Akizungumza katika mikutano aliyoifanya katika kijiji cha Mkiwa,Issuna na Ikungi Mtaturu akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
“Katika utumishi wangu mimi ni kazi tu,na serikali yetu inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi CCM inawapenda na kuwajali sana,nitahakikisha tunashirikiana pamoja ili kusukuma mbele gurudumu letu la maendeleo,na katika hii nimekuja na kauli mbiu isemayo,Maneno kidogo,kazi zaidi,hapa kazi tu,”alisema Mtaturu.
Ametumia mikutano hiyo kuweka bayana vipaumbele vyake atakavyovitekeleza katika kipindi cha ubunge wake kuwa ni elimu ambapo atahamasisha jamii kuunga mkono elimu bila malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia.
“Jamii iliyoelimika ndio yenye uwezo wa kujiletea maendeleo, hata nilipokuwa mkuu wa wilaya nilifanyakazi hiyo, Sasa nitaendelea kuhamasisha jamii yetu kusomesha watoto,nitaunga mkono elimu bila malipo kwa kukabiliana na upungufu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, walimu na ujenzi wa mabweni ili kuokoa watoto wakike kutopata mimba wakiwa shuleni,
“Katika sekta ya elimu nitahakikisha pia kila mwaka nasaidia wanafunzi 200 ambao wazazi wao hawana uwezo kwa kuwanunulia sare za shule,hapa ni wanafunzi 100 wa shule za msingi na 100 wa sekondari,nitaomba watendaji wetu wanisaidie katika kuwatambua,nafanya hivi ili kumuunga mkono Rais wetu dk John Magufuli,”alisema Mtaturu.
Pia nitawalipia ada wanafunzi 10 waliofaulu kujiunga na kidato cha tano katika shule zetu za serikali,watano wa kike na watano wakiume, “hili nilishaanza nikiwa mkuu wa wilaya kuna mtoto alipata daraja la pili kachaguliwa kuendelea na masomo wazazi hawana uwezo,nikamsaidia kumlipia helana mahitaji yake yote karibu laki 7 sasa hivi yupo shule,”alisema mbunge huyo.
Vipaumbele vingine alivyotaja ni kwenye[i] sekta ya maji,afya,kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuhamasisha kilimo cha kisasa badala ya kile cha mazoea na kuanzisha mradi wa kukopesha wananchi ng’ombe wa maziwa utakaojulikana kama Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ambao watasambazwa kwenye tarafa mbili.
Ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dk Magufuli kwa kuwapelekea sh bil mbili za ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA)kama alivyoomba akiwa mkuu wa wilaya ya Ikungi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.