ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 27, 2023

VICTORIA MARATHON 2023 ITAKAYOFANYIKA MWEZI JULY JIJINI MWANZA SAFARI HII 'NI FULL UTALII'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Mashindano ya riadha ya Transec Lake Victoria marathon kwa msimu wa tatu yanatarajia kufanyika Julai 2 mkoani Mwanza kwa kushirikisha wanariadha zaidi ya 1400 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali. Hayo yamesemwa na Mratibu wa mbio hizo Halima Chake wakati wa uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Mwanza Yatch Club pembezoni mwa Ziwa Victoria jijini Mwanza. Chake amesema kutakuwa na mashindano ya Kilomita 2.5 kwa watoto chini ya umri wa miaka 10,kilomita 5,kilomita 10 na kilomita 2.1, huku akizitaja gharama za ushiriki kwa kiliomita ni Shilingi 20,000, Kilomita 5 ni shilingi 30,000, Kilomita 10 ni shilingi 35,000 na Kilomita 21.1 ni Shilingi 35,000. Amesema usajili umeshafunguliwa rasmi, nakutoa wito kwa wakimbiaji wote kujisajili kwa wingi tufanikishe lengo lililokusudiwa. Aidha mratibu huyo amewashukuru wadau mbali mbali kwa udhamini wao katika mbizo zao ambapo baadhi ya wadau ni Transec, benki ya KCB,TBL na Konyagi. Mnamo mwaka jana (2022) mashindano hayo yalirejesha kwa jamii kupitia kituo cha watoto wenye uhitaji kwa kuwapatia bima ya afya watoto 85. Naye Katibu Tawala msaidizi wa mkoa wa Mwanza upande wa uwekezaji na Biashara Patrick Karangwa pamoja na kuushukuru uongozi wa Lake Victoria marathon kwa kuandaa mbio hizo pia ameziomba kampuni na mashirika mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono mbio hizo. Ameyataja mashindano kama chachu ya kuutangaza mkoa wa Mwanza kama sehemu ya kuhifadhi Ziwa Victoria na kuchochea biashara kwani kwenye msimu wa mbio hizi biashara zinafanyika na tukio hilo limekuwa likichochea na kukuza utalii Karangwa ameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mbio hizo zinafanyika kwa mafanikio makubwa kama zilivyo mbio za Kilimanjaro na kwingineko. "Matukio kama haya yanawezesha kukuza uchumi, kuainsha na kuzitangaza fursa za mkoa wetu sanjari na kuwakutanisha watu kujenga uhusiano wa kibiashara huku fedha zinazochangwa zikirudi katika kuisaidia jamii. Naye ofisa Mwakilishi wa kampuni ya Transec Victor Okeyo amesema kampuni yake itaendelea kuchangia kwa kile kinachoweza kufanikisha lengo la kuisaidia jamii. "Mbio ni sehemu mojawapo ya vitu vinavyotusaidia kuwa na afya bora, nawaomba wanamichezo washiriki kwa wingi katika mbio hizi" "Kanda ya Ziwa imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio yetu, na tunaona ni uamuzi sahihi kurudisha faida kwao" ilisema sehemu ya hotuba ya Victor Okeyo. #mwanza #samiasuluhuhassan #LakeVictoriaMarathon

SHUHUDIA MWANZO MWISHO - MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIAGIZA BAR NA KUMBI ZA STAREHE KUFUNGULIWA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

KIKAO cha wafanyabiashara wa bara na kumbi za starehe jijini Mwanza kimetamatika kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla kuagiza #kaziiendelee kwa baa na kumbi za starehe zilizofungiwa na Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) zifunguliwe huku akipiga marufuku kamata kamata ya nguvu na kuvizia inayofanywa na baraza hilo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Licha ya kuwa anakabidhiwa ofisi Mei 28 mwaka huu, Makalla ambaye aliteuliwa Mei 15 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akitokea Dar es Salaam ametoa maagizo hayo jana Mei 26, 2023 baada ya kukutana na kusikiliza kero za wamiliki, mameneja na wafanyakazi wa baa, hoteli, kumbi za starehe na burudani jijini Mwanza. Shuhudia kikao hicho mwanzo mwisho kupitia #JembeFmTz #mwanza #samiasuluhuhassan #kaziiendelee

Thursday, May 25, 2023

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA KUFUA UMEME NCHINI UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

 


Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.



