Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea wakati wa kikao cha wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza hapo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa mkoa wa Iringa amepiga
marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia
biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania
hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.
Akizungumza kwenye mkutano
na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi
alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya
biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha
kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.
“Toka nikiwa mkuu wa wilaya
najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi
ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema
Hapi
Hapi aliwataka polisi
wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.
Kauli hiyo imekuja mara
baada ya katibu na mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wadogo wadogo (machinga)
kutoa kilio hicho mbele ya mkuu ya mkoa kwa kusema wamekuwa wakinyanyaswa na
askari ambao wanafanya kazi katika stand kuu.
Katibu wa wafanyabiasha wadogo wadogo manispaa ya Iringa Joseph Kilyenyi alisema kuwa baadhi ya viongozi wa
halimashauri ya manispaa ya Iringa pamoja na baadhi ya polisi wamekuwa kikwazo
cha kufanya biasha kwa uhuru na kuongeza pato la manispaa ya Iringa.
“wafanyabiasha wadogo wadogo tupo zaidi ya elfu moja tukiwekewa mfumo sahihi kwa wakati sahihi tunaweza
kutoa kodi zaidi ya shilingi milioni tisa
ambapo hapo tunatoa shilingi mia tatu
na ikiwa shilingi mia tano halmashauri itaingiza mapato mengi ambayo
yatachangia maendeeleo ya manispaa” alisema Kilyenyi
Kilyenyi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo wa manispaa ya Iringa wapo tayari kulipa kodi kama ambavyo Rais wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo na
kuwapa nafasi wafanyabiasha wadogo wadogo kufanya kazi kwa uhuru na kuchochoe
maendeleo.
“Serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli amekuwa
akitupelea na kuthamini hivyo hata sisi tunawajibu wa kuhakikisha tunalipa
ushuru na kodi pale inapotakiwa ili kukuza juhudi za kuleta maendeleo ya nchi
yetu” alisema Kilyenyi
Kilyenyi alimpongeza mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard kasesela pamoja na MNEC wa mkoa wa Iringa Salim Asas
kwa kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiwakabili wafanyabiasha wadogo wadogo
“Baada ya kupokea kero za wafanyabiasha wadogo wadogo mkuu wa mkoa wa Iringa Hapi alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya
Iringa ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao utakuwa
utasidia kukusanya kodi kwa wafanyabiasha hao.
Nimetoa siku thelathini kwa
viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao hausababisha
wafanyabiasha wadogo wadogo kulipa kodi katika maeneo wanayofanyia kazi ili
kuwaondolea usumbufu wa kuwafuta mliko” alisema Hapi
Aidha hapi alisema kuwa
hatawavumia viongozi wowote wale ambao watakwamisha kuijenga Iringa mya ambayo
inatakiwa kuwa kama kituvu cha utalii nyanda za juu kusini
Naye afisa biashara wa
manispaa ya Iringa kassim majariwa alisema kuwa ameyapogea maagizo yote ambayo
mkuu wa mkoa ameagiza kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi
katika halmashauri ya Iringa.