ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 23, 2011

TAMASHA LA PASAKA LASUBIRIWA KWA HAMU KUHITIMISHWA MWANZA JUMANNE YA PASAKA

MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha kubwa la Pasaka, Alex Msama amesema kwamba maandalizi yote yamekamilika na ikiwa sambamba na waimbaji kutoka nchi mbalimbali kuwasilini nchini.Msama ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, amesema kwamba wanamuziki hao tayari wamekwisha wasili nchini kwa ajili ya tamasha hilo ambalo la kwanza litafanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es Salaam pia litafanyika mjini Dododma Aprili 25 na baadaye Mwanza Aprili 26 na wakati huo huo, kwaya ya Kinondoni Revival Choir imethibitisha kushiriki kwenye Tamasha hilo la Pasaka ikunganana na waimbaji wengine.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu linawashikisha waambiji wote nyota wa muziki wa Injili wanaotamba nchini na pia wengine kutoka nyingine barani Afrika. Waaimbaji watakaoshiriki kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Rose Mhando, Boniface Mwaitege, Christina Shusho, Updeno Nkone, Faraja Ntatoba kutoka nchini DR Congo, Ephraime sekeleti kutoka Zambia na Anastazia Mukabwa kutoka Kenya.
Wengine ni Solomon Mukubwa, Geraldine Odour na Pamela Wandela wote kutoka nchini Kenya.


Pia katika kilele cha Tamasha hilo ndani ya jiji la Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar itazinduliwa albamu mpya ya muziki wa Injili ya Haleluya Collections Vol 5. Albamu hiyo imeandaliwa na kusambazwa na Msama Promotions na malengo yake ni kusaidia watoto yatima na misaada kwa wanawake wajane.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.

Friday, April 22, 2011

TUNAWATAKIA IJUMAA KUU NJEMA

Leo ni Ijumaa Kuu, siku ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili yetu.Na haya ndiyo maandalizi: Mbuzi aliyenona kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

WAKITOKA KANISANI LEO IBADA YA IJUMAA KUU.
Sio kwenda kanisani au kuimba mapambio tu kwamba ndiko kutakompatia mwanadamu uzima wa milele bali matendo. Japo ni muhimu kujumuika na waumimni wenzetu makanisani,la muhimu zaidi ni kuishi kwa mfano wa Bwana Yesu ambaye licha ya upendo wake usiomithilika alikuwa tayari kufa msalabani kwa dhambi zetu ili atuletee ukombozi.

Wakati tovuti hii inakutakia wewe msomaji mpenda Ijumaa Kuu njema,siku hii inaweza kuadhimishwa ipasavyo kwa kutafakari kuhusu upendo wa Bwana,kujitoa kwake kwa ajili yetu na upendo kwa ujumla. Kama humpendi jirani yako unayemwona kila siku utakuwa mnafiki kudai unampenda Bwana mbaye hujawahi kumwona. Yesu ni upendo na amani.

"NAWATAKIA IJUMAA KUU NJEMA"
@G.Sengo

SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MAANDALIZI YAMEKAMILIKA MWANZA USHINDWE MWENYEWE.

Katika kuelekea siku husika ya bonanza la Serengeti soka ndani ya jiji la Mwanza leo majira ya asubuhi viongozi wa timu zote nane walifika katika studio za clouds fm Mwanza kwania ya kutangaza usajili wa timu zao sambamba na mikakati waliyoiweka kuibuka washindi kwa michuano hiyo.Pichani ni rais wa Arsenal Mwanza Bw. Arsenal Class akifanya mahojiano na mtangazaji mahiri wa kipindi cha Sports Extra cha Clouds fm, Alex Luambano.

Sambamba na soka kesho mapema subuhi kutakuwa na usaili kuibua wasanii wa filamu na watunzi wa filamu Mwanza, utakao fanyika katika hoteli ya kisasa Isamilo Lodge pichani ni mwigizaji maarufu nchini Jackline Wilper akifafanua jambo kuhusu mchakato mzima.

Rais wa Man U' Mwanza, Fransis Sissamo aka Papaa' amesema timu yake imejipanga kwa ushindi tu! kwani wamejifunza mengi kwa ndugu zao wa Dar es salaam nahawako tayari kurejea makosa.

Mratibu wa usaili Filamu Zamaradi Mketema amewataka washiriki wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi hiyo kesho jumamosi kwaajili ya kuzinyakuwa Golden Chance zilizopo nikimaanisha kupata dil kuigiza filamu sambamba na mastaa wakubwa.

"Wote wenye vipaji vya kuigiza fikeni Isamilo Lodge kwani hii ni Golden Moment kwani najua ni ndoto ya wengi kwamba siku moja ulitamani kuigiza na kuwa mwigizaji mkubwa basi wakati wa ndoto yako kutimia ndiyo huu" says Hemed.

Timu ya Sports Extra imekamilika kwaajili ya kuripoti matukio yote yatakayojiri ndani ya bonanza la klabu za mashabiki hapa ni Abdul Mohamed akizungumza naye Alex Luambano mbele ya marais wa mashabiki Mwanza ndani ya studio za Clouds 88.1

Hemed, Wolper, G.Sengo na Zamaradi.

Aaaaah Mwanzaaaaa!!

Thursday, April 21, 2011

WALIOTAKA 'KUMUUA' DK. CHEGENI KIZIMBANI

Watuhumiwa wa mtandao wa kula njama kutaka kumuua kwa risasi aliyekuwa mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega, wilayani Magu, mkoani Mwanza, Dk. Raphael Masunga Chegeni, wamefikishwa mahakamani kisha kusomewa mashitaka yanayowakabili.WATUHUMIWA WAKIINGIA KIZIMBANI.
Watuhumiwa hao kwa pamoja walipandishwa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, mbele ya Hakimu Angerus Lumisha, wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 113/2011, ambapo wakiwa katika chumba cha mahakama mawakili wao walianza kujibizana na hakimu kwa kutumia lugha ya Kiingereza kwa takriban dakika 15 hivi.

Katika kesi hiyo ya mauaji, Dismas Zacharia Kamani ni mtuhumiwa namba moja wa kesi hiyo ya mauaji, Erasto Casmil ni mtuhumiwa namba mbili, Queen Joseph Bogohe ni mtuhumiwa namba tatu na Ellen Bogohe, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa ya CCM mkoani Mwanza na diwani wa zamani wa viti maalumu Kata ya Kisesa wilayani Magu, mkoani hapa, ni mtuhumiwa namba nne wa kesi hiyo ya jinai.

Ilielezwa mbele ya mahakama kwamba, Aprili 13 mwaka huu, kwa pamoja watuhumiwa hao walikula njama za kutaka kumuua Dk. Chegeni. ALIYE PICHANI KULIA-->

Paschary Malungu ndiye mwanasheria wa upande wa mlalamikaji (Jamhuri), wa kesi hiyo, huku watuhumiwa Ellen Bogohe na Queen Joseph Bogohe wakitetewa na wanasheria wao wawili wa kujitegemea, Mathew Nkanda na Raurian Vedasto.

Mbele ya mahakama ilidaiwa kwamba watuhumiwa wote kwa pamoja walikula njama kutaka kuua kinyume cha kifungu cha sheria namba 215 ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


MJUMBE KAMATI YA SIASA CCM ALIYETANGULIA NA QUEEN.
Watuhumiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 6 mchana, walipandishwa kizimbani majira ya saa 9:25 alasiri, na wakiwa kizimbani, yalitokea majibizano kati ya hakimu na mwanasheria mmoja ambapo majibizano hayo yalifanyika kwa Kiingereza kuhusiana na mwenendo wa sheria za nchi, hasa zile za mauaji (jinai).

Baada ya majibizano hayo, Hakimu Malungu alimhoji mtuhumiwa mmoja baada ya mwingine akianzia kwa mtuhumiwa namba nne, Ellen Bogohe, Queen Joseph Bogohe, Erasto Casmil na Dismas Zacharia Kamani, iwapo wanataka kesi yao iendeshwe kwa Kiingereza ama Kiswahili, lakini watuhumiwa wote kwa pamoja walisema iendeshwe kwa Kiswahili.

Upande wa utetezi uliiomba mahakama hiyo kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao kwa madai kuwa hawawezi kuharibu upelelezi unaoendelea na kwamba bado haijafahamika iwapo kesi ya wateja wao itasikilizwa na Mahakama Kuu ama la, lakini hakimu alitupilia mbali ombi hilo. Badala yake aliamuru watuhumiwa kurudishwa rumande hadi leo saa 5 asubuhi mahakama itakapoamua kesi hiyo isikilizwe na mahakama ipi.

Wednesday, April 20, 2011

SHERIA NA KANUNI ZA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MWANZA ZAWEKWA HADHARANI.

Leo majira ya saa tano asubuhi viongozi wa timu za mashabiki wa soka la ulaya kwa timu za Real Madrid, Arsenal, Man U, Liverpool, Inter Milan, Ac Milan, Chelsea na Barcelona wamekutana na kamati ya maandalizi ya bonanza hilo kwa nia ya kupeana kanuni na taratibu mbalimbali juu ya uchezeshwaji wa ligi hiyo.

Ligi ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza inatarajiwa kufanyika jumamosi hii ya tarehe 23 April 2011 katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza kuanzia saa 4 asubuhi na kuendelea hatimaye kumpata bingwa.

Akizungumza mbele ya Marais wa timu hizo za Mashabiki mratibu mkuu wa Bonanza hilo Shafi Dauda amesema kuwa kanuni zitakazo tumika ni kama ifuatavyo:
1. Timu kila timu inapaswa kusajili wachezaji 15 tu, kati yao kila timu itasajili wanawake wa 3.
2. Kila timu mwisho kusajili wachezaji wa 2 wa ligi kuu (ambao si lazima)
3. Mchezo utachezwa kwa dakika 20 (kumi kumi kwa kila kipindi) na dakika 2 za mapumziko.
4. Substution ni kadri uwezavyo.
5. Hakuna offside
6. Timu zitacheza Wachezaji saba kila upande akiwemo golikipa.
7. Mchezo ukichezwa na ikipatikana draw zitapigwa penati tatu, tatu na kuamua mshindi na ikishindikana kumpata mshindi utaratibu wa moja moja utachukuwa nafasi.

8. Timu mbili au tatu zikifungana :
A Pointi nyingi ndiye atakaye pita
B Kanuni ya tofauti ya magoli kuzingatiwa.
C Zilipo kutana wenyewe kwa wenyewe nani alimfunga mwenzie.

Bonanza hilo litatanguliwa na maandamano majira ya saa 2 asubuhi yatakayoanzia Uwanja wa Njamagana hadi Uwanja wa tukio CCM Kirumba.
Wadhamini: Serengeti premium lager, Isamilo hotel, club lips, Star max hotel, Malaika hotel, Nyumbani Hotels na G&G hotel.

NUKUU YA LEO.

Nukuu hii ipo langoni pa Msalato Secondary School.

MAJAMBAZI MWANZA WAONJA JOTO YA POLISI. "ONDOKA UKIWA UMEAGA KABISA IKIWA UTAINGIA MWANZA KUFANYA UHALIFU" AONYA KAMANDA

Jana majira ya saa kumi na dakika kadhaa jioni jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwatia nguvuni watu wanne wanaotuhumiwa kwa kufanya ujambazi wakiwa na bunduki moja aina ya smg na bastola mbili moja ikiwa na risasi 12 na na ya pili ikiwa na risasi 2.

Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekematwa katika eneo la mtaa wa libert jirani na benki ya NMB wakiwa kwenye harakati za safari kuelekea Nyegezi ambako walipanga kwenda kufanya uvamizi kwenye duka moja.

BASTOLA ZILIZOKAMATWA.
Awali majambazi hayo yalivamia bar moja eneo la kilimahewa na kuwalaza watu chini kisha kupora mali zao na kuiba bastola ya mteja mmoja. Majambazi hayo yaliyokuwa katika gari dogo yalipostukia kuwa yanafuatiliwa yalianza kufyatua risasi hovyo hali iliyosababisha shughuli za biashara kwenye eneo la tukio kusimama kwa muda.

RISASI 14.
Raia wema ndiyo waliofanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao bila ajizi walifuatilia nyendo za majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni.

Wawili kati ya majambazi hayo manne hali zao ni mbaya na wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando, mmoja katwangwa risasi mguuni na takoni ile hali mwingine sugu anayetambulika kwa jina maarufu 'Askofu' akiwa amevunjika mguu kabisa kwa kutwangwa risasi wakati alipojaribu kuitoroka mikono ya polisi.

"Watu wanatafuta fedha kwa njia zisizo halali kwa kutumia nguvu na hata kufanya mauaji ili wapate fedha kwaajili ya sikuu ya pasaka, napenda kuwatahadhalisha wote waliopanga kuingia Mwanza kufanya uhalifu kuwa waondoke wakiwa wameaga makwao kwani hawatatoka wakiwa salama" amesema kamanda Sirro.

