ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 7, 2018

VIDEO:- RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA POLE KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOPATA AJALI



GSENGOtV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa Waandishi wa Habari waliopata ajali katika Msafara wake wa Ziara ya fupi mkoani Mwanza.

Akiwasilisha salamu hizo za pole, mapema asubuhi ya leo  kwa Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kuwa Rais anatambua mchango wa Waandishi kwa maendeleo ya taifa, upashaji wa habari na uelimishaji na toka alipofika jijini hapa 3, Septemba 2018 na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo utiaji saini mkataba wa Kandarasi ya  ujenzi wa meli kubwa ya kisasa wamekuwa wakitoa ushirikiano bila kuchoka kwa maslahi ya umma.

"Waandishi wa Habari wamefanya kazi kubwa mimi mwaka wa tatu nipo jijini hapa  mnatueleza changamoto ziko wapi naomba tuendelee hivyo kuchangia maendeleo ya nchi yetu," alisema Mongella.

Wakizungumzia ajali hiyo iliyotokea kwenye msafara wa Ziara ya fupi ya Rais, wilayani  Bunda kuelekea Kisorya ilisababishwa na mwendo kasi, vumbi kuwa jingi, madereva kushindwa kuona mbele hata 9dkupelekea magari kugongana na jingine kupinduka Waandishi hao walikuwa na haya ya kusema.

Aidha mmoja kati ya Wanahabari waliopata ajali hiyo Emmanuel Meshack aliyeumia sehemu ya bega na goti la mguu, ameshukuru Serikali ya Mkoa kutambua umuhimu wao na kuomba wasisite kutoa ushirikiano kwa waandishi kwa maendeleo ya Taifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.