ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 2, 2013

OBAMA AZIACHILIA PICHA ZAKE ZA SILAHA SIKU KADHAA KABLA YA MJADALA MZITO WA UMILIKI SILAHA



Obama shoots clay targets with a shotgun
Bang... Rais Obama akiwa kwenye mazoezi ya ulengaji shabaha.


BARACK Obama ameziachia picha zake zikimuonyesha akilenga shabaha kwa kutumia bunduki aina ya smoking shotgun - ikiwa ni siku kadhaa mara baada ya kuzuka kwa mjadala unaohusu umiliki silaha nchini Marekani.


The snap, which shows the US President clay pigeon shooting at his country retreat Camp David, is seen as a bid to appease critics in America's powerful gun lobby.

In a recent interview, Obama said he goes shooting "all the time" on the range in Maryland, near Washington DC.
Angels along a roadside representing the slain children from Newtown, Connecticut
Kumbukumbu... mabango ya malaika pembezoni mwa barabara yakiwakilisha habari za mauajia kwa kutumia silaha hususani kuwakinga watoto na dhahama hiyo.

Obama ametuma makundi kwa makundi ya wataalamu wake wa masuala ya ushauri ili kutia msukumo kuhusu elimu ya matumizi sahihi ya silaha, akiguswa na tukio lililotokea katika shule ya Sandy Hook school massacre, ambapo mtu mmoja mwenye silaha aitwaye Adam Lanza alipouwa watoto wapatao 20 pamoja na walimu sita.

Siku ya jumatatu kambi ya rais Obama itajikita katika mji wa Minnesota kujadili kwa kina na kutia msukumo wa kupunguza matumizi mabaya ya silaha za moto ikiwa ni mikakati mizitoya kuhakikisha kuwa nchi hiyoinapunguza mauaji kwa kutumia risasi, suala ambalo kwa sasa limekuwa sugu ndani ya jamii ya wamarekani.

Pia Rais Obama ametuma waangalizi wake wa kitaifa kufanya uchunguzi wa kina kwa chanzo cha mauaji mengi kutokea, sambamba na kulisimamia vyema zoezi la kurenyuu leseni za umiliki silaha na kuhakikisha kuwa watu wote wenye silaha wanatambulika na hakuna umiliki silaha kinyume cha sheria. Vijarida na magezetimbalimbali yenye maonyo na mafunzo vimesambazwa kwa makusudi ya kuboresha afya ya uelewa wa matumizi sahihi ya silaha.
Gun rights supporters rally in Connecticut, US
Hasira... Waungaji mkono sheria ya umilikisilaha wakiwa kwenye kusanyiko kwenye moja ya miji huko Marekani.

Obama is backing 'common sense' gun control in America
Mabadiliko (Change)... Obama is backing 'common sense' gun control in America, mwandamanaji akiwa alisimama kwa saa kadhaa mahala hapa kwa nia ya kufikisha ujumbe usemao ambapo ndani yake kuna kipande kisemacho "SILAHA HAIUWI MTU, BALI MTU HUUA MTU..."
Kisha akimalizia kwa kauli ya kushangaa inamaana   "TUMECHUKULIA POA..!!"

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA TAWI LA MWANZA.

Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi la Mwanza na kufanya Taasisi kuwa na matawi matano nchini, huku akishuhudiwa na  Mwenyekiti wa MAB - Prof. Isaya Jairo (wa pili kulia) pamoja na mkurugenzi wa TIA Shah Hanzuruni, matawi mengine yapo mikoa ya Mtwara, Mbeya, Singida na Makao Makuu Dar es salaam. 

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, akimkaribisha mgeni rasmi  Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum, kuzindua tawi la Taasisi hiyo ya fedha mkoani Mwanza,  

Hii ni ngoma ya Bujora ambayo hucheza na nyoka na hapa wachezaji wake wakionyesha 'mautundu' katika uzinduzi wa Tawi la Taasisis ya Uhasibu Tanzania (TIA) jijini Mwanza, taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Fedha. 

Ngoma ya kundi la Bujora toka kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za watu wa kabila la wasukuma ambayo hucheza na nyoka na hapa wachezaji wake wakionyesha 'mautundu' zaidi katika uzinduzi wa Tawi la Taasisis ya Uhasibu Tanzania (TIA) jijini Mwanza, taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Fedha.

 "Lekaga tobine Bamping"

Moja kati ya mashuhuda wa tukio, walimu wa taasisi ambao walichanganyika na wananchi.

Mwanza House of talent walifunika mbayaaa na igizo lao.

Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum akifanya ukaguzi kukagua majengo ya madarasa ya chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza.

Moja kati ya madarasa ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza yaliyopo Nyakato Buzuruga wilayani Ilemela.

Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum akifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi  wa Kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza shughuli iliyofanyika jana mkoani hapa.

Kama jiwe linavyosomeka .

Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo. Msikilize kwa kubofya play..

Picha ya pamoja kwa Naibu waziri wa Fedha  Mh. Saada Mkuya Salum pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania tawi la Mwanza.

MAANDAMANO YA KUDAI MAENDELEO KUANDALIWA


Na Shomari Binda
       Musoma,

DIWANI wa kata ya Kigera iliyopo katika Manispaa ya Musoma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Gabriel Ocharo aliliomba Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kuandaa maandamano makubwa yatakayokuwa na lengo la kuishinikiza Serikali kupeleka miradi ya Maendeleo katika Manispaa hiyo.

Ocharo alitoa kauli hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo ambapo alidai Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa ikipitishwa katika vikao vya bajeti imekuwa haitekelezwi hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo kwa Wananchi.

Alisema Miradi hiyo ikiwemo ya ujenzi wa zahanati,nyumba za walimu pamoja na miradi mingine inayotolewa katika bajeti imekuwa haitekelezwi na Serikali na kuiacha Manispaa hiyo ikiwa nyuma katika shughuli za kimaendeleo pamoja na elimu.

Diwani hayu alisema haiwezekani kulikalia kimya suala hilo huku Wananchi wakiendelea kwalalamikia madiwani kwamba hawafanyi kazi wakati Serikali ya (CCM) inashindwa kutimiza wajibu wake wa kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikitolewa.

Nje ya kikao hicho Ocharo aliliambia Gazeti la Mtanzania kuwa hapendi kuamini kama Serikali inashindwa kupeleka miradi ya kimaendeleo katika Manispaa hiyo kwa kuwa inaongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bali anachokisema ni kwa nini miradi ya Maendeleo inashindwa kutekelezwa.

Alisema ipo miradi ambayo ilitangazwa na Serikali katika Diwana wa kata ya Kigera iliyopo katika Manispaa ya Musoma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Gabriel Ocharo aliliomba Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kuandaa maandamano makubwa yatakayokuwa na lengo la kuishinikiza Serikali kupeleka miradi ya Maendeleo katika Manispaa hiyo.

Ocharo alitoa kauli hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo ambapo alidai Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa ikipitishwa katika vikao vya bajeti imekuwa haitekelezwi hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo kwa Wananchi.

Alisema Miradi hiyo ikiwemo ya ujenzi wa zahanati,nyumba za walimu pamoja na miradi mingine inayotolewa katika bajeti imekuwa haitekelezwi na Serikali na kuiacha Manispaa hiyo ikiwa nyuma katika shughuli za kimaendeleo pamoja na elimu.

Diwani hayu alisema haiwezekani kulikalia kimya suala hilo huku Wananchi wakiendelea kwalalamikia madiwani kwamba hawafanyi kazi wakati Serikali ya (CCM) inashindwa kutimiza wajibu wake wa kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikitolewa.

Nje ya kikao hicho Ocharo aliliambia Gazeti la Mtanzania kuwa hapendi kuamini kama Serikali inashindwa kupeleka miradi ya kimaendeleo katika Manispaa hiyo kwa kuwa inaongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo

"AKINA MAMA MWANZA MKO TAYARIiiiiiii.....!!!!?"


Mkurugenzi wa Mikaela Gateway Agency, Idda Ngaiza (kulia) akiwa na moja kati ya wadau wake kwenye matayarisho kuelekea siku ya kongamano kubwa la wanawake lijulikanalo kama Women Dialogue Front litakalo kwenda kufanyika Mwanza kwenye ukumbi wa Hotel JB Belmonte iliyoko jengo la NSSF siku ya tukio ni tarehe 10/3/2013.

