ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 27, 2019

Thursday, September 26, 2019

VIDEO: MWILI WA NELSON MABEYO ULIVYOPOKEWA MWANZA - MAZISHI LEO ALHAMIS 26 SEPT 2019

 Hatimaye Mwili wa  rubani, marehemu Nelson Mabeyo umewasili jijini Mwanza tayari kuelekea kijiji cha Masanzakona wilayani Busega mkoani Simiyu kwaajili ya mazishi.

Nelson ambaye alikuwa rubani wa ndege ya Kampuni ya Auric air yenye namba 5H-AAM alipata ajali katika uwanja wa Serengeti akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi na wote kwa pamoja walifariki dunia papo hapo.


Miili ya wawili hao akiwamo wa rubani huyo ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ilihifadhiwa katika Zahanati ya Soronera kisha baadaye kusafirishwa hadi jijini Dar es salaam, ambapo jana Jumatano uliwasili jijini Mwanza na kuelekea kijiji cha Masanzakona wilayani Busega mkoani Simiyiu kwaajili ya mazishi yatakayofanyika leo Alhamisi ya tarehe 26 Septemba 2019.
Wednesday, September 25, 2019

SIKU YA 5 MAENDELEO YA UJENZI JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA


Hatua hii ni mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa mnamo tarehe 15 ya Mwezi July 2019, akiagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoa TShs 2.2 bilioni na Manispaa ya Ilemela kutoa TSh1.8 bilioni na kufanya jumla Sh4 bilioni kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

KUTANA NA HISENSE BIDHAA ZENYE WARRANTY MIAKA MITATU - ZATINGA KANDA YA ZIWA.


Bidhaa za HiSENSE tayari zimeshatinga nchini Tanzania na katika maonesho ya biashara ya madini yaliyofanyika mkoani Geita imepata kushiriki. Hii ni Kampuni iliyopata mafanikio barani Afrika kutokana na kutengeneza bidhaa zenye chapa yake yenyewe.

Katika miaka mitatu iliyopita tangu kampuni ya Hisense ambayo ni kampuni maarufu ya vyombo vya umeme nyumbani iingie kwenye soko la Misri mwishoni mwa mwaka 2006, chapa ya kampuni hiyo inajulikana zaidi, kiwango cha uuzaji wake wa bidhaa kimeongezeka zaidi, na thamani ya uuzaji iko kwenye nafasi tatu za mwanzo nchini humo. 

Athanas Mang'ati ni Meneja wa Kampuni ya HISENSE Kanda ya Ziwa anasema katika muda mfupi wananchi wameweza kuzielewa bidhaa za kampuni yake na kuzigombania sokoni kutokana na kuja zikiwa za kisasa zenye bei nafuu sanjari na wananchi kuugundua umadhubuti wake yaani ubora, uliokuja na mfumo wa kukidhi mahitaji halisi yanayolingana na hali ya mazingira ya watu wa hali ya juu na wa kipato cha nchini.

Pia mafanikio ya kampuni hiyo yanatokana na wazo la kampuni hiyo la kutengeneza bidhaa zenye chapa yake yenyewe.

Tuesday, September 24, 2019

BALOZI GETRUDE MONGELLA AFUNGUA TAMASHA LA 14 LA JINSIA 2019


Balozi Getrude Mongella ambaye ni Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 Beijing China amefungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 leo Jumanne Septemba 24,2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

MPC YATOA PONGEZI KWA UTEUZI WA ANTHONY SANGA.


Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza MPC inampongeza Mhandisi Anthony Sanga aliyekuwa Mkurugenzi wa MWAUWASA kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Sanga amekuwa mtendaji makini kwa muda wote aliokuwa Mkurugenzi wa MWAUWASA.

Moja ya maeneo aliyoyasimamia vizuri ni mahusiano na wadau mbalimbali Mkoa wa Mwanza.

Sisi kama MPC tumekuwa na uhusiano mzuri na Sanga kwa muda wote aliokuwa Mkurugenzi hapa MWAUWASA .

MPC inamtakia kila la heri katika utendaji wake kwa nafasi yake hiyo hiyo.

