ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 25, 2014

AJALI NYINGINE YA NDEGE YAUWA 116.

Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.

Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso , Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga. KWA HISANI YA BBC.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MKOA WA MWANZA.

Askari wa parade akimkabidhi mkuki na ngao mwakiliashi  wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kwaajili ya uwekaji wa silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, akiweka silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe. Anthony Diallo, akisali mara baada ya kuweka silaha za asili za upinde na mshale, kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mr. Mkabenga, akiweka shoka kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Mwakilishi toka kanisa la Roman Catholic akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Wawakilishi toka watu wa madhehebu ya Hindu Union wakiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mama Joyce Masunga akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza
Wimbo wa Taifa ulipigwa.
Wadau mbalimbali wamehudhuria katika maadhimisho haya muhimu.
Wadau mbalimbali wamefika hapa ili kushiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa, yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza.
Eneo la tukio.
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa ambayo kitaifa yamefanyika leo kote nchini, ambapo katika ngazi ya mkoa pia yamechukuwa nafasi mkoani Mwanza.

Ndani ya 88.1 maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere, kwa Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa na wananchi kukusanyika katika eneo la kumbukumbu ya mnara wa mashujaa na kufanya ibada zikiwemo shughuli za uwekaji silaha za asili na mashada.

Mzee Nyambita Pima Fares Nyakutonya mwenye umri wa miaka 83 ambaye ni shuhuda wa vita ya pili ya dunia ameielezea siku hii ya mashujaa na wito wake kwa watanzania. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)

Mzee Nyambita Pima Fares Nyakutonya akizungumza na waandishi wa habari.
Kumbukumbu ya Mashujaa huadhimishwa kila mwaka Julai 25, ambapo mashujaa waliopigana vita katika kuikomboa nchi kutoka katika utawala wa wakoloni au kuikomboa nchi yao na wavamizi kama Nduli Idd Amini.

Pamoja na tukio hili la maadhimisho, tayari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka utaratibu kuwaenzi pia wale walio hai kwa kuwagharamia huduma mbalimbali za kila siku ikiwa ni pamoja na kuwatunza ipasavyo.

SCOTLAND RATIBA YA MABONDIA TIMU YA TANZANIA.

Patron CP Suleiman Kova
President:   -Mutta  Robert Lwakatale
Vice president:  Lukelo A. Willilo
Secretary General:  Makore .R.Mashaga
Tresurer: Maj.Kapandantava
Mob: +255 774 555 800
          +255 713 588 818
P.O.BOX 15558
TELL: +255 22 2850545
FAX:   +255 22 2850546
E-mail: bft.tanzania2009@gmail.com
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Affiliated to AIBA,AFBC&NSC
BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA

                                                                                                        Thursday, July 24, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
                                                 
Yah:- RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA WANAOWAKILISHA TAIFA
               KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA SCOTLAND (NDONDI).

Hatimaye ratiba ya mchezo wa ngumi kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola imetolewa leo tarehe 24/07/14 baada ya zoezi la kupima uzito na afya lililofanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 4.00 Asubuhi kwa saa za Scotland, kwa mabondia na waamuzi wote wanaotegemea kushiriki mashindano hayo`1.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mashindanoo yataanza  tarehe 25/07/14 na yatamalizika tarehe 02/08/14.katika ukumbi wa Secc (Hall 4A) na inaonyesha kuwa captain wa timu ya Tanzania Selemani kidunda ndiye atayeanza kupeperusha bendera ya taifa na hatiaye kufatiwa na mabondia wengine kama ifuatavyo:-

Tarehe 25/07/14 saa 1.45 Jioni  (69) kg
        Kehinde Ademuyiyiwa (Nigeria) v/s Selemani Kidunda (Tanzania)

Tarehe 26/07/14 saa 7.20 Mchana (60) kg
                    Jessie Lartey (Ghana) v/s Nasser Maffuru ( Tanzania)
                                      Saa 1.00 Jioni (64) kg
        Stevin Thanki (Malawi) v/s Fabian Gaudensi (Tanzania)

Tarehe 27/07/14 saa 12.45 Jioni( 52) kg
                         Bye                                   v/s Ezra Paul ( Tanzania)
                                               Saa 1.40 Jioni (8I)kg
                     Mohamed Hakimu (Tanzania) v/s Sumit Sangwan (India)

        Tarehe 28/07/14 saa 7.25 Mchana) (56)kg
        Bashiri Nasir (Uganda) v/s Emilian Patrick (Tanzania)
                                               Saa 1.35 jioni (49) kg
                  Paddy Barnes( Northern Ireland) v/s Hamed Furahisha (Tanzania)

Taarifa hizi zimeletwa na

Makore mashaga
KATIBU MKUU.