Mkurugenzi wa Mikaela Gateway Agency (kushoto) akiteta na Mh. Mama Getrude Mongela ambaye anatajwa kuwa ndiye atakaye kuwa mgeni rasmi wa siku ya kongamano kubwa la wanawake yaani Women Dialogue Front litakalo fanyika Mwanza kwenye ukumbi wa Hotel JB Belmonte iliyoko jengo la NSSF siku ya tukio ni tarehe 10/3/2013.
Kwa mujibu wa mratibu wa Kongamano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mikaela Gateway Agency, Idda Ngaiza amesema kuwa Mh. Vicky Kamata naye amethibitisha kuwepo kwenye kongamano hilo akiahidi pia kuikamata vyema sekta ya Burudani kwa siku hiyo hivyo amewaomba akina mama wajitokeze kwa wingi ili kufaidi mafunzo mazuri yenye manufaa kwa mstakbari wa maendeleo yao na familia zao.

VALENTINE'S DAY DODOMA NA UZINDUZI WA FILAMU YA KUSISIMUA

WAKAZI WA DODOMA JIANDAENI VEMA NA VALENTINE: KWANI TUMEWAANDALIA BONGE LA SHOO LA UZINDUZI WA MOVIE YA EFYANCYA, ALL EYE'S ON ME: SHILOLE NDANI YA NYUMBA PAMOJA NA WASANII WACHEKESHAJI KIBAO: SURPRISE KIBAO ZITAKUWEPO, VILE VILE  WALE WATAOTUPIA PAMBA NA KUPENDEZA ZAIDI WAJIANDAE KWA ZAWADI KIBAO:

Friday, February 1, 2013

WAZIRI WA UCHUKUZI DR.HARSON MWAKYEMBE AMALIZA MZOZO WA KIVUKO CHA SAMMAR III AGIZA KIENDELEE KUTOA HUDUMA ENEO LILILOPO AFUTA AGIZO LA PTA.

Hali ilivyokuwa hii leo mara baada ya kivuko hicho kurejea kazini.
 WAZIRI wa Uchukuzi Dkt..Harrison Mwakyembe ameagiza kivuko cha Mv.Sammar III kiendelee kutoa huduma ya usafiri  ndani ya  eneo la Bandari ya Mwanza Kaskazini linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari nchini PTA.


Agizo hilo la Waziri Mwakyembe limefuta uamuzi wa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari PTA nchini na kumaliza utata wa jambo hilo uliokuwa umezua sitofahamu na hata kutofautiana na agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama la Mkoa wa Mwanza la kukiruhusu Kivuko cha Sammar III kuendelea kutoa huduma katika eneo hilo la Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini Jijini Mwanza.

 Hatua hiyo inafuatia agizo la barua iliyotolewa kutoka kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari (PTA) waliyomwandikia na kumkabidhi Mwekezaji na Mkurugenzi wa Kivuko cha MV.Sammar III  Salum Ally yenye kumbukumbu  NaMN/2/3/04 ya Januari 29 mwaka huu iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari (PTA) Mwanza Richard Msechu,ambapo ilieleza kwamba agizo hilo limetoka na Wizara ya Uchukuzi.

Agizo hilo lilionekana kupingana na lile la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza lililoridhia Kivuko hicho cha MV.Sammar III kuendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na magari kati ya Mwanza na Kamanga Wilayani Sengerema ndani ya eneo la Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini baada ya tamko la awali la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr.Charles Tizeba alilolitoa Desemba 9 mwaka 2012 la kutaka Mamlaka hiyo imuondoe eneo hilo na kumhamishia sehemu nyingine.
Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha (UDP)
 Baada ya taarifa za kuruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na magari, mamia ya wananchi na baadhi ya abiria wanaotumia kivuko cha Sammar III wakiongozwa na Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha (UDP) alisema kwamba uamuzi huo ni bubusara na ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine katika kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia masilahi ya umma.


Aidha alipongeza uamuzi wa Waziri Dr. Mwakyembe umeonyesha kuwa ni mungwana na mtu anayejali sana na hata pengine kuondoa kero za wananchi na kuwajali zaidi badala ya kuangalia masilahi binafisi kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao husababisha hata wananchi kuwachukia na kuilaumu serikali yao iliyopo madarakani.


