ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 12, 2024

MSIGWA ASIFU 'Zogo Mchongo’ YA BENKI YA CRDB KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA UMMA.

 

Dar es Salaam. Tarehe 11 Julai 2024: Akizindua msimu wa pili wa kipindi maalum cha televisheni cha elimu ya fedha kwa umma cha zogo mchongo kinachoandaliwa na Benki ya CRDB, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa  na Michezo, Gerson Msigwa amesifu jitihada hizo zinazolenga kuwakomboa wananchi kiuchumi hali itakayowasaidia kuondokana na umasikini.

Msigwa amesema elimu ya fedha itakayotolewa katika kipindi hiki cha Zogo Mchongo kupitia televisheni ya Clouds, itawafungua Watanzania wengi juu ya fursa zilizopo kwenye taasisi za fedha zikiongozwa na Benki ya CRDB. Maarifa watakayoyapata pia yatawasaidia kujikomboa kiuchumi na kuliwezesha taifa kuyafikia malengo ya kuwa na uchumi jumuishi,” amesema Msigwa.
Katibu mkuu huyo amesema kipindi hicho cha elimu ya fedha pia kinakwenda kusaidia kupambana na maadui wawili kati ya watatu waliotajwa na Mwalimu Nyerere ambao ni ujinga na umasikini na hilo likifanyika rahisi jamii kukabiliana na magonjwa. “Ukishapambana na ujinga na umasikini ni rahisi kutafuta maarifa mengine yakiwamo ya kukabiliana na maradhi,” amesema Msigwa.

“Nawapongeza Benki ya CRDB kwa jitihada zenu za kuwaelimisha Watanzania. Kila mmoja akishiriki katika hili itakuwa rahisi kufanikisha malengo ya serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha maisha ya Watanzania,” amesema Msigwa.
Aidha, Msigwa amesema kuwa fedha nyingi nchini zinazunguka kwenye sekta isiyo rasmi kwasababu wananchi wengi hawafahamu faida za matumizi ya huduma za benki. Kutokana na hivyo, Wajasiriamali wengi wamekuwa wakijinyima fursa za kunufaika na mikopo pamoja na huduma nyingine za benki.

“Ni imani yangu kipindi hiki cha Zongo Mchongo kitawafungua macho na kuwawezesha kuchangamkia fursa zitakazosaidia kukuza biashara zao na uchumi wa taifa letu,” ameongezea Msigwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kipindi hicho cha Zogo Mchongo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu ya Fedha (2021/22 – 2025/26) unaolenga kuongeza ufahamu na matumizi ya huduma za fedha kwa wananchi.
Mbali na hayo, Nsekela alibainisha kuwa Zogo Mchongo imekuwa jukwaa muhimu la kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na akaunti za benki, kuwekeza, na kutumia huduma za kifedha kwa usalama na ufanisi. Hii ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya kujumuisha kifedha na kuimarisha uchumi wa taifa kwa ujumla.

“Tukiwa Benki kiongozi ya kizalendo tunawajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya fedha kwani kwa kufanya hivyo sio tu tunasaidia kuchochea ujumuishi wa kifedha bali pia wa kiuchumi kwani elimu hii itasaidia watu kuchangamkia fursa za kiuchumi kutokana na maarifa waliyonayo ya huduma za fedha ambazo zinatolewa na Benki yao ya CRDB,” amesema Nsekela.
Nsekela aliongeza kuwa kupitia programu mbalimbali za elimu na uwezeshaji kwa jamii, Benki ya CRDB inaendelea kujitolea katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia watu wengi zaidi, hususan wale wa vijijini na maeneo yasiyo na huduma za benki.

