ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 20, 2015

"NAFASI HII NILIYOIOMBA SI KWAAJILI YA KUPAMBANA NA MTU, BALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA WATANZANIA" ASEMA JANUARY MAKAMBA

"Nafasi hii niliyoiomba si kwaajili ya kupambana na mtu, bali kupambana na changamoto za jamii ya Watanzania"ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI NA KURUKA LIVE KUPITIA JEMBE FM 93.7 MWANZA.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATOA DOLA ZA MAREKANI 150,000 KWA HOSPITALI YA CCBRT KUSAIDIA WATOTO WENYE MIGUU ILIYOPINDA

Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kusisaidia Hospitali hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans na Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja  Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT baada ya kutiliana saini mkataba wa kusaidi matibabu ya ulemavu wa miguu Dar es Salaam jana. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute na Meneja Uwajibikaji kwa Jamii, Woinde Shisael.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Picha mbalimbali zikionesha miguu iliyopinda.
Wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Joyce Moshi akiwa amembeba mtoto wake Gedion ambaye anatibiwa katika Hospitali hiyo kutokana na miguu yake kupinda ambapo sasa anaendelea vizuri.

Na Dotto Mwaibale
HOSPITALI ya CCBRT, imepokea dola 150,000 (zaidi ya sh. mil. 320) kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa ajili ya kugharamia matibabu ya watototo wanaozaliwa na ulemavu wa nyayo zilizopinda kwa miaka mitatu ijayo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema hiyo si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kugharamia matibabu ya walewavu kwani miaka mitatu iliyopita pia waligharamia matibabu ya watoto wenye ulemavu wa midomo.

"Tuna amini watoto wenye ulemavu wa unyayo uliopinda watapatiwa matibabu mapema, hivyo tunaomba wazazi wenye watoto wao wanaozaliwa na ulemavu huo kujitokeza CCBRT kupatiwa matibabu kwani ni bure na kwa mwaka tunatoa dola 500," alisema Gutierrez.

Kwa upande wa Daktari wa Mifupa wa hospitali hiyo, Prosper Alute akizungumzia ugonjwa huo, alisema unasababishwa na kurithi kutoka kwa wazazi au ndugu na kunywa pombe kupindukia au kutumia dawa zenye viambata kali.

Alisema asilimia 50 ya watoto wanaozaliwa hupata ugonjwa huo kwa miguu yote ambapo tangu kuingia kwa mwaka huu hadi Aprili, watoto 117 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo ambao ni sawa na wastani wa watoto 10 kwa wiki.

Alisema ugonjwa huo usipotibiwa kwa haraka unaweza kumsababishia mtoto kutembea kwa shida na wakati mwingine kutotembea kabisa.

Kwa upande wa Joyce Mosha, Mkazi wa Mwenge,  ni mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake, Gidion ana miezi miwili alikutwa na tatizo hilo na kufanyiwa upasuaji, alisema mara baada ya kujifungua madaktari waligundua mtoto wake kuwa na tatizo hilo, hivyo waliamua aanze kupatiwa matibabu.

"Namshukuru Mungu alifanyiwa upasuaji mdogo na hivi sasa anaendelea vizuri, alipogunduliwa ana tatizo hilo kwanza walimfunga plasta ngumu (POP) kwa wiki tano na kisha kumfanyia upasuaji mdogo wa mfupa na kumpa viatu maalumu vya kuvaa na vingine huwa anavaa usiku tu wakati wa kulala," alitoa ushuhuda Joyce. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712727062)

KIPINDI KIPYA ' NYUMBANI NA DIASPORA'

Nyumbani na Diaspora!


Ni kipindi kipya cha saa nzima chenye kuhusiana na Watanzania wa nyumbani na walio nje ya mipaka yetu. Ni kipindi daraja kitakachowaunganisha Watanzania katika kubaini fursa mbalimbali za kuinuka kimaendeleo, kwa mtu mmoja mmoja, jumuiya na hatimaye taifa.

Ni kipindi kitakachoongozwa na mchambuzi na mmoja wa wanahabari nguli hapa nchini. 

Si mwingine ni Maggid Mjengwa. Jiunge nae kufuatilia mahojiano motomoto na watu wa kada mbalimbali kwenye masuala ya  kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ni kila siku ya Ijumaa saa 4 usiku na marudio Jumapili saa kumi jioni, hapa hapa TBC 1, ukweli na uhakika!

Friday, June 19, 2015

KILIMANJARO YAVUNJA REKODI YA UDHAMINI KWA MH. LOWASSA, WANACCM 33,780 WAMDHAMINI

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI


Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.

Umati wa wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, ukimshangilia kwa furaha, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipopanda jukwaani kuwashukuru wa kumdhamini kwa kishindo. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.

Sehemu ya WanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamefurika katika eneo la uwanja wa Ofisi ya CCM Mkoa huo wakifatilia kwa majini maelezo ya Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata leo Juni 18, 2015.
Mh. Lowassa akisomewa Dua na Sheikh wa mji wa Moshi mara baada ya kupewa udhamini wa Kishindo katika Safari yake ya Matumaini.

Mchungaji akitoa maombi.




Wadau wakipata taswira ya Mh. Lowassa wakati akiondoka kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro.

Vijana wa CCM wa Mji wa Muheza wakiuongoza Msafara wa Mh. Lowassa kwenye eneo hilo la Muheza kwa lengo la kuzumza nao.
Vijana wa CCM Mji wa Muheza wakimshangilia Mh. Lowassa wakati walipomzimamisha ili aongee nao, alipokuwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
Ujumbe wa Vijana wa Muheza.
Ni furaha tupu.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Muheza sambamba na kuwatakia Heri ya Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini watakamuwezesha kupata ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 18, 2015.
Baada ya kuwasalimia wanaCCM wa Mji wa Muheza, Mh. Lowassa alipata wasaa wa kwenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajab, Marehemu Mzee Rajab nyumbani kwao Muheza, Mkoani Tanga. anaezungumza na Mh. Lowassa ni Mama Mzazi wa Mh. Adadi Rajab, Bi. Fatuma Omar.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (katikati) pamoja na wananchi wa Korogwe wakiwa wamefunga barabara kuuzuia msafara wa Mh. Lowassa ili aweze kuzungumza nao, huku wakimuuga mkono katika safari ya Matumaini.
Mh. Lowassa alishuka garini na kuungana na wananchi hao.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Korogwe wakati akiwa safarini kuenekea Mkoani Kilimanjaro.
Shangwe tupu kwa wananchi wa Korogwe.
Kwaherini wana Korogwe.

Alipofika Mombo
Mh. Lowassa akikata nyama ya mbuzi katika moja ya Majiko eneo hilo la Mombo.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" akitoa neno.
Mh. Lowassa akitoa neno la shukrani kwa wakazi wa Mombo.
Mh. Lowassa akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa mji wa Hedaru.
Same.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonard Minja wakati alipofika kumpongeza kwa udhamini anaoendele kuupata.