WANANCHI WASEMA LISSU ALIWACHELEWESHEA MAENDELEO WAMTAKA MBUNGE MTATURU KUIOMBA SERIKALI KUTEKELEZA MRADI YA MAENDELEO ILIYOSAULIKA JIMBONI HUMO

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki amebadili hali ya hewa ya Jimbo hilo ambapo mambo yamekuwa moto kila kona na kudiliki wananchi wanapomuona kumtuza zawadi za vitu mbalimbali ikiwemo mifugo ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono na kumupatia imani ya kushirikiana naye katika kufikia malengo ya maendeleo katika Jimbo hilo ambayo kwa miaka saba yaligubikwa na changamoto za kisiasa na kusaulika kutokana namtangulizi wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hiloTundu Lissu kabla ya kutengeliwa kwa na Spika Job Ndugai kwa kukiuka kanuni na taratibu za kuduhumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutofuatwa hali iliyopelekea hata Lissu katika uwakilishi wake kuwagawa wananchi huku akiwahamsisha kutoiunga mkono serikali na viongozi wake katika suala zima la kuhamasisha kuchangia miradi ya maendeleo na utekelezaji wake jambo lilisababisha sintofahamu katika utekelezaji wake.
 NA WANDISHI WETU, IKUNGI SINGIDA.

WANANCHI wa Jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida wamemwambia Mbunge mpya wa Jimbo hilo, Miraji Mtaturu kuwa walicheleweshwa kupata maendeleo kutokana na mtangulizi wake kuwa mwakilishi aliyeshindwa kuzisemea kero zao serikalini kwa kuwa alikuwa Mbunge wa kuhudhulia kesi Mahakamani na mapambano dhidi ya viongozi wa serikali jambo lililowanyima kuwa na mwakilishi aliyewa tambua shida zao.

Maneno hayo yalijitokeza jana katika Kata ya Siuyu Wilayani Ikungi kwenye  mkutano wa hadhala wa Mbunge mpya  Mtaturu aliyechukua nafasi baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu aliyetenguliwa uwakilishi wake na Spika Jobu Ndugai kwa mujibu wa Kanuni za kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambapo amekuwa akifanya mikutano kwa lengo la kuwashukuru wananchi  baada ya kuapishwa na kuhudhulia Kikao cha Bunge la kumi na sita Jijini Dodoma.

Mbunge Mtaturu amekuwa akishuhudia mamia ya watu wakihudhulia mikutano yake huku wakimuomba awasaidie kuzifikisha serikalini kero na matatizo mbalimbali ya Jimbo hilo ambayo kwa miaka tisa hazikupatiwa ufumbuzi wa haraka na kusababisha wananchi kupata shida ya kukosa huduma bora za kijamii ikiwemo majisafi, elimu, afya, umeme, barabara, kilimo, ufugaji na mawasiliano pia wakikosa kuhamasishwa kushirikiana na viongozi na wataalamu wa serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mtaturu ametoa fursa kwa wananchi kuchangamkia mradi wa kopa ng'ombe wa kisasa lipa ng'ombe ambapo ametangaza wananchi 20 wa kwanza watakaojenga mabanda watakopeshwa mitamba 20 iliyo tayari kuwa ambapo kila aliyekopa atarejesha ng'ombe mmoja baada ya kuzaa na kukopeshwa wananchi wengine huku pia wananchi hao wakielezwa kuwa watanufaika na mradi huo kuwa kuongeza kipato cha uchumi kwa kuuza maziwa hivyo amewataka kujiandaa na mradi huo ambapo kila mwaka atatoa ng'ombe 20 kutekeleza katika Kata zote.
"Nimewasikia mlivyokosa uwakilishi wa kufikisha changamoto na matatizo mbalimbali kutoka katika Kata na Jimbo kwa kuwa aliyenitangulia alitumia muda mwingi kwenye mashauri mahakamani, kuwa Mbunge wa Kitaifa wa Chama chake na kusahau kuwa mlimchagua ili mmutume kufikisha kero zenu na kupatiwa ufumbuzi na serikali, kwangu itakuwa tofauti nachowaomba wananchi nipeni ushirikiano tufanyekazi ya maendeleo na tuachane na chuki na kutofautiana kiitikadi kama milivyojengwa na wanasiasa," alisema.

Mtaturu aliwahakikiahia wananchi katika Kata ya Siuyu Tarafa ya Mngaa kuwa atakuwa Mbunge wa kuwatumikia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao vya siasa, dini na makabila kwa kuwa Jimbo na Wilaya hiyo iko nyuma kimaendeleo hivyo muda uliopo sasa ni kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ilikwama kutoka na kutosemewa Bungeni na serikalini ili kupatiwa majibu na ufumbuzi wa haraka.

