Hali ilivyokuwa hii leo mara baada ya kivuko hicho kurejea kazini. |
Agizo
hilo la Waziri Mwakyembe limefuta uamuzi wa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari PTA
nchini na kumaliza utata wa jambo hilo uliokuwa umezua sitofahamu na hata kutofautiana
na agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama la Mkoa wa Mwanza la kukiruhusu Kivuko
cha Sammar III kuendelea kutoa huduma katika eneo hilo la Mamlaka ya Bandari ya
Mwanza Kaskazini Jijini Mwanza.
Agizo
hilo lilionekana kupingana na lile la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Mwanza lililoridhia Kivuko hicho cha MV.Sammar III kuendelee kutoa huduma ya
usafirishaji wa abiria na magari kati ya Mwanza na Kamanga Wilayani Sengerema
ndani ya eneo la Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini baada ya tamko la awali
la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr.Charles Tizeba alilolitoa Desemba 9 mwaka 2012
la kutaka Mamlaka hiyo imuondoe eneo hilo na kumhamishia sehemu nyingine.
Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha (UDP) |
Aidha
alipongeza uamuzi wa Waziri Dr. Mwakyembe umeonyesha kuwa ni mungwana na mtu
anayejali sana na hata pengine kuondoa kero za wananchi na kuwajali zaidi
badala ya kuangalia masilahi binafisi kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao
husababisha hata wananchi kuwachukia na kuilaumu serikali yao iliyopo
madarakani.
Mwenyekiti akizungumza kushukuru sakata hilo kumalizika...
Mama Ester ambaye ni mfanyabiashara ya chakula eneo hilo aliwakilisha akina mama kuzungumzia kumalizika kwa sakata hilo..
Wananchi wa Kamanga Wilaya ya Sengerema na bango lao. |
Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally |
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally alisema kwamba
anaupokea uamuzi huo wa Waziri kwa mikono miwili, kwa vile ni uamuzi ambao umezingatia kero na
adha ambayo wangelipata wananchi lakini pia naye kama mwekezaji kwakuwa
alitumia gharama kubwa kuwekeza ikiwemo miundombinu ya eneo la kivuko pande
zote mbili Mwanza na Kamanga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.