ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 7, 2020

POLISI WANNE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA ZANA UVUVI HARAMU.


JESHI LA POLISI Mkoa wa Mwanza linawashikilia jumla ya watu 6 kwa makosa ya kupatikana na zana haramu za uvuvi, kupatikanana dawa za kulevya (MIRUNGI NA BHANGI), pia linawashikilia kwa uchunguzi askari wake wanne kwa ukiukwaji wa maadili ya kazi wakati wa ukamataji wa watuhumiwa hao. Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Mwanza, Jumanne Muliro ametangaza kuwashikilia askari polisi hao kwa tuhuma za kukiuka kanuni za jeshi hilo za kukamata wahalifu. Jeshi la polisi linaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekenavyo.

DARAJA LINALOUNGANISHA MWANZA NA MUSOMA KUFUNGWA USIKU KWA MUDA WA SIKU 10 KUPISHA UKARABATI.


DARAJA la Simiyu lililopo wilayani Magu barabara kuu ya Mwanza - Musoma litalazimika kufungwa kwa muda kupisha matengenezo makubwa ya kuboresha kwa daraja hilo. Hayo yamesemwa leo Tarehe 6/March/2020 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa darajani hapo akirea jijini Mwanza akitokea mkoani Simiyu kumsindikiza Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu aliyewasili kwaajili ziara ya siku 3 kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo amnbapo anatarajia kuhitimisha ziara yake tarehe 8/03/2020 katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Akiwasilisha taarifa ya ufungwaji wa daraja hilo Meneja  wa Tanroads Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa M. Rubirya alisema watafunga barabara ya Mwanza- Musoma kuanzia Machi 8 hadi 18 mwaka huu ili kupisha matengenezo makubwa ya daraja hilo.
Mhandisi Rubirya ameongeza kuwa wameamua kufanya matengenezo ya haraka ili kujiepusha na hatari zitakazoweza kujitokeza kwa sababu kuchelewa kwa ujenzi huo yaweza kuwa hatarishi kwa watumiaji wa barabara hiyo .
Aliongeza kuwa barabara hiyo itafungwa ili kupisha matengenezo kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11 asubuhi  pia aliomba ushirikiano wa Jeshi la polisi katika kutekeleza kazi hiyo.
Alisema Serikali inampango wa kujenga daraja jipya hivyo hatua zinazofanyika sasa  ni za muda mfupi, aliwataka wananchi kuwa wavumilivu waweze kuboreshewa njia itakayowanufaisha na kuendeleza ujenzi wa taifa.
" Hali halisi ilivyo na nyie mmeiona ninachowaomba muwe wavumilivu ujenzi ufanyike ili kuepusha madhara makubwa ya baadaye" alisema Mhe.Mongella.
Lusia Isack ni mmoja wa wakazi wa Magu akizungumzia adha hiyo alisema wanakuwa wa hofu kila wanapopita kwenye daraja hilo hasa wanapofika katikati hivyo wanaishukuru Serikali kwa kuliona hilo kwani wameweza kutatua changamoto hiyo kabla haijaleta maafa.
"Hili daraja ni bovu sana  ata ukiwa umebebwa kwenye baiskel ukifika katikati daraja linaanza kucheza sasa ukiwa kwenye gari unawaza sijui nitapita salama kwa sababu likidondoka tu sizani kama kuna mtu atakayepona kinachobaki ni kuomba Mungu wakitutengenezea watakuwa wametusaidia sana." alisema Isack.

Hata hivyo daraja hili lililojengwa mwaka 1962 limeanza kuonyesha nyufa baada ya vyuma vilivyokuwa vinalishikilia kukatika jambo hilo limejenga hofu kwa Serikali na watumiaji wa njia hiyo harakati za haraka zinafanyika ili kubadilisha vyuma hivyo .

