ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 10, 2024

UWEPO WA MASHINE YA CT -SCAN KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA –BOMBO UMESAIDIA KUPUNGUZA RUFAA ZA WAGONJWA 900

 







Na Oscar Assenga,TANGA


SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu imejipambanua kwenye uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya kimkakati ikiwemo katika huduma za afya ambapo kuna maboresho makubwa yamefanyika na hivyo kuwezesha huduma kuendelea kuimarika kwenye maeneo.


Si tu katika Hospitali za Taifa na Kanda lakini pia Hospitali za Rufaa na wilaya ni miongoni mwa ambazo zimenufaika kupitia uwekezaji huo na hivyo kupunguza changamoto ambazo walikuwa wakikutana nazo wananchi awali kufuata baadhi ya huduma nyengine nje ya mikoa yao.


Miongoni mwa uwekezaji huo ni uwepo wa mashine za CT-Scan ambazo ni muhimu kwa kufanya uchunguzi kwa kutumia mionzi ambazo zinatumika kupima vipimo mbalimbali vya kichwa ,ubongo,kifua,tumbo pamoja na mshipa wa damu.


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa wanufaika wa uwekezaji huo ambapo kwa kiasi kikubwa umekuwa chachu na hivyo kuondoa changamoto ambazo walikuwa wanakumbana nazo wananchi hususani wa hali ya chini walikuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu.


Athumani Toba ni Mteknolojia wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga anasema uwekezaji huo uliofanywa na Serikali umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea wananchi adha kubwa waliokuwa wakikutana nayo kulazimika kusafiri nje ya mkoa huo kwa ajili ya kwenda kupata huduma hiyo.


Anasema kwamba uwepo wa CT Scan ambacho ni kifaa muhimu katika kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wakiwemo waliopata ajali za barabarani,wagonjwa walipata Shinikizo la damu, vipimo vya kifua ,kuangalia changamoto zilizopo kwenye vifua ikiwemo kufanya uchunguzi na kugundua magonjwa mbalimbali kwenye tumbo uvimbe,kansa na kugundua kansa kwenye utumbo na ubongo.


Toba anasema kitengo hicho kinamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na hivyo kusaidia kupunguza rufaa kwa wagonjwa kwenda kupata huduma hizo nje ya mkoa wa Tanga pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Frank Shega kwa kusimamia huduma hiyo ya CT Scan ambayo imewaondolea wananchi usumbufu wa kuifuata umbali mrefu.


Akielezea huduma hiyo ilivyoanza anasema ilianza mwezi February mwaka 2023 na mpaka sasa wamekwisha kutoa huduma kwa wagonjwa 900 ambao wangeweza kupewa rufaa kwenye hospitali mbalimbali za nje ya Tanga na hivyo uwepo wake umesaidia kupunguza gharama kwa wateja na usumbufu kwao.


“Kwa kweli tunaishukuru Serikali kwa hili kwani wagonjwa hao wangelezimika kupatiwa rufaa kwenda nje ya mkoa wa Tanga kupata huduma hizo hivyo tunapenda kuishukuru Serikali kwa uwekezaji huo ambao umesaidia kuondoa kero kwa wananchi wa mkoa wa tanga


Hata hivyo anasema kwa sasa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Bombo kupitia kitengo cha Mionzi,Idara ya Radiolojia inatoa huduma ya X-ray na Utrasound ambapo huduma za X-ray zinatolewa kuanzia za kawaida na zile maalumu hivyo hivyo kwa Utrou sound zinatolewa kuanzia zile za kawaida na maalumu na wanafanya ultrasound za wajawazito na magonjwa mbalimbali ya wakina mama na wanaume ikiwemo tezi dume.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU DKT JIM YONAZI AONGOZA KIKAO MAALUMU UENDELEZAJI WA MAKAO MAKUU DODOMA

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao maalum kilichohusu uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma, Kikao kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Dodoma, Tarehe 9 Februari, 2024.





MWENYEKITI WA CCM PWANI ATAO ONYO KWA VIONGOZI WANAOTUKANA MITANDAONI

 


VICTOR MASANGU,KIBAHA

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa  Pwani amewaonya vikali  baadhi ya wanachama  wa chama  na baadhi ya  wananchi wa mkoani Pwani  ambao wamekuwa na mazoea ya kuwatukana Viongozi wa Chama hicho kwenye mitandao ya kijamii kuacha mara moja.


Mlao ametoa onyo hilo Wilayani Kibaha wakati akizungumza na wananchi  pamoja na wana chama wa CCM   wakati wa ziara yake ya kawaida ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake katibu wa  chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Pwani Brnard Ghaty amewataka viongozi kuachana na tabia ya kutoa siri ya vikao mbali mbali ambavyo vinafanyika.

"Kuna baadhi ya watu tumeajiri lakini wamekuwa na changamoto ya kuamua kutoa siri za ndani ya vikao kwa kweli hii sio sahii kabisa kwa hiyo hii tabia tuachane nayo,"alifafanua Katibu. 


Kwa upande wake  Mwenyekiti wa UWT  Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu  aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka akieleza utekelezaji wa ilani


Naye Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka  amewahimiza viongozi kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatembelea wanachama.


Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma nyamka alisema kwamba utekelezaji wa ilani unaendelea kwa vitendo ikiwemo katika sekta ya afya elimu,maji pamoja na mambo mengine ya msingi.

"Kwa kweli utekelezaji wa ilani ya chama katika Wilaya yetu ya Kibaha kwa kweli unafanyika na ukiangalia miradi mbali mbali imetekelezwa hivyo ushahidi upo na siku zote mwenye macho aambiwi tazama,"alisema Nyamka.



Awali baadhi ya wana chama wa CCM na wananchi walieleza kero Mbalimbali zinazowakabili katika mitaa yao ikiwemo katika sekta ya miundombinu ya barabara,afya,maji pamoja na sekta ya elimu.

Wednesday, February 7, 2024

BRELA WAWEKA KAMBI YA SIKU 3 MWANZA WAKITOA HUDUMA BURE

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA