NA. VICTOR MASANGU,PWANI
Thursday, September 14, 2023
TRA PWANI YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA KUTUMIA MASHINE ZA EFD
Wednesday, September 13, 2023
Rais Mwinyi aipongeza Benki ya CRDB kwa huduma za kibenki zinazozingatia msingi ya Kiislamu
Unguja. Tarehe 10 Septemba 2023: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma za kibenki zinazofuata misingi ya sharia hivyo kuwahamasisha Waislamu wengi kutumia huduma zake jambo linalochochea ujumuishi wa kifedha.
Rais Mwinyi ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akaunti ya Al Barakah mwishoni mwa mwaka 2021 huduma hiyo ilipozinduliwa, ametoa pongezi hizo alipokabidhiwa kadi ya akaunti hiyo mwishoni mwa wiki alipotembelewa na ujumbe wa Benki ya CRDB ikulu mjini Zanzibar.
“Tulijua Al Barakah itakuwa na mafanikio lakini hatukutarajia kuwa yangepatikana ndani ya muda mfupi namna hii. Nawapongeza kwa mafanikio mliyoyapata na niwaahidi kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano na benki yenu kuhakikisha huduma hizi zinawafikia Waislamu wengi walipo visiwani humu ili kwa Pamoja tushiriki kulijenga Taifa letu huku tukimwabudu Mwenyezi Mungu bila kukiuka maagizo yake,” amesema Dkt Mwinyi.
Rais Mwinyi pia ameishukuru Benki ya CRDB kwa heshima iliyompa ya kuwa mteja wa kwanza kukabidhiwa kadi ya Akaunti ya Al Barakah na akasema jambo hilo limemhamasisha zaidi hivyo ataangalia namna ya kuongeza amana kwenye akaunti yake ili kufurahia huduma hizo zinazokidhi mahitaji yake ya kifedha na imani ya kiroho.
Akimkabidhi kadi ya Al Barakah, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB inayojumuisha Zanzibar na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Badru Idd amesema Rais Mwinyi sio tu alihamasisha kuanzishwa kwa huduma hizo bali alionyesha mfano kwa kuwa wa kwanza kufungua akaunti hiyo mwaka 2021 ambayo mpaka sasa ina wateja zaidi ya 70,000 nchini kote.
“Mpaka sasa hivi, tumekopesha zaidi ya shilingi bilioni 90 kwa misingi ya sharia na tumepokea amana za wateja zaidi ya shilingi 85 bilioni ndani ya miaka miwili ya kutoa huduma hizi. Huduma za CRDB Al Barakah Banking zinaendelea kutoa mchango mkubwa sana katika serikali yako ya Zanzibar na wananchi wake kwani tumekopesha zaidi ya shilingi 18 bilioni kwenye uchumi wa buluu na wafanyabiashara wamepata Zaidi ya shilingi bilioni 33,” amesema Idd.
Ili kusogeza huduma kwa wananchi visiwani humu, Benki ya CRDB ilifungua tawi mjini Wete lililozinduliwa na Rais Mwinyi mwaka 2021 alikoiomba benki kuanzisha huduma zenye misingi ya sharia na mpaka sasa, kwenye matawi manne ya Benki ya CRDB yaliyomo Zanzibar, wananchi wameweka amana za zaidi ya shilingi bilioni 28.
Kuhusu kadi za Akaunti ya Al Barakah, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Zinazofuata Sharia (Islamic Bankink) wa Benki ya CRDB, Rashid Rashid amesema zipo za aina nne na zote zinaweza kutumika katika majukwaa yote ikiwamo kwa mawakala zaidi ya 200 waliopo Zanzibar kama ilivyo kwa kadi zinazotumiwa na wateja wengine wote wa Benki ya CRDB.
“Pamoja na mafanikio haya makubwa, CRDB Al Barakah Banking tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwafikia wateja wetu na kuwapa amani wanayoitegemea kwa kuweka pesa zao katika akaunti za Al Barakah zinazofuatisha misingi ya sharia. Kila mteja mwenye akaunti hii, ana amani kwa kujua kwamba pesa zake ziko mahala salama na zina uangalizi maalum unaoendana na imani na maadili yake,” amesema Rashid.
Akizungumzia umuhimu wa huduma za fedha kwa maendeleo ya Taifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Fedha Zinazofuata Misingi ya Sharia ya Benki ya CRDB, Abdul van Mohammed amesema kuna fursa nyingi ambazo Zanzibar inaweza kunufaika nazo iwapo itafungua milango.