TANI 31 ZA MIFUKO YA PLASTIKI KUTEKEKEZWA SONGWE

 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila mapema leo akizindua zoezi la uteketezaji wa mifuko ya plastiki ambapo tani 9 kati ya 31 zimeteketezwa katika kichomea taka kilichopo katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika uliopo Wilayani Songwe.
 Sehemu ya tani 9 kati ya 31 za Mifuko ya plastiki ikiteketezwa katika kichomea taka kilichopo katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika uliopo Wilayani Songwe.
 Maafisa wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika uliopo Wilayani Songwe wakihakikisha Sehemu ya tani 9 kati ya 31 za Mifuko ya plastiki zinateketezwa katika kichomea taka kilichopo mgodini hapo ikiwa ni uzinduzi wa uteketezaji wa mifuko hiyo kwa Nyanda za Juu Kusini.
Sehemu ya tani 9 kati ya 31 za Mifuko ya plastiki iliyokamatwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kabla ya kuteketezwa katika kichomea taka kilichopo katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika uliopo Wilayani Songwe.
Tani 31 za Mifuko ya Plastiki iliyo kusanywa kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha Mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe itateketezwa Mkoani Songwe ikiwa ni utekelezaji wa katazo la serikali la matumizi ya mifuko ya plastiski isiyo ya lazima.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila mapema leo amezindua zoezi la uteketezaji wa mifuko ya plastiki ambapo tani 9 kati ya 31 zimeteketezwa katika kichomea taka kilichopo katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika uliopo Wilayani Songwe.
Kafulila amesema licha ya athari nyingi za kiafya kama vile kusababisha magonjwa ya saratani, taka za plastiki zinazoingia katika vyanzo vya maji zinaipelekea dunia kupoteza takribani dola trilioni 2.5 lakini pia tafiti zinabainisha kuwa taka hizo huharibu ubora wa ardhi.
Amesema Serikali ya Tanzania imekuwa kinara wa kutunza mazingira na maliasili kwa kuwa asilimia 70 ya wananchi hutegemea maliasili katika kuendesha maisha yao jambo ambalo ni la kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Ameongeza kuwa  Mkoa wa Songwe utaendelea kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali ya awamu ya tano ambalo linalenga utunzaji wa mazingira huku akisisitiza ngazi zote za uongozi kuanzia Vijiji, halmashauri na Mkoa kushirikiana katika kutekeleza agizo hilo ili kulinda taifa letu kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.
Naye Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Anorld Mapinduzi amesema katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lilianza kutumika rasmi  Juni 01, 2019 na lilitangazwa katika gazeti la serikali namba 349.
Mapinduzi amesema serikali imeruhusu baadhi ya bidhaa zifungashwe na sio kubebewa katika Mifuko ya plastiki na bidhaa hizo ni pamoja na baadhi ya dawa na vifaa tiba, baadhi ya vyakula na mbolea ambavyo visipo fungashwa katika plastiki vitapoteza ubora wake.
Ameongeza kuwa wananchi wasidanganyike kuwa mifuko laini ya plastiki imeruhusuiwa kwani serikali imeruhusu tu matumizi ya vifungashio vya plastiki ambavyo hutengenezwa maalumu kwa ajili ya bidhaa husika, vina nembo ya bidhaa iliyo fungashwa na vitatengenezwa kabla ya bidhaa kuingizwa sokoni.
Mapinduzi amesema lengo la kuteketeza rasmi mifuko ya plastiki ni kutoa ujumbe kwa wananchi waendelee kutambua kuwa serikali bado inapinga matumizi ya mifuko plastiki ambayo ina athari nyingi kwa taifa pia kaguzi mbalimbali zinaendelea na watakao kamatwa adhabu zitatolewa kwa mujibu wa sheria.
Menenja Mazingira wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta New Luika Washington Onyango amesema wako tayari kushirikiana na serikali katika kutunza mazingira na pia uwepo wa kichomea taka katika Mgodi huo ambacho kina ubora utawezesha uteketezaji wa taka katika Mkoa wa Songwe.
Onyango amesema uwezo wa kichomea taka katika mgodi huo ni kuchoma takataka tani moja kwa siku lakini taka ambazo huzalishwa na kuchomwa mgodini hapo ni tani tatu mpaka nne tu jambo ambalo hufanya kichomea taka hicho kufanya kazi chini ya kiwango huku kikiwa  ni rafiki wa mazingira kwakuwa hakiruhusu kemikali kusambaa.

Thursday, March 5, 2020

IDADI YA WATALII YAONGEZEKA NCHINI / MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII KUFANYIKA MWEZI JUNI MWANZA




Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangalla, amesema wizara hiyo kwa mwaka 2018 pekee imepokea watalii milioni 1.5 walioingia na kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo mbuga za wanyama.

 Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa maandalizi wa maonesho ya kimataifa ya Utalii kwenye Kanda ya maziwa makuu yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 19 hadi 21 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Aldof Mkenda akitoa ufafanuzi juu ya kusudio la kufanyika kwa Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Juni 2020 jijini Mwanza.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa rai kwa wadau kuchangamkia fursa za maonesho hayo ya Kimataifa sanjari na kuonesha bidhaa na huduma zilizokusudiwa kuutangaza utalii na si vinginevyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Mpawe Tutuba  

Wadau wa Sekta ya Utalii toka mikoa mbalimbali wakisikiliza kwa makini yanayojiri kwenye   uzinduzi wa maandalizi wa maonesho ya kimataifa ya Utalii. Kanda ya Maziwa Makuu yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 19 hadi 21 mwaka huu.
Wadau wa Sekta ya Utalii toka mikoa mbalimbali wakisikiliza kwa makini yanayojiri kwenye   uzinduzi wa maandalizi wa maonesho ya kimataifa ya Utalii. Kanda ya Maziwa Makuu yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 19 hadi 21 mwaka huu.
Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua maandalizi ya maonesho ya utalii ya kimataifa na makubwa yatakayofanyika Mwanza mwezi june 2020, Maonesho yanaandaliwa na mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Tabora na Kigoma kwa lengo la kutangaza vivutio vilivyopo kwenye mikoa hiyo.
Hureeeee.........
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Mwenyeji wa maonesho ya Utalii Kimataifa 2020, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John V.K Mongella  akiteta jambo na kamati ya maandalizi kuelekea maonesho ya kimataifa ya Utalii Kanda ya Maziwa Makuu yanayotarajiwa kufanyika mkoani kwake kuanzia Juni 19 hadi 21 mwaka huu.

Wednesday, March 4, 2020

SHILINGI BILIONI 16 KUWANUFANISHA ZAIDI YA WANANCHI LAKI MOJA WA CHALINZE KATIKA MRADI WA MAJI

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kwanza akiwa katika  moja  eneo la eneo la chanzo cha maji ya  mto wami na kupokea maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Dawasa kuhusiana na mradi huo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimpa maelekezo moja ya waandisi ambao wanatekeleza mradi mkubwa wa bomba la maji ambalo linatokea katika mitambo ya ruvu juu kuelekea katika maeneo mbali mbali ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo  (PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja kulia akimpatia maelekezo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati alipotembelea moja ya mradi wa maji ambao utawanufainisha wawekezaji wa viwanda mbali mbali kikiwemo cha kuchakata nyama  katika eneo la Zegereni Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR ,MASANGU)
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kulia akifafanua jambo katika kiwanda cha kuchakata nyama kilichopo katika kata ya Kongowe wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maji .(PICHA NA VICTOR MASANGYU)
 Mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maji katika Mkoa wa Pwani ukiwemo ule wa kutokea katika mtambo wa ruvu juu kuelekea chalinze ambao utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilini 16.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Pichani ni moja ya baadhi ya mafundi wakiwa na  mtambo ambao unatumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kutoka mtambo wa ruvu juu kuelekea katika maeneo mbali mbali ya Chalinze  Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Rizone Kikwete akitoa ufafanua kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuhisiana na mwenendo wa ujenzi wa mradi wa maji ambao unateke lezwa na serikali kwa lengo la kuowaondolea changamoto  ya huduma ya maji wananchi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
VICTOR MASANGU, PWANI
ZAIDI ya wakazi laki moja wanaoishi katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao walikuwa na kilio kikubwa cha miaka mingi ya kukosa huduma ya maji safi na salama hatimaye wanatarajia kuondokana na kero hiyo sugu  ifikapo Juni mwaka huu  mara baada ya kukamilika kwa  mradi mkubwa kutoka  eneo la ruvu juu  hadi maeneo mbali mbali ya Chalinze ambao umegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 16.
Hayo yalibainishwa  na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua na kujionea miradi mbali mbali ya ujenzi wa maji katika Wilaya ya Kibaha pamoja na  mradi wa wami ambao upo katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo na kuagiza mamlaka husika kuhakikisha wanakamilisha  mradi huo kwa wakati ikiwemo sambamba na kufikishia huduma hiyo katika makazi ya wananchi pamoja na maendeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda.
Aidha Ndikilo amezitaka taasisi zote nchini kuhakikisha zinaachana na vitendo vya kuwa ni moja ya vigwazo katika  kuwacheleweshea vibali mbali mbali wawekezaji wa  wa viwanda wa ndani na nje na badala yake washirikiane nao bega kwa bega    katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Kwanza kabisa nimeamua kufanya ziara hii kwa lengo la kuweza kujonenea miradi mbali mbali ya maji katika maeneo ya Mkoa wetu wa Pwani na kwa upande wangu nimeweza kujionea jinsi ya mwenendo mzima, na kiukweli nishukuru sana mtendaji mkuu wa Dawasa pamoja sa safu yake yote kwa kuweza kufanya kazi ambayo inatia moyo ya kutekeleza kwa vitendo miradi ya usambazaji wa maji katika maeneo ya viwandani pamoja na kwa wananchi wenyewe hii ni hatua kubwa sana katika Mkoa wetu,”alisema Ndikilo.
Pia alibainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbali mbali ya maji katika Mkoa wa Pwani kutaweza kuwavutia wawekezaji wa viwanda kuwekeza katika miradi mbali mbali sambamba na kuweza kutoa fursa za ajira kwa vijana hivyo amewaomba wamiliki wa viwanda hivyo kuhakikisha wanawapa kipaumbele zaidi wazawa katika suala zima la upatikanaji wa ajira lengo ikiwani ni kujiongezea kipato na kuondokana na wimbi la umasikini.   
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja  baada ya kutembelea baadhi ya miradi  ambayo ipo kwenye mpango wa kupatiwa maji ikiwemo viwanda  amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba  wanatekeleza kwa vitendo azma ya kumuunga Mkono Rais wa awamu ya tano katika kuwa na uchumi wa viwanda pamoja na kuwaondolea kero wananchi ambayo wamekuwa wakiipata kwa kipindi kirefu kwa  kuwasambazia huduma ya maji safi na salama.
Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa latika jitihada za kuboresha huduma  ya maji katika maeneo mbali mbali Dawasa iliingia mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba kuu la kusafirisha maji lenye uumbaro wa kilometa 59 kutoka katika mitambo ya ruvu juu hadi katika kijiji cha Mboga kilichopo katika halmashauri ya Chalinze na utekelezaji wake unaendelea vizuri.
“Ujazo huu wa mradi mkubwa wa kutoka mlandizi hadi chalinze unatarajiwa pindi utakapomalizika utasafirisha kiasi cha lita za ujazo milioni tisa na laki tatu kwa siku moja ambazo zitaweza kuwahudumia wakazi wapatao laki moja na ishirini sambamba na maunganisho mapya ya wateja zaidi ya elfu 18 ambao wataweza kunufaika na mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chailzinze  Chalinze Rizone  Kikwete alisema   kwamba wananchi wake kwa kipindi cha miaka mingi wamekuwa na adha kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama hivyo kukamilika kwa mradi huo utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa   katika maeneo mbali mbali ambayo yalikuwa yanakabiliwa na  changamoto sugu ya kutembea umbari mrefu kwenda kutafuta maji katika maeneo mengine ya mbali.
 “Hapo awali wananchi wangu wa chalinze walikuwa wana kero kubwa sana ya kipindi kirefu kutokana na ukosefu wa huduma ya maji, maana walikuwa wanatembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta maji lakini napenda kumshukuru sa Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kutoa kiasi hiki cha fedha ambacho kitasaidia kuleta neema kwa wananchi hawa kwani kwa sasa wao wenyewe wanajionea jinsi ya utekelezaji wa mradi huu na maswali yamepungua kabisa kila kona, alisema Rizone.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani yupo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika baadhi ya Wilaya kwa lengo la kugagua na kujionea shughuli mbali mbali zinazotekelezwa katika miradi  mbali mbali ya maji ambayo imelengwa kuwafikia wananchi pamoja na maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na mambo mengine.                       

