ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 1, 2017

MKUU WA WILAYA YA GEITA.,MWAL HERMAN KAPUFI AMEONGOZA MAMIA KUUHAGA MWILI WA ALIYEUWA MWAKILISHI WA CHANNEL TEN MKOA WA GEITA

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Valence Robart Mulamula ukiwa nje ya nyumba yao kwaajili ya heshima ya mwisho kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makazi yake ya milele.
Baba wa Marehemu wa katika kati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robart.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ua mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita.
Mwili wa Marehemu Valence Robart ukitolewa Nje.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robart.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji  Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robart.
Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili.
Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili wa marehemu Valence Robart.Marehemu Valence Robert alianza kusumbuliwa na maradhi mwaka jana mwishoni na katika juhudi za kutafuta matibabu alipelekwa jijini mwanza ambapo  alipatiwa matibabu na kurudia hali yake ya awali na kuendelea na Majukumu yake ya kazi lakini Mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa pili hali yake ya afya ilibadirika na kupelekea kuzidiwa mwezi wa tatu hali ambayo ilimrazimu kurudi Nyumbani kwaajili ya matibabu.

Kwa Mujibu wa Mzazi wake wa Kiume ,Mzee Robert Mulamula alisema kuwa hali yake ilibadirika ghafra siku ya juma nne ya tarehe 28 na walipo kuwa katika jitihada za kutaka kumkimbiza hospitali hali ilibadirika na kupelekea kukata kauli .

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwilimu Herman Kapufi amewataka wazazi kuwa na Moyo wa subira na kuachana na dhana ambazo zimekuwa zikiibuka pindi mtu anapofariki kuwa amelogwa na kwamba jambo hilo sio la kweli kwani marehemu alikuwa ni mgonjwa kama ambavyo wengine wamekuwa wakiugua.

Akimwakilisha Mbunge wa viti maalum kwa Tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Mkoani Geita Upendo Peneza  katibu wake Shida Mpondi alisema kuwa mbunge huyo ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu Valence Robart alikuwa ni mtu wa karibu ambaye walikuwa wakishirikiana katika kazi za ujenzi wa Taifa.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola ,aliwaasa wanajamii ,ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu kuendelea kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwani hayupo hajuae siku wala saa ya kuondoka Duniani.

Marehemu  Valence Robart wakati wa uhai wake ameshawai kuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na gazeti la Tanzania daima Mkoani Geita.

Na alizaliwa Tarehe 9mwezi wa 11 mwaka 1986 katika kijiji cha Mugana Wilayani Misenyi Mkoani Kagera akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya mzee Robart Mulamula na alifariki tarehe 28 mwezi wa 3 mwaka 2017.

Siku ya jana ya tarehe 30 mwezi wa March mwaka huu  amezikwa katika kijiji ambacho amezaliwa.

Kwa niaba ya wasomaji wa Mtandao wa Maduka Online inatoa pole kwa familia kwa kuondokewa na kijana wao Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake ribarikiwe.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

Thursday, March 30, 2017

KAMBI YA UPINZANI CONGO YAWATAKA WANANCHI KUNZISHA OPERESHENI "MJI WA MAZIMWI"


KAMBI ya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewataka wananchi wa nchi hiyo kuketi majumbani mwao Jumatatu ijayo na kutotoka nje ili kumlazimisha Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka. 
Taarifa iliyotolewa na muungano wa kambi ya upinzani imesema kambi hiyo itaanzisha operesheni ya "mji wa mazimwi" kwa ajili ya kusimamisha shughuli zote kote nchini Congo.

Muungano huo  umesema machafuko ya sasa nchini humo yamesababishwa na hatua ya Rais Joseph Kabila ya kukataa kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka yaliyotiwa saini Disemba 31 mwaka jana.

Makubaliano hayo ambayo yalisimamiwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki, yalimruhusu Rais Kabila kubakia madarakani baada ya kumalizika muhula wake wa uongozi hadi mwishoni mwa mwaka huu sambamba na kuunda serikali ya mseto itakayoongozwa na Waziri Mkuu atakayetoka kambi ya upinzani.
Rais Joseph Kabila wa Congo

Makumi ya raia wameuawa katika machafuko na maandamano ya raia wa Congo DR wanaomtaka Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila ang'atuke madarakani.  

FULL TIME: SERENGETI BOYS 3 vs 0 BURUNDI


Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana
maarufu kwa jina la Serengeti Boys. 


Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni  Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha  na habari/ Faustine Ruta.

Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Kaitaba


Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys

Taswira kabla ya mtanange

Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys

Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange

Picha ya pamoja

Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi.
Picha  na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara  bila Kiingilio!!!

Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati


Kipa hakuona kitu!

Nahodha wa Serengeti Boys  Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.

Bao tatu 3-0

Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati


Shangwe! 3-0

Chupuchupu afunge bao lingine!

Assad Ally Juma wa Serengeti Boys(kushoto) akiufukuzia mpira

Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni

Kibabane tena na mpira

Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi

Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja

Dakika 90 zilikamilika