MABONDIA WATATU WA TANZANIA LEO WATINGA ROBO FAINALI YA MASHINDANO KUFUZU KUSHIRIKI OLIMPIKI.
Watanzania watatu leo kuanzia saa kumi na moja jioni kwa saa za Senegal, watapanda ulingoni kutafuta tiketi ya kuingia nusu fainali katika mashindano ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki 2024 Paris Ufaransa yanayoendelea Dakar Senegal. Mabondia hao ni, katika uzito wa 66Kg. wanawake Grace Mwakamele (Tanzania) atapambana na Khelif Imane (Algeria), katika uzito wa 51Kg.
Abdallah Mohamed (Tanzania) atacheza na Mortaji Said (MOROCCO) na katika uzito wa 80Kg. Yusuf Changalawe atacheza na Seydna Konate (Senegal)
Mabondia waliofuzu kufika hatua hiyo jumla yao ni 104 kutoka katika mataifa 26 ya AFRIKA.
Jumla ya mabondia walioshiriki mashindano hayo ni 235 kutoka katika mataifa 41 ya Afrika.
Mabondia wengine wa Tanzania walishindwa katika hatua za awali ni 50Kg. Zulfa Macho, 57Kg. Mwalami Salum na 92 Kg. Mussa Maregesi.
Viongozi waliombatana na timu ni Lukello Wililo (Raisi na Mkuu wa Msafara),Makore Mashaga (katibu na kocha msaidizi), Samwel Batman (Kocha mkuu) na Aisha George (Matron) Fainali za mashindano hayo zitafanyika ijumaa ya tarehe 15.09.2023.
Timu itarejea nyumbani Jumapili ya tarehe 17.09.23 saa tisa Alfajiri.
Naambatanisha na ratiba ya leo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.