KAMBI ya upinzani katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo imewataka wananchi wa nchi hiyo kuketi majumbani
mwao Jumatatu ijayo na kutotoka nje ili kumlazimisha Rais Joseph Kabila
wa nchi hiyo kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka.
Taarifa iliyotolewa na muungano wa kambi ya upinzani imesema
kambi hiyo itaanzisha operesheni ya "mji wa mazimwi" kwa ajili ya
kusimamisha shughuli zote kote nchini Congo.Muungano huo umesema machafuko ya sasa nchini humo yamesababishwa na hatua ya Rais Joseph Kabila ya kukataa kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka yaliyotiwa saini Disemba 31 mwaka jana.
Makubaliano hayo ambayo yalisimamiwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki, yalimruhusu Rais Kabila kubakia madarakani baada ya kumalizika muhula wake wa uongozi hadi mwishoni mwa mwaka huu sambamba na kuunda serikali ya mseto itakayoongozwa na Waziri Mkuu atakayetoka kambi ya upinzani.
Rais Joseph Kabila wa Congo |
Makumi ya raia wameuawa katika machafuko na maandamano ya raia wa
Congo DR wanaomtaka Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila ang'atuke
madarakani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.