ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 19, 2023

SIMBA SC IMELETA MANUFAA HAYA NCHINI TANZANIA 'UJIO WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE'

 NA ALBERT G. SENGO

- Jeh ni zipi faida zinazotokana na Michuano ya African Football League kwa Taifa la Tanzania? - Ipi nafasi ya Simba Sc katika mashindano ya African Football League? - Kipi kimetokea kikasababisha Congo kugomea uwepo wa udhamini wa 'Visit Rwanda'? Ungana na Mc Suzuki aka Drum Drum akiwa namchambuzi wa michezo kutoka Jembe Fm Raymond Cuthbert. WAKATI HUO HUO UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa uwepo wa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi hicho eneo la uwanja wa mazoezi ni nguvu kubwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 20. Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kinaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wa African Football League utakaochezwa Uwanja wa Mkapa. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Ahmed Ally amesema kuwa kuna wachezaji ambao wanazidi kuimarika na uwezo wao utaonekana Uwanja wa Mkapa. “Kuna mtaalamu wa pasi zenye uhakika kiungo Fabrince Ngoma ana hatari huyo yule ambaye alionekana kwenye ligi atakuwa tofauti kabisa Oktoba 20 dhidi ya Al Ahly. “Sio Ngoma pekee yupo Luis Miquissone wengi wanambeza basi atawaonyesha ubora wake kwa vitendo. Kwenye ulinzi tupo na ukuta imara Che Malone huyu kazi yake inaonekana usisahau kuhusu Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ni watu wa kazi haswa. “Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kwa vitendo hizi burudani kwani ambacho kinatafutwa ni matokeo na huu mchezo tunaamini utakuwa na ushindani sisi tupo tayari,” amesema Ally.

Monday, October 16, 2023

Shirika la JHPIEGO laendesha mbio za hisani kuchangisha fedha za ujenzi wa wodi ya watoto njiti

 

Shirika la JHPIEGO Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Molles limeendesha mbio za hisani za 'Miles For Mothers' ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya Kwimba mkoani Mwanza.

Mbio hizo za kilomita tano, na kilomita kumi zimefanyika Jumapili Oktoba 15, 2025 katika Jiji la Mwanza na Jiji la Dar es salaam ambapo lengo ni kukusanya kiasi cha shilingi milioni 150 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa mbio hizo, Mganga Mkuu Mkoa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha zaidi huduma za mama na mtoto hususani kwa watoto njiti na hivyo kuokoa maisha ya watoto hao.

Amesema jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO pamoja na taasisi ya Doris Mollel zitasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma za watoto njiti katika Wilaya ya Kwimba huku mkakati ukiwa ni huduma hizo kupatikana kila wilaya.

Naye Mshauri Mwandamizi wa shughuli za utekelezaji wa mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAH, Dkt. Riziki Ponsiano amesema fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizo zitasaidia kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo hadi kukamilika litagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akizungumza kwa ni baya ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Mohamed Mtulyakwaku amesema ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya Kwimba utaondoa adha iliyopo ikiwemo kuwasafirisha umbali mrefu hadi Hospitali ya Kanda Bugando.

Katika mbio hizo, washindi wa kilomita tano na kumi wamekabidhiwa medali na vyeti kama sehemu ya kutambua ushiriki wao katika jitihada za kuokoa maisha ya mama na mtoto hususani watoto njiti.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Washiriki wakijiandaa na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizofanyika jijini Mwanza.
Mmoja wa wakimbiaji wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikimbiza upepo jijini Mwanza.
Washiriki wakikimbiza upepo kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizofanyika jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikata upepo jijini Mwanza.
Mshiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikata upepo.
Mmoja wa washiriki wa mbio za 'Miles For Mothers' akikimbiza upepo.
Washiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' 2023 jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizoandaliwa na shirika la JHPIEGO kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Mollel ili kushangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiendelea na mbipo za hisani za 'Miles For Mothers'.
Washirikiwa wakiwa kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zenye lengo la kushangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiwa kwenye mbio za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo katika mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizoandaliwa na shirika la JHPIEGO kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Molles ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers'.
Washiriki wakiwa kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa washindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' umbali wa kilomita tano, jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' umbali wa kilomita tano jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba, Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba, Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Washindi wa mbio za kilomita tano na kilomita kumi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

SERIKALI YAWAAHIDI USHIRIKIANO WAWEKEZAJI

#Azindua mtambo mpya na wa kisasa wa mabati ya rangi

#Ajira 500 kutolewa katika mtambo huo

#Asisitiza Sekta Binafsi kujenga uchumi imara


Imeelezwa kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wenye Viwanda, Wafanyabiashara na Wawekezaji kushiriki katika ukuzaji wa uchumi hususan kwenye Sekta ya Viwanda.


Hayo yamebainishwa leo Oktoba 15, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Mtambo Mpya wa Mabati ya Rangi kampuni ya ALAF jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa, tukio hilo ni sehemu ya matunda ya juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na pia kwa maono yake ya kuiamini Sekta Binafsi katika kujenga uchumi imara wa nchi.

“Napenda kuwaahidi kwamba, wenye viwanda, wafanyabiashara na wawekezaji, Serikali itawapa ushirikiano. Kwa upande wenu, mnao wajibu wa kuzingatia uendelevu wa ubora na tija kulingana na viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa katika shughuli za uzalishaji hatimae kunufaika zaidi na fursa za masoko zilizopo na zinazoendelea kujitokeza,’’ ameeleza Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa ALAF Limited, Bw. Ashish Mistry, Bodi na Menejimenti ya kiwanda cha ALAF kwa kuamua kujenga mtambo huo wa kwanza nchini na wa kisasa utakaotumika kutengeneza mabati ya rangi nchini.


“Nimeelezwa kwamba mtambo huu umegharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 25 na unatarajiwa kutoa ajira kwa watu 500. Ni dhahiri kuwa kukamilika kwake kunatoa mwelekeo mpya kwa Taifa letu kwa kuwa imekuwa ni ndoto ya nchi nyingi za Afrika kuwa na kiwanda kama hiki,” amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amesema kuzinduliwa kwa mtambo huo kunatoa fursa mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huo ikiwemo nafasi za ajira zitakazotolewa na kiwanda hicho kwa Watanzania.


Naye, Mkurugenzi  wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Angenya amesema kuwa kiwanda hicho kimeendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora nchini jambo linalofanya wafanye vizuri katika soko.


Vile vile, Mwenyekiti wa Bodi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Bilinith Mahenge amesema kuwa kituo hicho kimeendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi.


Pamoja na washiriki wengine, hafla hiyo imehudhuriwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa SAFAL Group, Bw. Anders Lindgren, Wakuu wa Wilaya wa Jiji la Dar es salaam, wadau na wafanyakazi kutoka ALAF.