KiIBAHA MJI YAJA NA MPANGO KABAMBE WA KUKUSANYA BILIONI 45.8 MAPATO YA NDANI


Na Victor Masangu,Kibaha

Halmashauri ya mji Kibaha kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 imekadiria kukusanya zaidi ya shilingi bilionj 45.8 kutokana na ruzuku, mapato yake ya ndani pamoja na mashirika mbali mbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha Selina Wilson wakati wa kikao cha Baraza la madiwani kwa kipindi Cha robo ya tatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka 2023.

Makamu huyo alibainisha kwamba kwa upande wa makusanyo kuanzia mwezi julai mwaka 2022 hadi machi 2023 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 29.9 ikiwa sawa na kiwango cha asilimia 65.5.

Aliongeza kuwa halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai 2022 hadi kufikia Machi 2023 kiasi cha shilingi mqilioni 587.8 ikiwa sawa na asilimia zipatazo 116 ya makisio ya mwaka.

Akizungumzia kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023 imepanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 113 kwa ajili kutumika katika miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira Hamis Shomari alisema kuwa kwa sasa zoezi la utambuzi wa wananchi waliovamia katika eneo la mtaa wa mkombozi limefanyika na kwamba wananchi 4509 tayari wameshatabuliwa.

"Uuzaji wa viwanja katika mtaa wa mkombozi umeshaanza ramsi tangu tarehe 24 mwaka huu ambapo wananchi walishajulishwa,ambapo jumla ya ankra ya viwanja 168 katika mtaa wa mkombozi zimeshatolewa,"alibainisha Shomari.
Akizungumzia kuhusiana na wananchi ambao wamevamia katika mtaa wa Lumumba tayari kazi ya utambuzi imeshafanyika ambapo wananchi wapatao 6952 wameshatambulika na kazi ya michoro 8 yenye viwanja 7,264 imekamilika.

                  
Kwa upande wake Mwnyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba amewahimiza madiwani kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kuleta tija kwa maslahi ya wananchi.


Wednesday, May 24, 2023

KAMISHNA WA POLISI JAMII CP SHILOGILE AMEZINDUA JENGO LA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO HALMASHAURI YA MSALALA KATA YA BUGARAMA.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi DCP, Merry Nzuki akiwasalimia Wananchi (Hawapo Pichani) kabla ya uzinduzi wa Jengo la Dawati na Jinsia na Watoto mkoani Shinyanga, Halmashauri ya Msalala Kata ya Bugarama. (PICHA NA JESHI LA POLISI)


Kamishna wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine  Shilogile, Mkuu wa Wilaya ya Msalala Mboni Mhita mwenye Suti nyeusi, Naibu Mkurugenzi Mkazi Nchini Tanzania Heo Eun na Melissa Barrett Naibu mwakilishi mkazi  toka UNFPA Tanzania wakiwa katika Picha ya pamoja katika zoezi la kukata utepe katika uzinduzi wa Jengo la Dawati Kata ya Bugarama.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

Kamishna wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine  Shilogile kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Msalala Mboni Mhita, mwenye suti nyeusi upande wa pili ni Naibu Mkurugenzi Mkazi Nchini Tanzania Heo Eun na Melissa Barrett Naibu mwakilishi Mkazi  toka UNFPA Tanzania wakiwa katika Picha ya pamoja katika zoezi la kuvuta kitambaa kuashilia Ufunguzi wa Jengo la Dawati Kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

Pwani kumekucha yapasua mawimbi miradi yote 99 ya maendeleo yapitishwa na mwenge wa uhuru

 Na Victor Masangu,


Jumla ya  miradi  99 ya maendeleo ambayo imetembelewa na mingine kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Asmsingi katika Mkoa wa Pwani imefanikiwa kupitishwa yote bila ya dosari yoyote na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wakati a awwkimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Robert Chalamila katika eneo la tazara na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja  na serikali.

Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge wa uhuru ukiwa katika mkoa wa Pwani umeweza kukimbizwa umbari wa kilometa zipatazo 1201 katika Wilaya saba na halmashauri zipatazo tisa.


Alifafanua kuwa katika miradi hiyo mbali mbali  ya maendeleo ambayo imeweza imegusa katika sekta mbali imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi  tilioni 4.4 ambazo zimetoka serikalini na nyingine kwa wadau wa maendeleo.