Joseline Kamuhanda, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, amesema kuwa msimu wa kwanza wa Zogo Mchongo ulikuwa na mafanikio makubwa, na kutokana na mafanikio hayo, wamefanya maboresho makubwa ili kurahisisha uelewa kwa watazamaji wa kipindi hiki kinachorushwa na Clouds TV.
"Msimu huu mpya tumeongeza mada nyingi ambazo zinaelimisha na kuburudisha. Tunataka watazamaji wetu wapate maarifa ya kina kuhusu masuala ya kifedha na waweze kujenga uelewa mzuri zaidi wa jinsi ya kudhibiti na kuwekeza fedha zao. Maboresho haya ni sehemu ya dhamira yetu ya kuendelea kuwahudumia wateja wetu na jamii kwa ujumla." amesema Joseline.

Kipindi cha Zogo Mchongo kinalenga kuongeza ufahamu wa masuala muhimu kama vile bajeti, utunzaji akiba, na namna ya kufanya uwekezaji. Mada zilizoongezwa ni katika msimu huu wa Zogo Mchongo ni pamoja na programu ya IMBEJU ambayo imekuwa kimbilio la vijana na wanawake wajasiriamali kote nchini,  bidhaa kama Hodari kwa wajasiriamali, Huduma zinazofuta misingi ya sharia ‘Al Barakah’,  huduma za Watanzania waishio nje ya nchi ‘Diaspora’, na uwezeshaji kwa biashara.





Wednesday, July 10, 2024

MWENYEKITI CCM KIBAHA MJI APITA KWENYE MASHINA NA MATAWI KUHIMIZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


 NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amefanya ziara ya kushtukiza katika tawi la Bamba kwa Mwenyekiti wa shina kata ya Kongowe kwa lengo la kuweza kujionea mwenendo  mzima wa maandalizi  ya kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Nyamka alisema kwamba kwa sasa chama cha mapinduzi kinajipanga kuanzia ngazi mbali mbali ikiwemo za matawi na mashina na lengo kubwa ni kuwatembelea wanachama na kuwahimiza waweze kujiandikisha kwa mfumo  mpya wa njia ya kielectoniki ili waweze kushiriki katikauchaguzi huo.
"Nimefanya ziara ya kushtukiza katika tawi la Bamba lililopo katika kata ya Kongowe na nia kubwa ni kuwatembelea wanachama wa ccm pamoja na viongozi wa matawi na shina ili niweze kujionea ni namna gani wameweza kujiandaa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa seriakali za mitaa pamoja na kuwahimiza waweze kujiandikisha,"alisema Nyamaka.

Kadhalika Mwenyekiti Nyaamka alisema kwamba katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu wamejipanga vilivyo na lengo lao kubwa ni kushinda kwa kushindo katika mitaa yote hivyo wanachama wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kupata kura nyingi katika uchaguzi huo

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema kwamba kwa sasa ni lazima mitaa yote kushiriki kikamilifu katika kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwataka kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi waliopo madarakani ili  waweze kuendelea kutekeleza miradi  mbali mbali ya maendeleo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.

Monday, July 8, 2024

KAIZER CHIEFS USO KWA USO DHIDI YA YOUNG AFRICANS SC KATIKA MECHI YA KWANZA KOMBE LA TOYOTA


 JOHANNESBURG - Kaizer Chiefs itacheza na wababe wa Tanzania Young Africans SC katika mechi ya kwanza ya Kombe la Toyota itakayochezwa Bloemfontein tarehe 28 Julai.

Mashindano hayo ya kujiandaa na msimu ujao yana hakika yatavutia watu wengi na kutaka kujua kwani yatashuhudia kocha mpya wa Amakhosi, Nasreddine Nabi akiongoza timu yake mpya katika ardhi ya Afrika Kusini kwa mara ya kwanza, na itakuwa dhidi ya timu yake ya zamani, ambayo alishinda mataji mawili ya ligi.

Mashabiki wa soka mjini Bloem wako kwenye karamu huku mechi kati ya Chiefs na Yanga itatanguliwa na mechi ya magwiji kati ya wachezaji wa zamani wa Glamour Boys pamoja na wale wa Bloemfontein Celtic.