Jeshi la polisi mwanza linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio zima ambamba na kuwahoji watuhumiwa wote wanne wa mkasa huo.

Tuesday, April 19, 2011

GOODLUCK JONATHAN NDIYE RAIS WA NIGERIA

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ambaye amechaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo, ametoa wito kwa raia kuwa watulivu na kumaliza kile alichokitaja kuwa ghasia na mauaji yasiyohitajika, Kaskazini mwa nchi hiyo. Rais Jonathan aliyasema hayo, baada ya kutangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais.Muda mfupi baada ya rais Jonathan, kutangazwa rasmi kama mshindi, wafuasi wa mpinzani wake mkuu Muhammadu Buhari, waliteketeza nyumba, makanisa na magari katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria.

Rais Jonathan amesema serikali yake itachukua hatua za dharura ili kulinda maisha ya raia na mali yao.


Wafuasi wa Generali Buhari, wanaripotiwa kusababisha ghasia hizo kulalamikia kile wanachodai kuwa ni wizi wa kura.

Shirika la msalaba mwekundi nchini Nigeria, limethibitisha kuwa watu kadhaa wameuawa. Makanisa na nyumba kadhaa ikiwemo ile ya makamu wa rais wa nchi hiyo Namadi Sambo katika jimbo la Kaduna zimeteketezwa.

Ripoti zaidi zinasema wafuasi hao wa Buhari walivamia gereza moja na kuwaachilia huru wafungwa wote. Hata hivyo, akizungumza na BBC msemaji wa Generali Buhari, amekanusha madai ya kuuawa kwa watu kadhaa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Ameongeza kuwa mwenyekiti wa chama chao tayari ametoa wito kwa raia kuwa watulivu.

BANANA ZORRO KULA PASAKA MWANZA....

USIKU WA BLACK $ WHITE NI THIS EASTER SUNDAY 24APRIL2011 NDANI YA CLUB Lips ILIYOPO ISAMILO LODGE MWANZA.
UKIJA UMETUPIA MAVAZI BLACK AU WHITE TUNAKUPIGA ZAWADI. DISCO LA UKWELI KUTOKA KWA DJ's KUTIKISA KUTA ZA SIKUKUU.

Imeletwa kwenu na
ISAMILO LODGE, CLUB Lips
PHOTOSPOT and Tanzania breweries.
,

SERIKALI YASITISHA SAFARI ZA LOLIONDO SABABU BABU ATAKA KULA PASAKA

SERIKALI mkoani Arusha imesitisha kwa muda safari za kwenda Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila kuanzia kesho hadi Aprili 25 mwaka huu.Uamuzi huo umetangazwa jana kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wali.

Shirima amewaambia waandishi wa habari mjini Arusha kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na utaratibu aliojiwekea mchungaji huyo kwamba hatatoa tiba siku za Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka. Mbali na kusitishwa kwa safari hizo kwa muda, watu wanapaswa kuzingatia utaratibu wa kwenda Samunge kwa vibali ili kuondoa msongamano usiokuwa wa lazima.

Kwa upande wake, Lali amesema kuwa urefu wa foleni ya magari Samunge sasa umefikia zaidi ya kilometa 10 kutoka kwa Mchungaji Mwasapila.


NYUMBA YA BABU.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila ameiomba Serikali idhibiti uingiaji zaidi wa magari yanayopeleka wagonjwa kupata tiba katika Kijiji cha Samunge kutokana na foleni kuwa kubwa na kutishia maisha ya wagonjwa.

Akizungumza kwa niaba ya mchungaji huyo, Msaidizi wake, Fred Nsajile amesema kama magari yasipodhibitiwa hasa yanayotoka Kanda ya Ziwa, vifo vinaweza kutokea.


60 WANUSURIKA AJALINI WAKIELEKEA KWA BABU.
Zaidi ya watu 60 wamenusurika kufa jana alfajiri baada ya basi walilokuwa wamepanda kutoka Kondoa, mkoani Dodoma kuanguka kabla ya kufika Samunge.

Basi hilo lililokuwa linaendeshwa na Idrisa Ramadhani lilianguka majira ya saa 10 alfajiri likiwa linashuka katika mlima uliopo eneo la Mdito. Baadhi ya abiria ambao wamejeruhiwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Samunge na hakuna aliyefariki.


WAGENI WAZIDI KUONGEZEKA SEMUNGE.
Raia wa nchini Uganda jana walianza kuingia kwa wingi Samunge, sambamba na wale wa Kenya ambao hadi jana mchana walikuwa wamefikia 2,568.

Raia wengine waliokwishafika Samunge ni wa nchi za Lebanon, Sweden, Uingereza, Zimbabwe, Rwanda, Uholanzi na Falme za Kiarabu (UAE).


kwa hisani ya mwananchi.

Monday, April 18, 2011

HAPA NA PALE....


Majuzi nikiwa pale Geita mida ya misosiz majira ya mchana ilipowadia nikaulizia sehemu pa chakula safi nao waungwana wakani elekeza hapa panapoitwa Maisha Plus, sasa baada ya kurekebisha nakushushia nikatoka mahala hapa nikijiuliza je! kijiwe hiki kina uhusiano wowote na Massoud Kipanya?

IAskwambie mtu' Ilani nyingine hazitekelezwi kutokana na jinsi zenyewe zilivyoandikwa 'kiuchafu-uchafu' kama choo hiki! laiti kama maneno haya yangeandikwa kwa maandishi mazuri ya thamani ninauhakika hata mtumiaji angeheshimu matumizi paswa ya choo tajwa.

Wenye lugha zao, 'ACHIA JIWE LIWAFUMUE'.

KISESA YAZINDUKA KISAWASAWA!!!....

Jana jioni kijiji cha Kisesa wilaya ya Magu, mkoa wa Mwanza kulikuwa na show safi yamtakato ya muziki wa kizazi kipya iliyofanyika kuhamasisha utumiaji wa vyandarua na vita dhidi ya maralia. ZINDUKA.Fid Q. alikuwa ndiye rais wa mpango huo nae alishiriki vilivyo kutoa elimu sambamba na kutoa burudani kwa hadhira. Duh hadi watoto wanazikwachu songi zake!!

Eh bana Mpango wa Zinduka umetuletea mengi kwani kuna vichwa vya ukweli vimejificha kitaa na hii ilikuwa fursa kuona kwaliti zao kama Mc huyu aitwe D-Malick' wa RNB na wimbo 'Mtima wange' ni nowmaaa mazee!

Mtoto atumwi dukani-Ingawaje Show hiyo iliingiliwa na mvua kubwa katikati wakati ndo ngoma imenoga, baadaye mvua hiyo ilikoma na utamu kuendelea...

Kwakila ambacho Fid Q. alikuwa akiwaomba mashabiki kufanya hawakumwangusha....!!

Jitah man aka Zagamba wenye roho mbaya lazima waisome namba akikamua...

Amini usiamini huyu ni babu wa miaka 62 jukwaani, aliwaacha hoi wananchi kwa kuzikamata fresh swaga za ki-hip hop, akinata na beat kwa mashairi makali...
Shangwe wacha zilipuke kwa babu!!!!Namuna hiii.

AAaaah! Wacha Babu awe *Star* cheki kwenye snepu Watangazaji Philbert Kabago wa Passion Fm (shoto) na Ezden (kiss Fm).

Adja-dja-dja- Pale katii bonge la 'mmechisho'

Toka rock city wasanii lebo ya Mo-records kwa producer Q.The Don pichani kutoka shoto ni X-lady, B-snicker na Zombi.

Kabla ya burudani hiyo . Balozi wa malaria Fid Q alitembelea nyumba kwa nyumba kukagua, kuangalia na kuona kama kaya jeh! zimepata vyandarua? jeh! vinatundikwa? na vinatundikwaje?

"Kulala kwenye chandarua hiki kila siku kutakukinga dhidi ya maambukizi ya malaria" Fid Q akimsaidia kutundika mama wa kaya hii mwalimu Pendo Musa wa shule ya msingi Gedeli B.

Kwa mujibu wa Distinct coach bwana Timoth Lugejuna: Mtaa wa Nyakato mashariki jumla ya nyumba zipatazo 270 zimekaguliwa mpaka sasa ikiwa malengo ni kukagua nyumba 420. Twawashukuru sana na twawatakia usingizi mnono kwenye vyandarua vyenu pindi usiku utakapoingia. by ZINDUKA