Kunenge alibainisha kuwa katika mbio hizo miradi tisa iliweza kufunguliwa na mingine 15 kuzinduliwa huku miradi mingine 20 iliweza kupata fursa ya kuwekewa mawe ya msingi huku miradi 15 imekaguliwa.

"Tunashukuru tumemaliza salama kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu wa Pwani na kwamba miradi yetu yote imeweza kupitishwa bila ya kuwa na dosari yoyote Ile kutokana na kuwa na vigezo ambavyo vinatakiwa,"alisema Kunenge.

Kwa Upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim alisema kwamba ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo wameweza kuitembelea.

Alimpongeza kwa dhati mkuu wa .Mkoa wa Pwani kwa kuweza  kusimamia watendaji wake katika suala zima la  kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itaweza kuwasaidia wananchi.

Nao baahi ya viongozi walioudhulia katika makabidhiano hayo hawakusita kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa Mkoa wa Pwani kwa kujitahidi kuibua miradi hiyo ambayo imefanikiwa kupitishwa yote bila kukataliwa.



Walisema kitendo cha miradi yote 99 kupitiwa na mbio za Mwenge na kufanikiwa kupitishwa bila dosari yoyote ni mafaniko makubwa kwani inaonyesha namna ya watendaji wanavyojitahidi kushirikiana bega kwa bega kwa maslahi ya wananchi kwa ujumla.


Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Pwani zimeweza kupita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuweka mawe ya msingi.kufunguliwa,kuzinduliwa na mingine kutembelewa katika sekta tofauti.

Tuesday, May 23, 2023

WANANCHI MAFIA WAONDOKANA NA KILIO CHA CHANGAMOTO YA JENGO LA DHARULA NA MAHUTUTI.

 


Na Victor Masangu,Mafia 


Wananchi wa Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani wamemshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta za afya ,elimu,maji na mambo mengine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilayani Mafia kwa ajili ya kutembelea ikiwa sambamba na  kukagua,kuzindua,na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Mmoja wa wananchi hao Amina Tuki alisema kwamba ujio wa Mwenge wa Uhuru ni mkombozi mkubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo na wananchi kuweza kupata fursa ya kupata huduma za kijamii kwa urahisi.

Aidha alipongeza juhudi zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi  (ICU) pamoja na jengo la dharura.

"Kwa kweli tunashukuru sana ujio wa Mwenge wa Uhuru umeweza kuja na kutembelea miradi yetu ya maendeleo sisi kwetu imeweza kutusaidia wananchi kutokana na kuwepo kwa huduma ambazo tunazipata kama vile,maji,afya,elimu na mambo mengine muhimu,"alisema 

Kwa upande wake  kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa  AbdalahKaim amewapongeza  viongozi wa Wilaya ya Mafia kwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

 Kadhalika kiongozi huyo amewahimiza watendaji na viongozi kuitunza na kuilinda miradi ambayo wameianzisha ikiwa sambamba na kuunga mkono  juhudi  zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.


 Pia amebainisha kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuendekea kuwafikishia huduma za Afya Kwa ukaribu wananchi wake Ili kuondokana na gharama kubwa kwa ajili ya kupata matibabu.


Awali akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya Ya Mafia Zephania Sumaye amesema mwenge huo utakimbizwa kilomota 99.8 na utatembelea, kuzindua, Kufungua,na kukagua miradi mbali mbali.



Awali akisoma taarifa ya  mradi wa jengo la wagonjwa mahututi  Mganga Mkuu wilaya amesema Mradi huo umegharimu Kiasi Cha Milioni miatano  sitini na nne lengo ikiwa kuboresha huduma za Afya pia  majengo haya yatapunguzo vifo visivyo vya lazima kupunguza Gharama za rufaa Kwa  Wananch


Naye Mbunge wa Jimbo la Mafia Omary Kipanga amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya maendeleo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na wananchi wake katika kuwaletea mabadiliko chanya.