Wakati tahadhari, wakati wa uzinduzi wa shindano hilo siku ya Jumatatu asubuhi, awali ilikuwa kwenye tukio hilo jipya, pia kulikuwa na uthibitisho wa Nabii kama mtu mpya kwenye usukani baada ya msururu wa uteuzi usio na mafanikio katika miaka michache iliyopita.

Mkurugenzi wa Masoko wa Chiefs, Jessica Motaung, alionyesha ni nini kilimfanya kocha huyo wa Tunisia atoke miongoni mwa baadhi ya wagombea kutoka sehemu mbalimbali duniani, kuwania nafasi hiyo.

"Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo tuliangalia. Mapenzi yake kwa mchezo, mapenzi yake kwa Kaizer Chiefs na uelewa wake wa nafasi ya Afrika na taaluma yake,” Motaung alisema.

Nabi ana rekodi iliyothibitishwa ya mafanikio, na mashabiki wengi wa Chiefs watakuwa na matumaini kwamba atakuwa na athari mara moja kwa klabu ambayo ina kiu ya mafanikio. Ukame wa kombe la Amakhosi umedumu kwa misimu tisa nzima katika hatua hii na wa 10 bila shaka hautastahimilika kwa wafuasi wao.

Ingawa ana matumaini kuhusu uwekezaji walioufanya kwa Nabi, makocha wake wasaidizi na wasaidizi wake watalipa, Motaung alionya kuwa na subira kidogo kwani kurejea siku za utukufu wa klabu na mafanikio ya kudumu yangehitaji Nabi kuweka msingi wa ushindi kwanza.

“Jambo moja tulilojifunza ni kwamba subira ni muhimu. Wakati fulani, tumefanya maamuzi kwa haraka na tukajifunza kutoka kwao. Huu ndio wakati ambao ninaweza kusema kwa wafuasi wetu kwamba tunataka mafanikio endelevu na kwa hilo tunaweka msingi sahihi; tunatakiwa kufanya hivyo kwa pamoja na tunatakiwa kuipa timu muda,” alisema Motaung.

Tikiti za Kombe la Toyota kwa mara ya kwanza zinauzwa rasmi katika maduka yote ya TicketPro nchini Afrika Kusini kutoka chini ya R40. Mashabiki wanaohudhuria mchezo huo wana nafasi ya kujishindia gari jipya kabisa la Toyota Corolla Cross XI CVT lenye thamani ya zaidi ya R400 000.

RASMI YUSUPH ALLY KAGOMA NI MCHEZAJI MPYA WA SIMBA SC

 


KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo wa ulinzi, Yusuph Ally Kagoma (28) kuwa mchezaji mpya kutoka Singida Big Stars kuwa mchezaji wake mpya wa 12 kuelekea msimu ujao.

Wachezaji wengine wapya 11 Simba SC ni mabeki, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya DRC, wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.

Wengine ni kiungo wa ulinzi, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, kiungo mzawa Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma na winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe.

Wapya wengine ni kiungo mshambuliaji, DĂ©bora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia na  washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'AdjamĂ© ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.

Aidha, Simba SC imeleta Kocha Mkuu mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids (43) raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mualgeria Abdelhak Benchika aliyeondoka April 28, mwaka huu.

Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.

Kikosi kinatarajiwa kuondoka Jumatatu kwenda mjini Ismailia nchini Misri kuweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya. 

YANGA YASAJILI BEKÄ° WA KUSHOTO MKONGO KUTOKA ST ELOI LUPOPO

 


KLABU ya Yanga imemtambulisha beki wa kushoto, Chadrack Issaka Boka (24) kutoka St Eloi Lupopo ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao.

Chadrack Issaka Boka anakuwa mchezaji mpya wa tatu tu Yanga baada ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama kutoka Simba na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo kutoka Azam FC.

KOKA AWASOGEZEA HUDUMA YA MATIBABU BURE KWA MASIKIO NA VIFAA VYA KUSIKIA WANANCHI WA JIMBO LAKE.

