ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 8, 2024

KOKA AWASOGEZEA HUDUMA YA MATIBABU BURE KWA MASIKIO NA VIFAA VYA KUSIKIA WANANCHI WA JIMBO LAKE.

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Wananchi zaidi ya mia 400 katika Jimbo la Kibaha mjini mkoani Pwani pamoja   na maeneo  ya jirani  wamepatiwa huduma ya matibabu ya  masikio bila malipo  ambapo  baadhi  yao wamepatiwa vifaa vya maalumu kwa ajili ya kuongeza  usikivu  vilivyogharimu kiasi cha shilingi milioni 250.

Vifaa hivyo vya usikivu wa masikio vimetolewa na kufadhiliwa na kwa  kampuni ya Starkey cares  ya nchini Marekani chini ya mmiliki wake William Haston ambaye ni daktari bingwani.

Kambi hiyo ya Matibabu ya siku moja  imefanyika katika hosptali teule ya  Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi  kwa ushirikiano wa Ofisi ya mbunge Jimbo la Kibaha mjini na Kampuni ya Selous Biotechnology  ya Jijini Dar na kuwezesha ujio wa  daktari bingwa Kutoka Marekani

Akizungumza katika kambi hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba aliwasiliana na daktari bingwa kutoka marekani William Austin kwa ajili ya kusaidia vifaa kwa watu wenye matatizo ya masikio.

"Tunashukuru hawa rafiki zetu kutoka marekani kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watu wenye matatizo ya usikivu na kwamba zoezi letu limekwenda vizuri na tulipanga kuwafikia watu 250 lkn tumevuka lengo na kuwafikia watu zaidi ya 400,"alisema Mbunge Koka.

Aidha Koka alibainisha kwamba aliamua kutafuta marafiki kutoka marekani kutokana na kubaini kuwepo kwa wananchi wengi kukabiliwa.na tatizo la masikio na wengine kushindwa kusikia.
Koka alibainisha kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kuwasaidia kwa hali na mali wananchi mbali mbali ambao wamekuwa wana shida hiyo na kuongeza kwamba wananchi wamepatiwa vifaa hivyo bila malipo.

Pia Mbunge huyo alibaisha  kuwa vifaa hivyo  ambavyo wamepatiwa wagonjwa wa masikio  vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo zimetolewa na daktari bingwa huyo kutoka marekani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickosin Simon alisema vifaa ambavyo wananchi wamepatiwa katka kambi la kliniki vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa.

Aidha Mkuu huyo alimpongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa juhudi zake za kuweza kuwezesha ujio wa daktari huyo bingwa kutoka marekani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira mazuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha sekta ya afya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amemshukuru Mbunge Koka kwa kuweza kuwajali na kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo ya matibabu ya masikio.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amani Halima 
Mganga amesema kwamba huduma hiyo imekuja wakati wa muafaka kutokana na uhitaji kuwa ni mkubwa.

Nao Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupatiwa huduma katika kambi hiyo ya kliniki wamesema kwamba ujio wa daktari huyo bingwa umekuwa ni msaada mkubwa kwani wameweza kupata matibabu pamoja na kupewa vifaa  vya usikivu.

Wananchi hao akiwemo Mariam Salumu na Richard Mkanza hawakusita kutoa pongeza na shukrani kwa kuwasaidia upatikanaji wa huduma ya matibabu ya masikio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.