ZAIDI BILIONI 126 HUPATIKANI KUTOKANA NA ZAO LA UFUTA MKOA WA LINDI

 

Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kamishina wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Mhe. Zainab Telack akizingua gari kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Lindi ambapo gari hilo limetolewa na  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) limekabidhiwa wakati wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi lililofanyika Mjini Lindi likiwa na kauli mbinu "Ushirika ni Biashara". Kwenye jukwaa hilo Mkuu wa Mkoa,ametoa rai kwa wana Lindi wanaojishugulisha na masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kujiunga na Vyama vya Ushirika ili waweze kuuza kwa  pamoja kwenye soko.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kamishina wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Zainab Telack akikagua bada la mjasiliamali anayeuza bidhaa za asili Kwenye Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi,ametoa rai kwa wana Lindi wanaojishugulisha na masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kujiunga na Vyama vya Ushirika ili waweze kuuza kwa  pamoja kwenye soko.
Washiriki mbalimbali walioshiliki Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi
Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkoa wa Lindi umekuwa unapata Zaidi ya bilioni 126 kutokana na uuzaji wa zao la ufuta kutoka wilaya zote za mkoa huo kutokana na zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakhabadhi gharani.

Akizungumza wakati wa jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Lindi 2023, mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Taleck alisema kuwa wamekuwa wakipata kiasi cha fedha kutokana na mazao ambayo yamekuwa yanahifadhiwa kwa mfumo wa stakhabadhi gharani.


Taleck alisema kuwa shilingi billion 126 zimepatikana kwenye zao la ufuta kutoka na kuuza zao hilo kwa njia ya stakhabadhi gharani ambapo wakulima wamekuwa wakipangia bei tofauti na zamani wakulima walikuwa wanapangiwa bei.

Telack amewataka wakulima na wavuvi kuingia katika vyama mbalimbali vya ushirika kwa lengo la kujenga umoja,kuongeza vipato vyao na kupata uongozi utakaoenda kutetea haki na maslahi ya shughuli zao wanazozifanya

"Uaminifu na Uadilifu tu ndio unaowaweka salama viongozi wa ushirika na wakulima salama hivyo amewataka kuacha vitendo viovu vinavyodhorotesha Maendeleo ya Ushirika ndani ya Mkoa wa Lindi"

Alimalizia kwa kuwataka wakulima kuuza mazao mbalimbali kwa njia ya stakhabadhi gharani ili wapate faidi ya kilimo wanacholima.

Kwa mwenyekiti wa vyama vya ushirika Odasi Mpunga alisema kuwa wakulima wanatakiwa kuuza mazao kwa mfumo wa stakhabadhi gharani ili wapate faida kulingana na thamani ya mazao yao.

Mpunga  aliwaomba wakulima wa zao la mbazi kuanza kuuza zao hilo kwa njia ya stakhabadhi gharani ili nao wapate faida kama wakulima wengine ambavyo

Naye naibu Mrajis Uhamasishaji, Consolata Kiluma, amevitaka Vyama vya Ushirika Mkoani Lindi kushirikiana na Maafisa Ushirika na ofisi ya Mrajis Mkoa kujibu  hoja za wakulima kwa wakati. 

Naibu Mrajis amesema kuwa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi vimefanikiwa kusajili  vyama ila idadi ya wakulima na wanachama wamewasajili  wachache hivyo wamalizie kusajili wakulima wao wote wanaowahudumia.

Monday, May 22, 2023

Mfuko wa WCF watoa Mafunzo ya Tathmini kwa Madaktari Kanda ya Ziwa

 

Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepewa mafunzo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ili kuwawezesha kufanya tathmini stahiki kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini.

Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku tano kuanzia Jumatatu Mei 22, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka washiriki kuzingatia elimu watakayoipata.

“Mkahakikishe tathmini zinafanyika kwa usahihi na wafanyakazi watakaopata majanga ya ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wapate fidia stahiki na kwa wakati. Hii itaongeza ari kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii wakijua wana uhakika wa kinga ya majanga kazini” amesema Masala.

Masala ambaye amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla ameongeza kuwa ni vyema waajiri wakahakikisha wafanyakazi wao wanajiunga na mfuko wa WCF ili kuondolewa mzigo wa gharama za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea kazini.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, amesema mafunzo hayo yatawaongezea weledi madaktari hao kufanya tathmini sahihi na kwa wakati hatua itakayosaidia pia wafanyakazi wanaopata majanga kazini kulipwa fidia stahiki na kwa wakati.

Baadhi ya madaktari walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi wamekiri kuwa yatawaongezea ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi zaidi na hivyo WCF kulipa fidia stahiki.