Thursday, July 24, 2014

BREAKING NEWS: FIESTA 2014 KUANZIA MWANZA.


FIESTA 2014 si hii hapa...Ratiba imesha tangazwa rasmi ambapo kwa mara nyingine tena Tarehe 09 August mzigo utapigwa MWANZA. Akizungumza kupitia Clouds Fm hii leo ile mida ya XXL na B. Dozen, Mwenyekiti wa kamati ya Fiesta 2014 Sebastian Maganga amesema kuwa baada ya mikikimikiki ya shughuli mbalimbali za utafutaji na uwajibikaji kwa watanzania basi hawana budi kukutana mahali pamoja penye hadhi na service zote za uhakika kwaajili ya kupata michongo mipya huku wakitoa stress kwa kula burudani.

Mkoa wa Mwanza umepata 'shavu' kukabidhiwa funguo za burudani ya Serengeti FIESTA kwa mwaka 2014 ambapo Tarehe 09 August mzigo utapigwa pale pale palipo vunjika shoka mpini ukabakia, penye dimba lenye historia ya kuvunja rekodi ya mahudhurio CCM Kirumba MWANZA.

Maganga amesema kuwa baada ya hapo FIESTA 2014 itajisogeza ikiwa ni kwa mara ya kwanza August 15 katika mji wa BUKOBA mkoani Kagera, kisha KAHAMA 17 August nao kwa mara ya kwanza watashuhudia hizoooo shamra shamra.

Mzigo utaenda kupigwa MUSOMA 22 August, halafu vuuum SHINYANGA hii hapa tarehe 24 August. "Nafurahi kuona Shinyanga peke yake ndiyo imepewa nafasi 2 so kama utakosa Shy Town tunakutana Kahama lakini fanya tukutane zote 2 tu.... Au siyo....'Ni sheeedah!!" alisema Mwenyekiti wa kamati ya FIESTA 2014, Sebastian Maganga. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA. 

MKUTANO WA PILI WA USHIRIKIANO WA TANAPA NA JESHI LA POLISI KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU UNAOLENGA MALIASILI WAFANYIKA MOROGORO HII LEO.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa .
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, (TANAPA) Allan Kijazi akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya  Mashirikiano kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa inayopakana na Hifadhi za Taifa. Mkutano unaofanyika katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa .
Baadhi ya washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alipokuwa akifungua warsha hiyo.
Sekretarieti.
Baadhi ya washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia masuala muhimu ndani ya warsha hiyo.
Meneja Mawasiliano, TANAPA Pascal Shelutete akitoa mada ya Utaratibu wa kutoa Taarifa kwa Umma juu ya masuala ya Ulinzi na Usalama wa Maliasili na Watalii.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 45 WA CPA JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch Sephir Motanyane,   wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC jijini Arusha baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Azan Zungu, wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la kimasai wakati walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha kufungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Picha na OMR

MV. KIGAMBONI KUSITISHA HUDUMA KWA MUDA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI
WAKALA WA UFUNDI NA UMEME(TEMESA)

Telegrams TEMESA DSM        S.L.P  70704
Simu: +255-22-2862796/97                                                           DAR ES SALAAM
Fax:   +255-22-2865835                                                                TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ana watangazia wananchi wote kuwa kivuko cha MV. Kigamboni kinatarajiwa kwenda kwenye matengenezo makubwa wakati wowote kuanzia leo.
Hivyo huduma za uvushaji zitaendelea kwa kutumia vivuko vya MV. Magogoni pamoja na MV. Lami katika kipindi chote cha matengenezo husika.
Uongozi wa TEMESA unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu
TEMESA
          23/7/2014

Wednesday, July 23, 2014

NISSAN MARCH FOR SALE.