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Wananchi zaidi ya mia 400 katika Jimbo la Kibaha mjini mkoani Pwani pamoja   na maeneo  ya jirani  wamepatiwa huduma ya matibabu ya  masikio bila malipo  ambapo  baadhi  yao wamepatiwa vifaa vya maalumu kwa ajili ya kuongeza  usikivu  vilivyogharimu kiasi cha shilingi milioni 250.

Vifaa hivyo vya usikivu wa masikio vimetolewa na kufadhiliwa na kwa  kampuni ya Starkey cares  ya nchini Marekani chini ya mmiliki wake William Haston ambaye ni daktari bingwani.

Kambi hiyo ya Matibabu ya siku moja  imefanyika katika hosptali teule ya  Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi  kwa ushirikiano wa Ofisi ya mbunge Jimbo la Kibaha mjini na Kampuni ya Selous Biotechnology  ya Jijini Dar na kuwezesha ujio wa  daktari bingwa Kutoka Marekani

Akizungumza katika kambi hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba aliwasiliana na daktari bingwa kutoka marekani William Austin kwa ajili ya kusaidia vifaa kwa watu wenye matatizo ya masikio.

"Tunashukuru hawa rafiki zetu kutoka marekani kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watu wenye matatizo ya usikivu na kwamba zoezi letu limekwenda vizuri na tulipanga kuwafikia watu 250 lkn tumevuka lengo na kuwafikia watu zaidi ya 400,"alisema Mbunge Koka.

Aidha Koka alibainisha kwamba aliamua kutafuta marafiki kutoka marekani kutokana na kubaini kuwepo kwa wananchi wengi kukabiliwa.na tatizo la masikio na wengine kushindwa kusikia.
Koka alibainisha kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kuwasaidia kwa hali na mali wananchi mbali mbali ambao wamekuwa wana shida hiyo na kuongeza kwamba wananchi wamepatiwa vifaa hivyo bila malipo.

Pia Mbunge huyo alibaisha  kuwa vifaa hivyo  ambavyo wamepatiwa wagonjwa wa masikio  vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo zimetolewa na daktari bingwa huyo kutoka marekani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickosin Simon alisema vifaa ambavyo wananchi wamepatiwa katka kambi la kliniki vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa.

Aidha Mkuu huyo alimpongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa juhudi zake za kuweza kuwezesha ujio wa daktari huyo bingwa kutoka marekani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira mazuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha sekta ya afya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amemshukuru Mbunge Koka kwa kuweza kuwajali na kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo ya matibabu ya masikio.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amani Halima 
Mganga amesema kwamba huduma hiyo imekuja wakati wa muafaka kutokana na uhitaji kuwa ni mkubwa.

Nao Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupatiwa huduma katika kambi hiyo ya kliniki wamesema kwamba ujio wa daktari huyo bingwa umekuwa ni msaada mkubwa kwani wameweza kupata matibabu pamoja na kupewa vifaa  vya usikivu.

Wananchi hao akiwemo Mariam Salumu na Richard Mkanza hawakusita kutoa pongeza na shukrani kwa kuwasaidia upatikanaji wa huduma ya matibabu ya masikio.

Sunday, July 7, 2024

WAZIRI SILAA,RC PWANI WATUA CHAMAKWEZA CHALINZE KUINGILIA KATI SAKATA LA MGOGORO WA ARDHI

VICTOR MASANGU, PWANI

SERIKALI mkoani Pwani imesema haitowafumbia macho watu watakao kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga wananchi wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali na kuliagiza  Jeshi la polisi kuwakamata mara moja wale wote ambao wamehusika kwenye makosa ya hivi karibuni kwani wamekuwa ni chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Abubakari Kunenge wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa ardhi Jerry Silaa yenye lengo la kusikiliza kero na changamoto za  wananchi kutoka vijiji mbali mbali  vilivyopo katika  Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo  ili kuweza  kuzitafutia ufumbuzi.