Mfuko wa WFC ulianza kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini mwaka 2016 ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa, ukichukua nafasi ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo ilionekana kutotoa fidia stahiki kwa wafanyakazi waliopata majanga kazini.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanaoumia wakiwa kazini.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Mei 22, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu WCF.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera ili kuwaongezea ujuzi wa kufanya tathmini kwa wafanyakazi wanaoumia kazini (kupata ajali, kuugua ama kufariki wakiwa kazini) ili kupata fidia stahiki na kwa wakati kutoka WCF.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo hayo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia kufanya tathmini kwa weledi zaidi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini.
Daktari kutoka Hospitali ya Magai Kahama, Dkt. Peter Magai akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo ambao ni pamoja na kuwawezesha madaktari kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa WCF wanaoumia kazini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Madaktari walioshiriki mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Profesa Mkenda kufungua maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu UDSM

 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anatarajia kufungua maonesho ya nane ya Utafiti na Ubunifu yanayotarajia kuanza Mei 23 - 25, 2023 katika Viwanja vya Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Akizungumza na Wanahabari Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu "Utafiti na Ubunifu kwa Ustawi wa Uchumi - jamii nchini Tanzania"

Prof. Nelson Boniface asema kuwa maonesho hayo yatataguliwa na ufunguzi ambapo wazungumzaji watakuwa ni Leticia Lutashobya ambaye ni mbobezi katika masuala ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Michael Shirima mwenyekiti na Mwanzilishi wa Presicion Air Tanzania.

Amesema kuwa katika maonesho hayo ya nane wanatarajia kuonesha miradi 99 iliyotokana na maonesho yalifanyika katika ngazi ya vitengo ambapo jumla ya miradi 350 na wakachagua hiyo 99.

"Malengo ya Tafiti hizi ni kuwavutia wanataaluma kutoka chuo chetu na taasisi nyingine zinazohusiana na Taaluma Pamoja na utafiti na watu wote wa serikalini ikijumlisha wenye viwanda kuja kushuhudia tafiti na bunifu zao wanazofanya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," amesema Prof. Nelson Boniface.

Ameongeza kuwa tafiti zote zinazofanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zinalengo la kuboresha maisha ya Watanzania hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kuhudhuria maonesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbali mbali.

MWENYEKITI WA UVCCM UBUNGO ANOGESHA NUSU FAINALI KIMWANGA CUP, HAWA ABDUL REDE CUP KWA KISHIND0

 



Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

Hekaheka za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu katika ligi ya Kimwanga CUP na mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP yamepamba moto huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula, akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Katika mtanange huo kwa upande wa mpira wa miguu umezikutanisha timu za Ting Wayland ambapo ilifanikiwa kuvuka hatua ya fainali kwa kuchambana timu cha kituo cha kulea vipaji Lamasia FC kwa bao 2-0 huku upande wa Rede timu ya Kanuni ikifanikiwa nayo kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.


Hayo ameyasema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayopigwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, katika mashindano hayo ya kuwania ng’ombe aliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo, Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulraman ambaye amekutanisha mabinti nao kuwania ng’ombe katika michuano hiyo.


“Kwanza, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wetu kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake yanawasaidia vijana wetu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, lakini pia inasaidia kupata exposure (fursa) na kubwa zaidi kutengeneza mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi.


“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakeleketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza nusu fainali kuhakikisha kuwa wakati wa michezo hiyo inapoendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu tutakapoanzisha vurugu uwanjani hapa tutawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwa ujumla wake,” amesema Makangula


Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amewataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao michezo hiyo iwe endelevu.

Sunday, May 21, 2023

YANGA YAKATA TIKETI NYINGINE KWA FAINALI NYINGINE

 

MFUNGAJI mwenye kasi ya hatari kuwatesa makipa ndani ya Bongo msimu wa 2022/23 amepachika bao pekee la ushindi katika hatua ya nusu fainali ya pili ya Azam Sports Federation yupo Yanga.

Anaitwa Fiston Mayele amemtungua Benedick Haule wa Singida Big Stars dakika ya 82 na kubadali usomaji wa ubao kwenye mchezo huo.

Mpaka inagotea dakika ya 90 ubao umesoma Singida Big Stars 0-1 Yanga.

Sasa Yanga inakwenda kutetea taji lake mbele ya Azam FC ambao walitangulia katika nusu fainali ya kwanza.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi ni Yanga ambao walitwaa taji hilo mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa fainali.

Mayele ni mshambuliaji hatari mwenye ushikaji mkubwa na nyavu.

Uwanja wa Liti kwa Singida Big Stars ni huzuni huku Yanga kwao ikiwa ni kicheko mwanzo mwisho mpaka watakapokwenda Tanga kucheza fainali.