"Wananchi muda haupo wa kuanza kujadili mambo ya siasa kilichopo ni kushirikiana na kuanza kutekeleza yale ambayo yametufikisha kuwa Wilaya ambayo ilisuasua kimaendeleo katika Mkoa wa Singida hivyo niwahakikishie barabara ya hii ya kutoka Ikungi, Makiyungu hadi kufikia Jimbo la Nchemba mkoani Dodoma yenye urefu wa km 400 tumepatiwa fedha hivyo Tarura wataitengeneza wakati wowote kuanzia sasa pia kuna kisima cha majisafi Kijiji cha Makotea kitakamilishwa tumepata Sh milioni 100 za utekelezaji wake," alisema.

Mbunge hiyo alisema katika utekelezaji wa kupatiwa umeme wa REA awamu ya pili tayari vijiji 75 vipo kwenye utekelezaji hivyo kuwa Kijiji umeme utawaka, ujenzi wa Hispitali ya Wilaya unaendelea serikali imetoa Sh bilioni 1.5 ujenzi umeanza pia serikali imeikubali kutupatia Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) Wilaya na mradi wa majisafi mkubwa wa kihistoria utakapoanza kujengwa utapitia Wilaya ya Ikungi kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma kwa sasa tumepewa Sh bilioni 2 za kukamilisha mradi wa majisafi visima 28.

Mtaturu aliwaeleza wananchi kuwa atahakikisha anaunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli za utolewaji elimu bila malipo ambapo atasaidia ada za wanafunzi 10 watakao faulu kuingia Kidato cha tano na sita kutoka katika familia zisizokuwa na uwezo kabisa lakini akijitolea kusaidia watoto 200 ambapo wazazi wao kutoka familia masikini watakofedha za kununulia sale za shule ambapo atanunua 100 kwa watoto wa shule ya msingi na 100 wa sekondari kwa kila mwaka atakapokuwa mwakilishi wao.

Monday, September 23, 2019

MBUNGE MTATURU AJA NA KAULI MBIU, MANENO KIDOGO, KAZI ZAIDI, HAPA KAZI TU! !!

 Mtaturu aliapishwa septemba 3 mwaka huu bungeni baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Tundu Lissu(CHADEMA)kupoteza ubunge kwa kutohudhuria vikao bila ya taarifa na kutojaza fomu za tamko la mali na madeni.
 Akizungumza katika mikutano aliyoifanya katika kijiji cha Mkiwa,Issuna na Ikungi Mtaturu akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
 “Katika utumishi wangu mimi ni kazi tu,na serikali yetu inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi CCM inawapenda na kuwajali sana,nitahakikisha tunashirikiana pamoja ili kusukuma mbele gurudumu letu la maendeleo,na katika hii nimekuja na kauli mbiu isemayo,Maneno kidogo,kazi zaidi,hapa kazi tu,”alisema Mtaturu.
 Ametumia mikutano hiyo kuweka bayana vipaumbele vyake atakavyovitekeleza katika kipindi cha ubunge wake kuwa ni elimu ambapo atahamasisha jamii kuunga mkono elimu bila malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia.
 “Jamii iliyoelimika ndio yenye uwezo wa kujiletea maendeleo, hata nilipokuwa mkuu wa wilaya nilifanyakazi hiyo, Sasa nitaendelea kuhamasisha jamii yetu kusomesha watoto,nitaunga mkono elimu bila malipo kwa kukabiliana na upungufu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, walimu na ujenzi wa mabweni ili kuokoa watoto wakike kutopata mimba wakiwa shuleni,
“Katika sekta ya elimu nitahakikisha pia kila mwaka nasaidia wanafunzi 200 ambao wazazi wao hawana uwezo kwa kuwanunulia sare za shule,hapa ni wanafunzi 100 wa shule za msingi na 100 wa sekondari,nitaomba watendaji wetu wanisaidie katika kuwatambua,nafanya hivi ili kumuunga mkono Rais wetu dk John Magufuli,”alisema Mtaturu.