Tuesday, March 3, 2020

ASKARI ZIMAMOTO KIWANJA CHA NDEGE DODOMA KUJENGEWA UWEZO KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA

 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi, akizungumza na Maafisa na Akari wa Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Maafisa na Akari wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Meneja wa Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma Bertha Bankwa (wapili kulia), akimshukuru Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu kulia), Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo ambaye ni Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya Ndege nchini (ACF) Bakari Mrisho (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo (ACF) Christom Manyologa (kulia) kwa kuona haja ya kuandaa mafunzo hayo kwani yataongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa Maafisa na Askari hao. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Sehemu ya Maafisa na Akari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Ukuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. 
 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu kulia waliokaa), Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji ambaye ni Mkuu wa Zimamoto Viwanja vya Ndege nchini (ACF) Bakari Mrisho (watatu kushoto waliokaa), Meneja Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma Bertha Bankwa (wapili kulia waliokaa), Kamishna Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo (ACF) Christom Manyologa (kushoto), Mratibu wa mafunzo Uwanja wa Ndege Dodoma Swalha Soka (wapili kushoto waliokaa), Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Uwanja wa Ndege Dodoma Liberatus Monella (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo, baada ya Kamanda wa Mkoa wa Dodoma wa Jeshi hilo, kufungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Maafisa na Akari wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.

Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Aidha imeelezwa kuwa mafunzo hayo yataendelea kwa siku tano mfululizo, na zaidi ya Maafisa na Askari 30 watanufaika na mafunzo hayo pia yataendelea kwa Mikoa mingine kote nchini.