Wananchi wa Jiji la Mwanza na Kamanga Wilaya ya Sengerema leo asubuhi wamedhuru eneo la kamanga wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti ya kuwapongeza Waziri Dkt.Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo na Kamati yake na Mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja kwa kusimamia na kuondosha kero hiyo kwa kukiruhusu Kivuko cha Sammar III  kuendelea kutoa huduma ya usafiri. 


Mwenyekiti akizungumza kushukuru sakata hilo kumalizika...
Mama Ester ambaye ni mfanyabiashara ya chakula eneo hilo aliwakilisha akina mama kuzungumzia kumalizika kwa sakata hilo.. 
Akina mamalishe nashughuli zao za kipato eneo la Kamanga upande wa Sengerema leo wameendelea na shughuli zao kama kawaida mara baada ya kusitisha zoezi hilo kwa muda wa siku kadhaa wakati kivuko hicho kikiwa kwenye katazo.

 Wananchi wa Kamanga Wilaya ya Sengerema na bango lao.

Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally alisema kwamba anaupokea uamuzi huo wa Waziri kwa mikono miwili, kwa vile ni uamuzi ambao umezingatia kero na adha ambayo wangelipata wananchi lakini pia naye kama mwekezaji kwakuwa alitumia gharama kubwa kuwekeza ikiwemo miundombinu ya eneo la kivuko pande zote mbili Mwanza na Kamanga.

ROYAL OVEN WAGUSWA NA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MWANZA

Uongozi wa kampuni ya Royal Trinity ambao wanamiiki kampuni ya Royal Oven ambao ni waokaji wa mikate jijini Mwanza wakiingia katika lango kuu la kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu cha Upendo Daima kilichopo Lumala jijini Mwanza, kwaajili ya kutoa mchango wao wa chakula mara baada ya kuguswa na maisha waishio watoto wa kituo hicho.


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akikabidhi madaftari kwaajili ya watoto hao waishio katika mazingira magumu cha Upendo Daima kilichopo Lumala jijini Mwanza, ambapo sambamba na kampuni hiyo kutoa vifaa vya elimu pia kampuni hiyo ilitoa mchango wa chakula ikiwa ni mara baada ya kuguswa na maisha waishio watoto wa kituo hicho.


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akimkabidhi mikate na vitafunwa vingine mtoto Isack Lucas kwa niaba ya watoto wote wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Kampuni yauokaji mikate ya Royal Oven iliyopo barabara ya Posta ikitizamana na New Mwanza Hotel pia ilikabidhi vyakula vingine kama Mchele, Unga na Mafuta.
Ekzaud Kiwali akiongea na watoto wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza. Msikilize Bofya Play..


Uongozi wa juu wa kampuni ya Royal Oven pia walipata fursa ya kutembezwa idara mbalimbali za maeneo ya nyumba waishio watoto hao kama sehemu ya ukaguzi kuona changamoto zilizopo. 


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa akiongoza ujio wa wakurugenzi wa Kampuni ya Uokaji Mikate ya Royal oven kuingia kwenye darasa la kituo hicho kama sehemu ya ukaguzi kujionea changamoto zilizopo kituoni hapo.


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa akitoa ufafanuzi kwa Wakurugenzi wa Kampuni ya Uokaji Mikate ya Royal Oven mara baada ya kuingia kwenye darasa la kituo hicho kama sehemu ya ukaguzi kujionea changamoto zilizopo kituoni hapo


Hii ni  moja kati ya sehemu mbili zilizopo kituoni hapa kwa ajili ya kulia chakula ikitumika pia kama maktaba ya kujisomea kituo cha Upendo Daima


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akifurahia matandiko ya watoto wa kituo cha Upendo Daima, kituo ambacho kinaongozwa kwa misingi ya kumjua Mungu (chekshia matandiko)


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa (wapili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kwa Wakurugenzi wa Royal Trinity mara baada ya kuingia kwenye moja ya vyumba vya kulala watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo Lumala jijini Mwanza, kutoka kushoto ni Mwanabure Mberea, Leonard Shayo na Ekzaud Kiwali ambao wote ni Wakurugenzi kampuni ya Royal Trinity.

Msikilize Bofya Play..


Royal Oven pia ilipata picha ya pamoja na watoto hao na walezi wao.
Mkurugenzi wa Royal Trinity Bw. Leonard Shayo akipata pix na  madaktari  wetu wa kesho. Msikilize Bofya Play..