Pia nitawalipia ada wanafunzi 10 waliofaulu kujiunga na kidato cha tano katika shule zetu za serikali,watano wa kike na watano wakiume, “hili nilishaanza nikiwa mkuu wa wilaya kuna mtoto alipata daraja la pili kachaguliwa kuendelea na masomo wazazi hawana uwezo,nikamsaidia kumlipia helana mahitaji yake yote karibu laki 7 sasa hivi yupo shule,”alisema mbunge huyo.

Vipaumbele vingine alivyotaja ni kwenye[i] sekta ya maji,afya,kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuhamasisha kilimo cha kisasa badala ya kile cha mazoea na kuanzisha mradi wa kukopesha wananchi ng’ombe wa maziwa utakaojulikana kama Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ambao watasambazwa kwenye tarafa mbili.

Ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dk Magufuli kwa kuwapelekea sh bil mbili za ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA)kama alivyoomba akiwa mkuu wa wilaya ya Ikungi.

MBUNGE WA KWIMBA AIMWAGIA SIFA SERIKALI BAADA YA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI

 Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor (CCM) (katikati) akinawa mikono wakati wa sherehe za kupokea mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji, Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kikubiji, Alfred Luteja.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor (CCM) (katikati) akinywa maji ya Mradi wa Kijiji cha Shilima wakati wa sherehe za kupokea mradi huo.
 Wananchi wa Shilima wakijipatia huduma ya maji kutoka kwenye mradi uliyozinduliwa hivi karibuni ambao unatoa maji kutoka Ziwa Victoria.  
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Shilima na vijiji vya jirani wakimsikiliza Mbunge wao Shanif Mansoor (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kuupokea mradi wa maji wa Shilima.

Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor (CCM) ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kukamilisha mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza.

Ametoa pongezi hizo jana alipojumuika na wapiga kura wake wa Kijiji cha Shilima kusherehekea kukamilika kwa mradi huo ambao ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013 lakini kutokana na udhaifu wa Mkandarasi haukuweza kukamilika kwa wakati.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni ya vitendo, ikiahidi inatimiza kwani ameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati na kuongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo ni kama ndoto ambayo wananchi wake wamekuwa hawana uhakika wa lini itatokea hasa ikizingatiwa kwamba kero ya maji kwa wananchi hao ilikuwa ni kubwa.

Akizungumzia historia ya mradi huo, Mhe. Mansoor alisema ulianza kutekelezwa mwaka 2013 lakini Mkandarasi alikua akisuasua na baada ya Waziri kufika kwenye eneo hilo alifanikisha kuvunja mkataba na kazi ya ujenzi wa mradi huo kukabidhiwa rasmi kwa MWAUWASA. "Namshukuru sana Profesa Mbarawa, alifika hapa na kujionea hali halisi na hatimaye alifanikiwa kusitisha mkataba na Mkandarasi na kukabidhi rasmi ujenzi wa mradi kwa MWAUWASA," alisema.

Mhe. Mansoor alitoa shukrani zake kwa Serikali kwa niaba ya wananchi wa Shilima ambapo alielezea adha waliyokuwa wakiipata kabla ya kukamilika kwa mradi huo, alisema shughuli nyingi za kimaendeleo zilisuasua kutokana na kukosekana huduma ya maji ya uhakika kwani wananchi walitumia muda mwingi kufuata maji umbali mrefu na hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu shughuli nyingine za maendeleo.

"Kwa niaba ya wananchi wa Shilima naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano, Waziri Mkuu alifika hapa na baadaye Waziri wa maji, waliahidi na wametimiza," alisema Mhe. Mansoor.

Kwa upande mwingine Mhe. Mansoor aliipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) chini ya aliyekuwa Mkurugenzi wake, Mhandisi Anthony Sanga ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati kama ilivyokuwa imeagizwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa. "Kwakweli MWAUWASA inafanya kazi kubwa na nzuri sana, kwa kipekee nampongeza sana Mhandisi Sanga kwa kuusimamia mradi huu kwa weledi mkubwa na sasa umekamilika," alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Kikubiji, Alfred Luteja aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Maji ambayo ilielekeza mradi huo ukamilishwe na MWAUWASA. "Serikali yetu ni sikivu, tumeieleza na imesikia na imefanyia kazi kilio chetu, hatimaye sasa tunatumia maji kutoka Ziwa Victoria," alisema Luteja.

Mradi wa Shilima ulizinduliwa rasmi na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa Septemba 14, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayoelekeza kuwapatia  huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 85 wakazi wote waishio vijijini ifikapo mwaka 2020.