ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 19, 2023

SIMBA SC IMELETA MANUFAA HAYA NCHINI TANZANIA 'UJIO WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE'

 NA ALBERT G. SENGO

- Jeh ni zipi faida zinazotokana na Michuano ya African Football League kwa Taifa la Tanzania? - Ipi nafasi ya Simba Sc katika mashindano ya African Football League? - Kipi kimetokea kikasababisha Congo kugomea uwepo wa udhamini wa 'Visit Rwanda'? Ungana na Mc Suzuki aka Drum Drum akiwa namchambuzi wa michezo kutoka Jembe Fm Raymond Cuthbert. WAKATI HUO HUO UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa uwepo wa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi hicho eneo la uwanja wa mazoezi ni nguvu kubwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 20. Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kinaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wa African Football League utakaochezwa Uwanja wa Mkapa. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Ahmed Ally amesema kuwa kuna wachezaji ambao wanazidi kuimarika na uwezo wao utaonekana Uwanja wa Mkapa. “Kuna mtaalamu wa pasi zenye uhakika kiungo Fabrince Ngoma ana hatari huyo yule ambaye alionekana kwenye ligi atakuwa tofauti kabisa Oktoba 20 dhidi ya Al Ahly. “Sio Ngoma pekee yupo Luis Miquissone wengi wanambeza basi atawaonyesha ubora wake kwa vitendo. Kwenye ulinzi tupo na ukuta imara Che Malone huyu kazi yake inaonekana usisahau kuhusu Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ni watu wa kazi haswa. “Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kwa vitendo hizi burudani kwani ambacho kinatafutwa ni matokeo na huu mchezo tunaamini utakuwa na ushindani sisi tupo tayari,” amesema Ally.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.