Nissan March,2002 Model,1300cc, Automatic transmission, Power windows, Power mirrors ,Retractable mirrors, Alloy Rims, Spoiler, Tinted windows, Rear wiper, Good sound  system, low mileage ..
Very clean car and fuel efficient. For only ksh325,000 o.n.o
Call 0723106130

KIBA SQUQRE - PITA MBELE.

Kiba Square566689510_n
Ally Kiba na Abdu Kiba ni ndugu wawili wanaounda kundi linaloitwa Kiba Square wamekuja na ngomayao mpya inaitwa 'Pita mbele' SIKILIZA KWA KUBOFYA PLAY.

1st DEATH ANNIVERSARY OF JOHN SHILATU.

The late John Shilatu.

It is exactly one year since you passed away, the way we miss you, and the way we remember you, the gap is clearly shown, we exactly know how much you meant to us. We still think about you everyday, we just love and miss you in our own special way.
Deeply missed by your Wife Bernadina; Your Children Benigna, Emmanuel, Geofrey, Gerald & Digna; your only grandson Jayden; Your Sisters Laura & Clara; Your Sisters inlaws, friends, neighbours, relatives and clans of Shilatu & Makere.
May GOD rest your soul in peace wherever you are. Deeply Missed John Shilatu.

CHAMA CHA BAISKELI CHASIMAMISHA WAJUMBE WAWILI KWA UTOVU WA NIDHAMU.

Katibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) John Machemba (kushoto) akitoa tamko la kuwasimamisha wajumbe wawili wa chama hicho ngazi ya Taifa kutoka mikoa ya Mwanza na Arusha baada ya kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikiwakabili. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Saimon Tungu (katikati) na Katibu msaidizi Fabian Bukanu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli mkoa wa Mwanza Salum King (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli mkoa wa Simiyu, Balele (kulia) walikuwa ni moja kati ya wahudhuriaji kusanyiko la tamko.
Taswira ya mkutano huo.
UONGOZI wa Chama cha Baiskeli nchini Tanzania (CHABATA) umeeleza kuwa uamuzi wa kikao cha Kamati ya Utekelezaji taifa kuwasimamisha Wajumbe wawili wa Chama hicho ngazi ya Taifa kutoka mikoa ya Arusha na Mwanza  kuwa ulizingatia taratibu na kanuni dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Katibu Mkuu wa CHABATA, John Machemba alieleza maamuzi yaliofikiwa na kikao hicho kilichofanyika hivi majuzi mkoani Shinyanga kuzungumzia mambo mbalimbali ya mchezo huo Kanda ya Ziwa na nchi kwa ujumla.

Machemba alisema kwamba, “Tulipowaita katika kikao baada ya kujadili tuhuma za viongozi hao wawili ili waje kujieleza kwa wajumbe juu ya tuhuma zao ilibainika kuwa tuhuma hizo niza ukweli baada ya wao kukubali baadhi ya tuhuma zao, hivyo kuamliwa kusimamishwa hadi kusubiri maamuzi ya mkutano mkuu taifa,”alisisitiza.

Katibu huyo aliwataja waliosimamishwa ni Moses Andrew (Arusha) na Lucas Bupilipili (Mwanza) ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo kufatia tuhuma zinazowakabili ambapo moja ya tuhuma hizo zimedaiwa ni Utovu wa nidhamu walioonyesha hivyo kusubilia majaliwa ya maamuzi ya mkutano mkuu utakaoketi badaye.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Saimon Jackson alieleza kuwa kikao cha kamati tendaji kiliwachagua Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Seleman Kova kuendelea kuwa mlezi wa chama hicho huku Mbunge wa zamani wa Shinyanga Leonarld Derefa akiteuliwa kuwa mshauri mkuu na wakili Shabani Masamaki pia kuwa mshauri wa Chama hicho.

Jackson aliweka bayana gharama za mashindano ya mbio za baiskeli zilizofanyika mkoani Shinyanga zilizotolewa na wadhamini Kampuni ya Barrick inayomiliki Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kilikuwa kiasi cha Sh. Milioni 97.5 na kukana kuwepo matumizi mabaya ya sehemu ya fedha hizo.

MEYA WA ILALA JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu. Picha Zote Na Dj Sek Blog

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar.
Mwonekano wa Bara barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.