Taarifa ya Jeshi hilo imeeleza kuwa dhumuni la mafunzo hayo kuhakikisha Maafisa na Askari wote wanaohuduma Viwanja vya Ndege kote nchini wanapatiwa mafunzo ya aina hiyo kwa awamu hasa katika kipindi hiki tunapoelekea Tanzania ya Uchumi wa kati unaotegemea Viwanda.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PROFESA LIPUMBA PAMOJA NA JAMES MBATIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Picha na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWANASIASA MKONGWE MAALIM SEIF SHARIF HAMAD IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokugusana mikono, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Salamu hiyo ya kutokugusana mikono ni kutekeleza ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAFUNGWA 150 WAPELEKWA KWITANGA KULIMA MCHIKICHI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) na Mkuu wa Gereza Kwitanga, Mrakibu Mwandamizi, Dominick Kazmil wakiangalia matunda ya mchikichi yaliyovunwa katika gereza hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma  kuwa Kituo Kikuu cha  Uzalishaji wa zao la  Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu mstari wa mbele) akimsikiliza  Mkuu wa Gereza Kwitanga, Mrakibu Mwandamizi, Dominick   Kazmil baada ya kuangalia miche ya michikichi iliyooteshwa  katika gereza hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma  kuwa Kituo Kikuu cha  Uzalishaji wa zao la  Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo.Wengine ni ujumbe uliofuatana na Naibu Waziri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Matunda ya Mchikichi yaliyovunwa katika mashamba ya Gereza Kitwanga yakiwa yameanikwa juani tayari kwa kukamuliwa mafuta ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza hilo  lililopo wilayani Kigoma  kuwa Kituo Kikuu cha  Uzalishaji wa zao la  Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia mpango kazi wa kilimo cha mchikichi katika Gereza la Kwitanga ikiwa ni ufuatiliaji wa  utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza hilo  lililopo wilayani Kigoma  kuwa Kituo Kikuu cha  Uzalishaji wa zao la  Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo,Kushoto ni Mkuu wa Gereza  Mrakibu Mwandamizi, Dominick Kazmil na Kulia ni Mkuu wa Magereza Kigoma Kamishna Msaidizi Leonard Bushiri. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu,Kigoma

Wafungwa 150 kutoka katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora wamepelekwa katika Gereza la Kwitanga Mkoani Kigoma ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali kuliteua gereza hilo kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa zao la  mchikichi nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mkakati huo uliotolewa maagizo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katikati ya mwaka 2018 alipofanya ziara gerezani hapo  ukiwa na lengo la kulifanya Jeshi la Magereza kuingia katika mfumo wa uzalishaji mali.

“Katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambalo ni agizo la serikali, wizara tumeongeza nguvukazi hapa kwa kuleta wafungwa 150 na muda si mrefu tutaongeza wafungwa wengine 300 kutoka magereza mbalimbali nchini ili kuweza kuongeza uzalishaji huku eneo lenye ukubwa wa ekari 6000 linatarajiwa kulimwa zao hilo sambamba na kusambaza mbegu zinazozalishwa gerezani hapo kwenda Halmashauri za Mikoa, Taasisi za Umma, Asasi za Kiraia na Sekta Binafsi,” alisema Masauni

“Lakini pia ili kuliwezesha gereza hili tumeliagiza Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza kulichukua Gereza la Kwitanga na kuliingiza katika kundi la magereza yanayowezeshwa na shirika ili kuweza kutatuliwa matatizo yao ya kifedha badala ya kusubiri bajeti kuu kutoka serikalini ambayo inakua haitoshi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Magereza mkoani Kigoma, Kamishna Msaidizi Leonard Bushiri aliunga mkono hoja ya Gereza Kwitanga kuchukuliwa na Shirika la Uzalishaji Mali huku akikiri baadhi ya masuala kukwama kutokana na changamoto za kibajeti.

“Nafikiri hili suala la gereza kuchukuliwa na Shirika la Uzalishaji Mali litatatua changamoto nyingi za kibajeti na kiuendeshaji maana gereza halina gari kubwa kwa ajili ya uvunajina usafirishaji wa mafuta kutoka gerezani kwenda kwa mtumiaji, hakuna bajeti ya uendeshaji kwa mfano kukamua lita 100 mpaka 120 za mafuta tunahitaji maji lita 1000 hivyo fedha kwa ajili ya kununulia umeme ili kusukuma maji ni changamoto, kwahiyo kuingizwa kwenye shirika itasaidia changamoto nyingi” alisema ACP Bushiri

Sambamba na kulima zao la mchikichi Gereza Kwitanga linalima pia mahindi, mpunga, mihogo, maharage na Bustani za mbogamboga.