“Zanzibar ndio yenye matumizi makubwa ya Islamic Banking Afrika Mashariki. Naomba Serikali iangalie uwezekano wa kuifanya kuwa ya kwanza kuuza hatifungani ya Kiislam ili kupata fedha zitakazochangia maendeleo ya watu wetu,” amesema Mohammed.
TPA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT SAMIA KWA KUTOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA YA KOROGWE
MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo , Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
Alisema wao wametoa kwa jamii walichokipata mwaka huu na wameamua kupeleka msaada huo kwenye Hospitali hiyo ili kuweza kuwasaidia kuwapunguzia baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwenye Hospitali ya Korogwe.
“Licha ya kutoa msaada huu hapa lakini tutaendelea kusaidia kitakachpatikana ili kuweza kutatua changamoto kwenye hospitali ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na vikwazo mbalimbali katika kupata huduma za matibabu”Alisema
Awali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo aliishukuru Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa msaada huo mkubwa ambao wamewapatia kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Korogwe ambao ni vitindi mwendo ambavyo uhitaji wake ulikuwepo.
Alisema pia msaada huo mashine ya ECG kwa ajili ya matibabu ya moyo utawasaidia wananchi katika wilaya hiyo kutokana na idadi ya watu wenye matatizo ya moyo inaongezeka vijijini kutokana na matumizi ya chumvi kuongezeka.
Alisema pia matumizi ya mafuta vinachangia pia na mtindo wa maisha huku akieleza kifaa hicho kitakwenda kuwatibu wananchi na hivyo kuwasaidia kuwa na afya bora kutokana na kwamba Taifa lenye nguvu lazima wananchi wake wawe na afya bila afya hawaweze kufanya kazi na kuweza kushiriki shughuli za kijamii ili kuweza kukuza uchumi.
Naye kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Korogwe Miriam Cheche aliishukuru TPA kwa kugawawia msaada wa vifaa hivyo ikiwemo kifaa cha kisasa ambacho kinagundua matatizo ya moyo kwa mtu anayeugua kabla ya kupelekwa kwenye Hospitali za Rufaa.
“Kwa kweli tunawashukuru sana TPA kwa msaada huu kwa sababu wananchi watafaidika na mashine hii lakini tunamshukuru DC kwa hamasa zake na hivyo kupelekea wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia pia Rais Dkt Samia Suluhu kuendelea kutupatia fedha kuendeleza hospitali yetu ya wilaya hapa Makuyuni”Alisema
MBUNGE KOKA AFANYA KWELI ATEKELEZA AHADI ZAKE SOKO LA MNARANI.
Na Victor Masangu,Kibaha
TRA PWANI YAZINDUA KAMPENI YA KUWANOA WAFANYABISHARA JUU YA UMUHIMU WA KODI
Na Victor Masangu,Pwani
WATATU KUPAMBANA LEO HATUA YA ROBO FAINALI
MABONDIA WATATU WA TANZANIA LEO WATINGA ROBO FAINALI YA MASHINDANO KUFUZU KUSHIRIKI OLIMPIKI.
Watanzania watatu leo kuanzia saa kumi na moja jioni kwa saa za Senegal, watapanda ulingoni kutafuta tiketi ya kuingia nusu fainali katika mashindano ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki 2024 Paris Ufaransa yanayoendelea Dakar Senegal. Mabondia hao ni, katika uzito wa 66Kg. wanawake Grace Mwakamele (Tanzania) atapambana na Khelif Imane (Algeria), katika uzito wa 51Kg.
Abdallah Mohamed (Tanzania) atacheza na Mortaji Said (MOROCCO) na katika uzito wa 80Kg. Yusuf Changalawe atacheza na Seydna Konate (Senegal)
Mabondia waliofuzu kufika hatua hiyo jumla yao ni 104 kutoka katika mataifa 26 ya AFRIKA.
Jumla ya mabondia walioshiriki mashindano hayo ni 235 kutoka katika mataifa 41 ya Afrika.
Mabondia wengine wa Tanzania walishindwa katika hatua za awali ni 50Kg. Zulfa Macho, 57Kg. Mwalami Salum na 92 Kg. Mussa Maregesi.
Viongozi waliombatana na timu ni Lukello Wililo (Raisi na Mkuu wa Msafara),Makore Mashaga (katibu na kocha msaidizi), Samwel Batman (Kocha mkuu) na Aisha George (Matron) Fainali za mashindano hayo zitafanyika ijumaa ya tarehe 15.09.2023.
Timu itarejea nyumbani Jumapili ya tarehe 17.09.23 saa tisa Alfajiri.
Naambatanisha na ratiba ya leo.