Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kamishina wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Mhe. Zainab Telack akizingua gari kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Lindi ambapo gari hilo limetolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) limekabidhiwa wakati wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi lililofanyika Mjini Lindi likiwa na kauli mbinu "Ushirika ni Biashara". Kwenye jukwaa hilo Mkuu wa Mkoa,ametoa rai kwa wana Lindi wanaojishugulisha na masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kujiunga na Vyama vya Ushirika ili waweze kuuza kwa pamoja kwenye soko.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Kamishina wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Zainab Telack akikagua bada la mjasiliamali anayeuza bidhaa za asili Kwenye Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi,ametoa rai kwa wana Lindi wanaojishugulisha na masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kujiunga na Vyama vya Ushirika ili waweze kuuza kwa pamoja kwenye soko.
Washiriki mbalimbali walioshiliki Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi
Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Lindi
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkoa wa Lindi umekuwa unapata Zaidi ya bilioni 126 kutokana na uuzaji wa zao la ufuta kutoka wilaya zote za mkoa huo kutokana na zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakhabadhi gharani.
Akizungumza wakati wa jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Lindi 2023, mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Taleck alisema kuwa wamekuwa wakipata kiasi cha fedha kutokana na mazao ambayo yamekuwa yanahifadhiwa kwa mfumo wa stakhabadhi gharani.
Taleck alisema kuwa shilingi billion 126 zimepatikana kwenye zao la ufuta kutoka na kuuza zao hilo kwa njia ya stakhabadhi gharani ambapo wakulima wamekuwa wakipangia bei tofauti na zamani wakulima walikuwa wanapangiwa bei.
Telack amewataka wakulima na wavuvi kuingia katika vyama mbalimbali vya ushirika kwa lengo la kujenga umoja,kuongeza vipato vyao na kupata uongozi utakaoenda kutetea haki na maslahi ya shughuli zao wanazozifanya
"Uaminifu na Uadilifu tu ndio unaowaweka salama viongozi wa ushirika na wakulima salama hivyo amewataka kuacha vitendo viovu vinavyodhorotesha Maendeleo ya Ushirika ndani ya Mkoa wa Lindi"
Alimalizia kwa kuwataka wakulima kuuza mazao mbalimbali kwa njia ya stakhabadhi gharani ili wapate faidi ya kilimo wanacholima.
Kwa mwenyekiti wa vyama vya ushirika Odasi Mpunga alisema kuwa wakulima wanatakiwa kuuza mazao kwa mfumo wa stakhabadhi gharani ili wapate faida kulingana na thamani ya mazao yao.
Mpunga aliwaomba wakulima wa zao la mbazi kuanza kuuza zao hilo kwa njia ya stakhabadhi gharani ili nao wapate faida kama wakulima wengine ambavyo
Naye naibu Mrajis Uhamasishaji, Consolata Kiluma, amevitaka Vyama vya Ushirika Mkoani Lindi kushirikiana na Maafisa Ushirika na ofisi ya Mrajis Mkoa kujibu hoja za wakulima kwa wakati.
Naibu Mrajis amesema kuwa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi vimefanikiwa kusajili vyama ila idadi ya wakulima na wanachama wamewasajili wachache hivyo wamalizie kusajili wakulima wao wote wanaowahudumia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.