouds Fm Radio, TANAPA, Ngorongoro Creater, VETA Hotel, Side Way Lodge, Shabibi Buss Service, Moronga By Makai Enterprises, Tanzania Daima & Sayari News Paper, Image Masters, Papaa Msofe, Zizzuu Fasheni, Dar City College, Kumekucha Action Mart, Viovena & Co LTD, pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Dodoma.

Taarifa hii Imetolewa na Charles Gabriel Mkurugenzi wa Miss Utalii Mkoa wa Dodoma na Kuthibitishwa na Gideon Chipungahelo Rais Miss Utalii Tanzania

Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"
Regard,

Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.
www.misstourismtanzaniaorganisation.blogspot.com

Tuesday, September 27, 2011

MAHMOOD KITANO & REHEMA NA CHEREKO LAO.

Mahmood Kitano akiwa na mkewe Rehema mara baada ya kufunga ndoa katika msikiti wa Makongoro Kirumba Mwanza.

Mara baada ya harusi kufungwa majira ya asubuhi, baadae jioni sherehe ya kufana ilihamia katika ukumbi wa uwanja wa michezo wa CCM Kirumba.

Msafara toka Tilapia Hotel kupitia barabara ya Kenyeta hatimaye barabara ya Makongoro to CCM Kirumba.

Mashoster.

Mabeste.

Keki na maharusi.

To bi. harusi.

To bwana harusi

Maharusi stape kwa stape kuwakabidhi wazazi.

Bi harusi akiwakabidhi wazazi wa mumewe keki, Mama Kitano mpokeaji huku Mr kitano (kushoto) akipiga makofi.

Kamati kuu ya Harusi haikusahaulika.

Mchana Ilikuwaje?Huko nyumbani kwa bwana harusi majira ya mchana kulikuwa na pilikapilika nzito.

Ng'ombe zisizo na idadi zilichinjwa bwana!

Rejea Usiku.Vijana wa masauti Akudo Sound walishuka kukamilisha sekta ya burudani kwani sherehe ilianza saa 11 jioni hadi saa 2 asubuhi siku inayofuata, Unacheza weeee!!!.

Ngoma asili nazo zilikuwepo, za wahaya, wakerewe na wajita.

Wabunge Hayness na Wenje wote ndani ya nyumba.

Dance....dance.

FAIR PLAY.COM JKT OLJORO YALAMBA POINTI ZOTE LAKE VICTORIA.

Mshambuliaji wa timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza akisaidiana na daktari wa timu ya JKT Oljoro kubeba machela kumtoa mchezaji wa JKT Oljoro nje ya uwanja kupata matibabu katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa dimba la CCM Kirumba.

Majeruhi akiwa tayari amefikishwa nje na soka liendelee.

JKT Oljoro.
Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Toto kufungwa nyumbani. Goli la kwanza la JKT Oljoro lilipatikana dakika ya 6 mfungaji Sunday Mussa baada ya kupokea pasi toka safi yake Paul Nonde, mfungaji alipiga shuti katikati ya mabeki wa toto Laban Kandole na Ladislaus Mbogo lililomshinda kipa wa toto. Goli la pili lilifungwa na Karage Ngunda. Mwisho JKT Oljoro 2 Toto 0.

UTAKUMBUKWA DAIMA PROF WANGARI MAATHAI

Mtunukiwa wa tuzo ya Amani ya Nobel Prof Wangari Maathai ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 71.

Mwanaharakati huyo mashuhuri wa mazingira na haki za binadamu wa Kenya Profesa Wangari Maathai amefariki dunia mjini Nairobi usiku wa kuamkia , Jumatatu kutokana na maradhi ya saratani.

Prof Karanja Njoroge ambaye ni mkurugenzi wa Green Belt Movement, shirika ambalo Prof Maathai alilianzisha amethibitisha kifo hicho. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Prof Njoroge amesema wakati wa kifo chake Wangari alikuwa na wanafamilia na marafiki. Marehemu ameacha watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.

Profesa Wangari Maathai alipata tuzo la amani ya Nobel mwaka 2004, kufuatia juhudi za kupigania uhifadhi wa mazingira nchini Kenya.

Mbali ya kuwa Mwanaharakati wa Maswala ya Mazingira na haki za binadamu , Wangari Maathai pia alikuwa mwanasiasa shupavu. Amewahi kuhudumu kama Mbunge na Naibu waziri wa Mazingira nchini Kenya.

Prof Maathai pia katika uhai wake alipata tuzo mbalimbali za kimataifa kwa kutambua mchango wake. Prof. Wangari Muta Maathai alianzisha vuguvugu la Green Belt mnamo mwaka 1977, ambapo alifanya kazi na wanawake kote nchini kuboresha maslahi yao na kuhifadhi mazingira.

Alikuwa mtetezi mashuhuri wa matumizi bora ya mali asili . Shughuli zake zilitambuliwa mara kwa mara kote duniani