ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 7, 2020

DARAJA LINALOUNGANISHA MWANZA NA MUSOMA KUFUNGWA USIKU KWA MUDA WA SIKU 10 KUPISHA UKARABATI.


DARAJA la Simiyu lililopo wilayani Magu barabara kuu ya Mwanza - Musoma litalazimika kufungwa kwa muda kupisha matengenezo makubwa ya kuboresha kwa daraja hilo. Hayo yamesemwa leo Tarehe 6/March/2020 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa darajani hapo akirea jijini Mwanza akitokea mkoani Simiyu kumsindikiza Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu aliyewasili kwaajili ziara ya siku 3 kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo amnbapo anatarajia kuhitimisha ziara yake tarehe 8/03/2020 katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Akiwasilisha taarifa ya ufungwaji wa daraja hilo Meneja  wa Tanroads Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa M. Rubirya alisema watafunga barabara ya Mwanza- Musoma kuanzia Machi 8 hadi 18 mwaka huu ili kupisha matengenezo makubwa ya daraja hilo.
Mhandisi Rubirya ameongeza kuwa wameamua kufanya matengenezo ya haraka ili kujiepusha na hatari zitakazoweza kujitokeza kwa sababu kuchelewa kwa ujenzi huo yaweza kuwa hatarishi kwa watumiaji wa barabara hiyo .
Aliongeza kuwa barabara hiyo itafungwa ili kupisha matengenezo kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11 asubuhi  pia aliomba ushirikiano wa Jeshi la polisi katika kutekeleza kazi hiyo.
Alisema Serikali inampango wa kujenga daraja jipya hivyo hatua zinazofanyika sasa  ni za muda mfupi, aliwataka wananchi kuwa wavumilivu waweze kuboreshewa njia itakayowanufaisha na kuendeleza ujenzi wa taifa.
" Hali halisi ilivyo na nyie mmeiona ninachowaomba muwe wavumilivu ujenzi ufanyike ili kuepusha madhara makubwa ya baadaye" alisema Mhe.Mongella.
Lusia Isack ni mmoja wa wakazi wa Magu akizungumzia adha hiyo alisema wanakuwa wa hofu kila wanapopita kwenye daraja hilo hasa wanapofika katikati hivyo wanaishukuru Serikali kwa kuliona hilo kwani wameweza kutatua changamoto hiyo kabla haijaleta maafa.
"Hili daraja ni bovu sana  ata ukiwa umebebwa kwenye baiskel ukifika katikati daraja linaanza kucheza sasa ukiwa kwenye gari unawaza sijui nitapita salama kwa sababu likidondoka tu sizani kama kuna mtu atakayepona kinachobaki ni kuomba Mungu wakitutengenezea watakuwa wametusaidia sana." alisema Isack.

Hata hivyo daraja hili lililojengwa mwaka 1962 limeanza kuonyesha nyufa baada ya vyuma vilivyokuwa vinalishikilia kukatika jambo hilo limejenga hofu kwa Serikali na watumiaji wa njia hiyo harakati za haraka zinafanyika ili kubadilisha vyuma hivyo .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.