|
Askari wa parade akimkabidhi mkuki na ngao mwakiliashi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kwaajili ya uwekaji wa silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza. |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, akiweka silaha za asili kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza. |
|
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe. Anthony Diallo, akisali mara baada ya kuweka silaha za asili za upinde na mshale, kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza |
|
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mr. Mkabenga, akiweka shoka kama ishara ya heshima kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza. |
|
Mwakilishi toka kanisa la Roman Catholic akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza |
|
Wawakilishi toka watu wa madhehebu ya Hindu Union wakiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza. |
|
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mama Joyce Masunga akiweka shada la maua kwenye mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa, maadhimisho yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza |
|
Wimbo wa Taifa ulipigwa. |
|
Wadau mbalimbali wamehudhuria katika maadhimisho haya muhimu. |
|
Wadau mbalimbali wamefika hapa ili kushiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa, yaliyofanyika leo asubuhi eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere jijini Mwanza. |
|
Eneo la tukio. |
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa ambayo kitaifa yamefanyika leo kote nchini, ambapo katika ngazi ya mkoa pia yamechukuwa nafasi mkoani Mwanza.
Ndani ya 88.1 maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la mviringo wa makutano ya barabara ya Kenyata, Makongoro na Nyerere, kwa Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa na wananchi kukusanyika katika eneo la kumbukumbu ya mnara wa mashujaa na kufanya ibada zikiwemo shughuli za uwekaji silaha za asili na mashada.
Mzee Nyambita Pima Fares Nyakutonya mwenye umri wa miaka 83 ambaye ni shuhuda wa vita ya pili ya dunia ameielezea siku hii ya mashujaa na wito wake kwa watanzania. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)
|
Mzee Nyambita Pima Fares Nyakutonya akizungumza na waandishi wa habari. |
Kumbukumbu ya Mashujaa huadhimishwa kila mwaka Julai 25, ambapo mashujaa waliopigana vita katika kuikomboa nchi kutoka katika utawala wa wakoloni au kuikomboa nchi yao na wavamizi kama Nduli Idd Amini.
Pamoja na tukio hili la maadhimisho, tayari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka utaratibu kuwaenzi pia wale walio hai kwa kuwagharamia huduma mbalimbali za kila siku ikiwa ni pamoja na kuwatunza ipasavyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.