ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 24, 2019

WANANCHI WASEMA LISSU ALIWACHELEWESHEA MAENDELEO WAMTAKA MBUNGE MTATURU KUIOMBA SERIKALI KUTEKELEZA MRADI YA MAENDELEO ILIYOSAULIKA JIMBONI HUMO

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki amebadili hali ya hewa ya Jimbo hilo ambapo mambo yamekuwa moto kila kona na kudiliki wananchi wanapomuona kumtuza zawadi za vitu mbalimbali ikiwemo mifugo ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono na kumupatia imani ya kushirikiana naye katika kufikia malengo ya maendeleo katika Jimbo hilo ambayo kwa miaka saba yaligubikwa na changamoto za kisiasa na kusaulika kutokana namtangulizi wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hiloTundu Lissu kabla ya kutengeliwa kwa na Spika Job Ndugai kwa kukiuka kanuni na taratibu za kuduhumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutofuatwa hali iliyopelekea hata Lissu katika uwakilishi wake kuwagawa wananchi huku akiwahamsisha kutoiunga mkono serikali na viongozi wake katika suala zima la kuhamasisha kuchangia miradi ya maendeleo na utekelezaji wake jambo lilisababisha sintofahamu katika utekelezaji wake.
 NA WANDISHI WETU, IKUNGI SINGIDA.

WANANCHI wa Jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida wamemwambia Mbunge mpya wa Jimbo hilo, Miraji Mtaturu kuwa walicheleweshwa kupata maendeleo kutokana na mtangulizi wake kuwa mwakilishi aliyeshindwa kuzisemea kero zao serikalini kwa kuwa alikuwa Mbunge wa kuhudhulia kesi Mahakamani na mapambano dhidi ya viongozi wa serikali jambo lililowanyima kuwa na mwakilishi aliyewa tambua shida zao.

Maneno hayo yalijitokeza jana katika Kata ya Siuyu Wilayani Ikungi kwenye  mkutano wa hadhala wa Mbunge mpya  Mtaturu aliyechukua nafasi baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu aliyetenguliwa uwakilishi wake na Spika Jobu Ndugai kwa mujibu wa Kanuni za kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambapo amekuwa akifanya mikutano kwa lengo la kuwashukuru wananchi  baada ya kuapishwa na kuhudhulia Kikao cha Bunge la kumi na sita Jijini Dodoma.

Mbunge Mtaturu amekuwa akishuhudia mamia ya watu wakihudhulia mikutano yake huku wakimuomba awasaidie kuzifikisha serikalini kero na matatizo mbalimbali ya Jimbo hilo ambayo kwa miaka tisa hazikupatiwa ufumbuzi wa haraka na kusababisha wananchi kupata shida ya kukosa huduma bora za kijamii ikiwemo majisafi, elimu, afya, umeme, barabara, kilimo, ufugaji na mawasiliano pia wakikosa kuhamasishwa kushirikiana na viongozi na wataalamu wa serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mtaturu ametoa fursa kwa wananchi kuchangamkia mradi wa kopa ng'ombe wa kisasa lipa ng'ombe ambapo ametangaza wananchi 20 wa kwanza watakaojenga mabanda watakopeshwa mitamba 20 iliyo tayari kuwa ambapo kila aliyekopa atarejesha ng'ombe mmoja baada ya kuzaa na kukopeshwa wananchi wengine huku pia wananchi hao wakielezwa kuwa watanufaika na mradi huo kuwa kuongeza kipato cha uchumi kwa kuuza maziwa hivyo amewataka kujiandaa na mradi huo ambapo kila mwaka atatoa ng'ombe 20 kutekeleza katika Kata zote.
"Nimewasikia mlivyokosa uwakilishi wa kufikisha changamoto na matatizo mbalimbali kutoka katika Kata na Jimbo kwa kuwa aliyenitangulia alitumia muda mwingi kwenye mashauri mahakamani, kuwa Mbunge wa Kitaifa wa Chama chake na kusahau kuwa mlimchagua ili mmutume kufikisha kero zenu na kupatiwa ufumbuzi na serikali, kwangu itakuwa tofauti nachowaomba wananchi nipeni ushirikiano tufanyekazi ya maendeleo na tuachane na chuki na kutofautiana kiitikadi kama milivyojengwa na wanasiasa," alisema.

Mtaturu aliwahakikiahia wananchi katika Kata ya Siuyu Tarafa ya Mngaa kuwa atakuwa Mbunge wa kuwatumikia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao vya siasa, dini na makabila kwa kuwa Jimbo na Wilaya hiyo iko nyuma kimaendeleo hivyo muda uliopo sasa ni kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ilikwama kutoka na kutosemewa Bungeni na serikalini ili kupatiwa majibu na ufumbuzi wa haraka.

"Wananchi muda haupo wa kuanza kujadili mambo ya siasa kilichopo ni kushirikiana na kuanza kutekeleza yale ambayo yametufikisha kuwa Wilaya ambayo ilisuasua kimaendeleo katika Mkoa wa Singida hivyo niwahakikishie barabara ya hii ya kutoka Ikungi, Makiyungu hadi kufikia Jimbo la Nchemba mkoani Dodoma yenye urefu wa km 400 tumepatiwa fedha hivyo Tarura wataitengeneza wakati wowote kuanzia sasa pia kuna kisima cha majisafi Kijiji cha Makotea kitakamilishwa tumepata Sh milioni 100 za utekelezaji wake," alisema.

Mbunge hiyo alisema katika utekelezaji wa kupatiwa umeme wa REA awamu ya pili tayari vijiji 75 vipo kwenye utekelezaji hivyo kuwa Kijiji umeme utawaka, ujenzi wa Hispitali ya Wilaya unaendelea serikali imetoa Sh bilioni 1.5 ujenzi umeanza pia serikali imeikubali kutupatia Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) Wilaya na mradi wa majisafi mkubwa wa kihistoria utakapoanza kujengwa utapitia Wilaya ya Ikungi kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma kwa sasa tumepewa Sh bilioni 2 za kukamilisha mradi wa majisafi visima 28.

Mtaturu aliwaeleza wananchi kuwa atahakikisha anaunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli za utolewaji elimu bila malipo ambapo atasaidia ada za wanafunzi 10 watakao faulu kuingia Kidato cha tano na sita kutoka katika familia zisizokuwa na uwezo kabisa lakini akijitolea kusaidia watoto 200 ambapo wazazi wao kutoka familia masikini watakofedha za kununulia sale za shule ambapo atanunua 100 kwa watoto wa shule ya msingi na 100 wa sekondari kwa kila mwaka atakapokuwa mwakilishi wao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.