Hisia zinaanzia lango la chumba cha kulala.


Royal Trinity wameamua kutoa msaada kwa kituo hicho ikiwa ili kuungana na makampuni mengine na watanzania wanaoguswa, walio mstari wa mbele kusaidia kuwezesha vituo vya watoto waishio mazingira magumu kuwa na tabasamu, na pia wakiunga mkono kauli za wadau wengine wanaoamini kuwa watoto hawa ni wetu sote.


Meneja wa Royal Trinity ambao ni wamiliki wa kampuni ya uokaji mikate ya Royal Oven, Bi. Carolyne Mhando akifunga lango la kituo cha Upendo Daima ikiwa ni ishara ya kuondoka eneo hilo la kituo na makaribisho ya karibu tena.

Thursday, January 31, 2013

HII NDIYO HALI HALISI SOKO KUU MWANZA LEO

Hebu liperuzi eneo la soko kuu jijini Mwanza kunakouzwa vitunguu, mboga mboga na kunakochinjiwa kuku, jeh unalakusema...!!!!? 

'Buraza' akipata kifungua kinywa.

Ndani nako pilika pilika zikiendelea.

Shughuli zikisonga mazingirani.

SERIKALI IWEKE BAYANA TARATIBU ZILIZOFANIKISHA UAMUZI GESI YA MTWARA


Na.Dkt A. Massawe,

massaweantipas@hotmail.com


Pamoja na habari njema za maelewano kupatikana baina ya Serikali na wenyeji wa Mtwara kuhusiana na swala la gesi asilia ya Mtwara kutumika Dar es Salaam badala ya huko huko Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, ukweli ni kwamba bado hilo sio jibu kwa watanzania wengine wengi ambao bado wanaona kwamba gesi ya Mtwara ilibidi izalishe umeme huko huko Mtwara badala ya Dar es Salaam ili kuwezesha taifa kupata faida kubwa zaidi.

Ukweli ni kwamba upembuzi yakinifu ulikuwa ni muhimu sana ili kubaini faida na hasara za matumizi yote mbada ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme ili kuwezesha ule mbada wenye faida kubwa zaidi kwa taifa kwa kipindi chote cha uhai wa mradi kuchaguliwa.

Hii ni kuzingatia kwamba, uzalishaji wa umeme tarajiwa kutokana na gesi asilia ya Mtwara ni mradi mkubwa unaogharimu fedha nyingi sana na wa muda mrefu na kwamba matumizi mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji umeme ni mingi na inayotofautiana sana kwa gharama na faida kwa vipindi vyote vya uhai wake. Miongoni mwa matumizi hayo mbadala ni yale ya gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme huko huko Mtwara na gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme Dar es Salaam ambayo hutofautiana sana kwa gharama na manufaa kwa taifa kwa vipindi vyote vya uhai wake.

Pia maamuzi ya Serikali kuhusu ni mbadala upi miongoni mwa matumizi ya gesi ya Mtwara mbadala kwa ajili ya uzalishaji wa umeme utumike hapa Tanzania yalibidi yahusishe wataalamu kutoka wizara zote, sekta binafsi na watanzania wote kupitia Bunge lao tukufu kwani matarajio na matakwa ya sekta mbalimbali za kiuchumi hapa nchini kutokana na matumizi mbada ya gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji umeme yanaweza kutofautiana na kupingana sana.

Hivyo, ilibidi upembuzi yakinifu ufanywe kwa kuzingatia mapendekezo ya wataalamu kutoka Wizara zote, sekta binafsi na watanzania wote kwa kupitia Bunge lao tukufu ili kuwezesha kubaini gharama na faida za matumizi yote mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa kuzingatia matarajio na matakwa ya wote kitaifa ili kuwezesha kuchaguliwa kwa ule mbadala wa matumizi ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa umeme unaozingatia matarajio na matakwa ya wote na ulio na manufaa makubwa zaidi kwa wote na kwa taifa lote kwa ujumla kwa kipindi chote cha uhai wake.

Ni vizuri serikali ikaweka bayana vipengele vilivyozingatiwa na taratibu zote zilizofuatwa kuwezesha kuamuliwa na Serikali gesi asilia ya Mtwara izalishe umeme Dar es Salaam badala ya Mtwara.

Naomba kuwasilisha.