VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani amewaonya vikali baadhi ya wanachama wa chama na baadhi ya wananchi wa mkoani Pwani ambao wamekuwa na mazoea ya kuwatukana Viongozi wa Chama hicho kwenye mitandao ya kijamii kuacha mara moja.
Mlao ametoa onyo hilo Wilayani Kibaha wakati akizungumza na wananchi pamoja na wana chama wa CCM wakati wa ziara yake ya kawaida ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Brnard Ghaty amewataka viongozi kuachana na tabia ya kutoa siri ya vikao mbali mbali ambavyo vinafanyika.
"Kuna baadhi ya watu tumeajiri lakini wamekuwa na changamoto ya kuamua kutoa siri za ndani ya vikao kwa kweli hii sio sahii kabisa kwa hiyo hii tabia tuachane nayo,"alifafanua Katibu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka akieleza utekelezaji wa ilani
Naye Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amewahimiza viongozi kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatembelea wanachama.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma nyamka alisema kwamba utekelezaji wa ilani unaendelea kwa vitendo ikiwemo katika sekta ya afya elimu,maji pamoja na mambo mengine ya msingi.
"Kwa kweli utekelezaji wa ilani ya chama katika Wilaya yetu ya Kibaha kwa kweli unafanyika na ukiangalia miradi mbali mbali imetekelezwa hivyo ushahidi upo na siku zote mwenye macho aambiwi tazama,"alisema Nyamka.
Awali baadhi ya wana chama wa CCM na wananchi walieleza kero Mbalimbali zinazowakabili katika mitaa yao ikiwemo katika sekta ya miundombinu ya barabara,afya,maji pamoja na sekta ya elimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.