ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 25, 2025

MABINGWA WATETEZI IVORY COAST WAICHAPA MSUMBIJI 1-0

 


MABINGWA watetezi, Ivory Coast wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa Kundi F jioni ya leo Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
24 December 2025 – Marrakech – Grand Stade de Marrakech 


Match : Côte d’Ivoire 1-0 Mozambique 

Amad Diallo – Forward- Côte D’Ivoire


Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Samuel Uwikunda wa Rwanda, bao pekee la The Elephants limefungwa na winga wa Manchester United, Amad Diallo dakika ya 49.

EYONG AFUNGA BAO PEKEE CAMEROON YAICHAPA GABON 1-0

 


BAO la dakika ya sita la mshambuliaji wa Levante ya Hispania, Karl Edouard Blaise Etta Eyong limeipa Cameroon ushindi wa 1–0 dhidi ya Gabon katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco inayoendelea michuano hiyo. 
Bryan Mbeumo.

Bryan Mbeumo, Mchezaji Bora wa Mechi: 
"Nina furaha sana. Timu ilicheza mchezo mzuri. Tulikuwa imara na tumefurahishwa na ushindi. Tulijua Gabon wangekuwa mpinzani mgumu, lakini dhidi ya Côte d'Ivoire itabidi tuwe tayari kwa sababu tunajua ni timu yenye nguvu sana. 

Tulikaa makini na imara sana. Kila mtu alilinda vizuri na alifanyia kazi kwa bidii matokeo ya kila mmoja."
Cédric Moubamba,

Cédric Moubamba, Kocha Msaidizi wa Gabon: 
"Hatukuwa na mwanzo mzuri wa mechi, jambo ambalo lilifanya mambo kuwa magumu kwetu. Tuliruhusu bao kutoka kwa pasi na safu mbovu ya ulinzi. Utambulisho wa Aubameyang na Lemina ulipangwa, lakini mwendo wa mechi ulimaanisha walikuja mapema. 

Na tuliona ni kiasi gani walitusaidia kushinda mechi yao. Cameroon ni kweli. vizuri na kulinda uongozi wao vyema ni juu yetu kurejea kazini na kujiboresha kwa mchezo unaofuata.

Wednesday, December 24, 2025

USIKU WA SIMULIZI - NILITAKA KUJIUA , MCHUMBA WANGU KAOA MKE MWINGINE SEHEMU YA KWANZA.```

 Alikuwa mwanamke aliyejenga ndoto za maisha na mchumba wake kwa matumaini na subira kubwa, akiamini ahadi walizoshirikiana zingefikia siku ya ndoa;

Hata hivyo ghafla alijikuta akiachwa bila maelezo ya kuridhisha huku yule aliyempa matumaini akigeuka na kwenda kumuoa mwanamke mwingine jambo lililomuacha na maumivu ya moyo maswali yasiyo na majibu na funzo zito kuhusu ukatili wa mapenzi na mabadiliko ya ghafla ya ahadi za binadamu.

Sunday, December 21, 2025

MGANGA MKUU MANISPAA YA KIBAHA ACHARUKA AKEMEA TABIA YA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KWA MAZOEA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dr. Catherine  amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kuagiza kuimarishwa kwa huduma za wateja katika vituo vya afya ili kuboresha huduma ya matibabu.


Pia ametoa wito kwa kamati za afya kuhakikisha wanaweka misingi mizuri ya  kujadili kwa kina taarifa za takwimu zilizowasilishwa katika kikao cha tathmini ya mwaka 2024/2025 kwa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe.

Hayo ameyabainisha wakati wa kikao hicho cha tatmini kwa kipindi cha mwaka wa 2024/2025 Dkt. ambapo amebainisha kuwa  idara ya afya wanapaswa   kufanikisha ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha asilimia 50 hadi kufikia kipindi cha tathmini.

Kadhalika  amesisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mikakati madhubuti ya upatikanaji wa bima ya afya kwa wananchi wote, wakianza na kaya zenye mahitaji maalum.

Amesema  kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote utaanza kwa kaya ambazo zitachangia kiasi cha shilingi 150,000 kwa mwaka kwa ajili ya baba, mama na watoto, na kuagiza utolewaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na mpango huo.

Aidha,  ameongeza kuwa kuanzia Januari 2026, kituo cha afya cha Kilimahewa kianze kutoa huduma rasmi. Alionya kuwa mtu yeyote aliyepokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi lakini hawezi kuumaliza, anatakiwa kutoa taarifa mapema kwa uongozi.

 
Kwa upande wake, Mratibu wa Kitengo cha Dharura, Dkt. Majaliwa, alieleza kuwa kuna upungufu mkubwa wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani, na kueleza kuwa walipo ni wachache na hawapati posho zao kwa wakati. 

Pia amebainisha kuwa madereva wa sekta ya afya pia hukumbwa na changamoto hiyo hiyo ya kucheleweshwa kwa malipo yao.

Naye mwakilishi kutoka Ofisi ya Utumishi wa Umma Happyness Anania akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  amewataka watumishi kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinafikishwa kwa viongozi wao moja kwa moja.

Ameingeza kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha watumishi wanasililizwa  kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kina na kusisitiza suala la  umuhimu wa kubuni njia mpya za kuongeza mapato kupitia sekta ya afya.