Msama ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, amesema kwamba wanamuziki hao tayari wamekwisha wasili nchini kwa ajili ya tamasha hilo ambalo la kwanza litafanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Tamasha la Pasaka la mwaka huu linawashikisha waambiji wote nyota wa muziki wa Injili wanaotamba nchini na pia wengine kutoka nyingine barani Afrika. Waaimbaji watakaoshiriki kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Rose Mhando, Boniface Mwaitege, Christina Shusho, Updeno Nkone, Faraja Ntatoba kutoka nchini DR Congo, Ephraime sekeleti kutoka Zambia na Anastazia Mukabwa kutoka Kenya.
Wengine ni Solomon Mukubwa, Geraldine Odour na Pamela Wandela wote kutoka nchini Kenya.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment