ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 10, 2016

RAIS WA GAMBIA AKATAA MATOKEO BAADA YA KIONGOZI WA UPINZANI KUSHINDA URAIS.

Rais wa Gambia akataa kukubali matokeo ya uchaguzi alioshindwa na upinzani.


Mtu aliyechaguliwa juma lililopita kuwa rais mpya wa Gambia amesema kuwa rais wa sasa, Yanya Jammeh, amevuruga sifa ya taifa hilo kidemokrasia kwa kukataa kukubali kushindwa katika uchaguzi.

Kundi la kusimamia shughuli za kuandaa kukabidhiana madaraka limesema kuwa rais Mteule, Adama Barrow, na wafanyakazi wake wako salama, baada ya Rais Jammeh, kubadilisha msimamo wake kuwa hakushindwa uchaguzi.

Rais Jammeh alisema kuwa kura zilihesabiwa vibaya na akatoa wito kuwa uchaguzi urudiwe.

Msemaji wa serikali alisema kuwa mkuu wa majeshi nchini anamuunga mkono Bw Barrow.

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Banjul, umetoa wito kwa wanajeshi kuheshimu matakwa ya watu wa Gambia.

Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wameweka mifuko ya changarawe katika maeneo mbalimbali jijini kama vizuizi.

Serikali katika taifa jirani la Senegal imetoa wito kwa rais Jammeh kukabidhi madaraka kwa mshindi kwa njia ya amani.

Kukubali kushindwa kwa awali kwa rais Jameh kuliwapa matumaini raia walioona kama mwisho wa utawala wa kimabavu wa zaidi ya miongo miwili ulikuwa umekamilika.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA ALHAJI DANGOTE.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda. 

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje. 

Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini. 

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida. 

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA MHE LUHAGA MPINA Zanzibar.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo ya utendaji wa Tume hiyo wakati akiwasilisha Ripoti ya Utafiti iliofanywa na Tume hiyo wakati wa ziara ya Mhe Luhaga, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Tume hiyo maruhubi Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akipitia Ripoti ya Tume ya Sayansi na Teknolijia Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume hiyo ilioko Zanzibar.
Mratibu wa Kituo cha Tume Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina alipofika katika Kituo hicho maruhubi Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizunhgumza na waandishi wa habari Zanzibar baada ya kumalizia mazungumzo yake na kupoata taarifa ya Utendaji wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar katika ofisi zake ziliko maruhubi Zanzibar.  
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muunganio na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwasili katika viwanja vya Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar kutembelea kituo hicho kujionea shughuli zinazofanywa katika kazi za Utafiti wa Zao la Kilimo Zanzibar. 
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar Ndg Khatib Juma akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina alipofika Kituoni hapo kutembelea na kujionea shughuli za utafiti zinazofanya na Kituo hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa katika ziara yake Zanzibar.
Mratibu wa Tume ya Sayansi na Teknolijia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake na wafanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar kutembelea Miradi inayofadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina akitembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa na Mkuu wa Kituo hicho Ndg.Khatib Juma. 
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar Ndg Khatib Juma akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakiwa katika maabara ya kituo hicho kizimbani Zanzibar wakati wa ziara yake. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiangalia mpunga unaofanyiwa utafiti katika Kituyo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo hicho Ndg Juma Khatib katikati.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitoka katika Jengo la Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ilinayodhaminiwa na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Tanzania katika utafiti wake.

Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.< /b>
othmanmaulid@gmail.com
Zanzinews.com </ span>
0715 424152.or 0777424152.
Zanzibar. 

Friday, December 9, 2016

RAIS ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5678

Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Rais Dkt Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 5000; 

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI SEKTA YA USAFIRI WA ANGA.

Rais John Magufuli akizungumzia serikali ya awamu ya tano inavyokusudia kuliboresha shirika la ndege la ATCL miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika; 

Thursday, December 8, 2016

VILABU VILIVYOTINGA HATUA YA MTOANO KLABU BINGWA.

Jumla ya timu kumi na sita zimefuzu kwa hatua ya kumi na sita bora ya michuano ya klabu bingwa ulaya, huku timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika kila kundi zitaenda kushiriki michuano ya Europa ligi.

Droo ya kupanga raundi ya mtoano ya timu kumi na sita itapangwa siku ya jumatatu Decemba 12.Timu zilizofuzu kutoa kundi A ni Arsenal wakiwa vinara wa kundi na pili nafasi ya pili wako Psg, Kundi B vimefuzu timu za Napoli na Benfica.

Kundi C wamefuzu vigogo Barcelona na Manchester City huku kundi D kukiwa na Atletico Madrid na Bayern Munich.Kutoka kundi E zimefuzu Monaco na Bayer Leverkusen, na kundi F wamefuzu Borussia Dortmund na Real Madrid.

Leicester na Porto wamefuzu kutoa kundi G huku Juventus na Sevilla wakiwa wamefuzu katika kundi la mwisho kundi H

CHADEMA WATAKA MKAPA ANYANG'ANYWE SHAMBA KAMA SUMAYE.

MEYA wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu sasa.

Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze kufanyiwa shughuli nyingine.

Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.

Meya huyo amesema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa.

MAGUFULI AMUONDOA MAFURU HAZINA AIPANGUA TENA CCM, AJIRA 70,000 SERIKALINI ZAANIKWA, 6 WAOKOTWA MTONI NDANI YA VIROBA.


Magufuli amuondoa Mafuru hazina aipangua tena CCM, Ajira 70000 serikalini zaanikwa, 6 waokotwa mtoni ndani ya viroba. 

CHADEMA wataka Mkapa apokwe shamba kama Sumaye, Machinga sasa warejea kila kona, Maalim Seif aja na kituko kingine. Pata kwa undani dondoo hizi hapa; 

MTOTO AFANYIWA UKATILI.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOFUATA KWANI ZINATISHA NA KUSIKITISHA ILA ZIMEWEKWA HAPA KWAAJILI YA KUONESHA UKATILI ULIOFANYIKA. @gsengo
  ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

MTU mmoja aliefahamika kwa jina la Rhoda Juma (30) Mkazi wa Kijiji cha Kilabela Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumfanyia Ukatili Mtoto mdogo wa kike wa mwaka mmoja.

Tukio hilo limetokea Disemba 6,mwaka huu saa nane mchana kijijini humo ambapo mama huyo alimfungia ndani ya Nyumba mtoto huyo kwa muda wa miezi minne na kumshambulia sehemu zake za mwili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Naibu Kamishina wa  Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa mwanamke huyo alikuwa akiishi na mtoto huyo Nyumbani kwake baada ya kuletewa na rafiki yake ajulikanae kwa jina moja la Rahel (Recho) ambaye inadaiwa kuwa ndiye mama mzazi wa mtoto huyo.

Amesema inadaiwa kuwa  mama mzazi wa mtoto huyo alimuacha mwanaye Julai mwaka huu na kwenda  kusikojulikana katika shughuli zake za huduma ya baa

“Kwa kipindi chote cha miezi minne mtoto alikuwa akifungiwa ndani na kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake na Rhoda Juma ambaye ni mama alieachiwa mtoto hali iliyopelekea mtoto kuwa na makovu na kudhoofika mkiafya”amesema Msangi.

Aidha Mtuhumiwa amekatwa na atafikishwa  mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake na kwamba mtoto amelazwa hospitali ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hata hivyo Kamanda Msangi amewataka wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuacha vitendo vya ukatili  kwa watoto au watu wazima kwani ni kosa la jinai na kwamba kwa yeyote atakaye bainika atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

SudiBoy - Kidonda [Official Video]


Published on Dec 7, 2016
The Visuals are based on a True Story.
Audio was done by P_Lion
Video by _ One Montage Films.

RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU KIFO CHA MCHEZAJI MBAO FC.

1.jpegRipoti iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Thoma Rutta na kusomwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi inaeleza kuwa kusimama kwa moyo ghafla ndio chanzo cha kifo chipukizi wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Khalfan Mrisho.

Taarifa hiyo ilitolewa na kamanda huyo alipokuwa akizungumza kuelezea chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea Jumapili wakati wa mchezo wa Mbao FC dhidi ya Mwadui FC ikiwa ni ligi ya vijana katika uwaja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Daktari ametoa taarifa ya uchunguzi na kusema chanzo ni kusimama kwa moyo ghafla. Marehemu hakuwa na jeraha lolote, alisema Kamanda Ollomi.

Ismail Mrisho alizaliwa Mei 22, 1997 akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia yao. Amesoma Shule ya Msingi Nyakabungo kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Mwana 2013 alijiunga na Sekondari ya Mwanza ambapo alihitimu mwaka 2016. Ismail alikuwa amepata ufadhili wa kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Louisiana State nchini Marekani kuanzia mwakani.

Ismail lifikwa na mauti muda mfupi baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui, alipojaribu kusimama baada ya hapo alianguka tena ndipo alipokimbizwa hospitali mjini Bukoba lakini akafariki. 

Kabla ya kukumbwa na mauti hayo, aliifungia timu yake ya Mbao goli la kuongoza ambapo mchezo ulimalizika kwa Mbao kupata ushindi wa 2-0. 

Wednesday, December 7, 2016

MAMA AFANYA UNYAMA KWA MWANAYE.

 TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOFUATA KWANI ZINATISHA NA KUSIKITISHA ILA ZIMEWEKWA HAPA KWAAJILI YA KUONESHA UKATILI ULIOFANYIKA. @gsengo

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 7.12.2016


·         MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI MTOTO MDOGO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MIWILI WILAYANI SENGEREMA.

KWAMBA TAREHE 6.12.2016 MAJIRA YA SAA 14:00 KATIKA KIJIJI CHA KILABELA KATA YA NYATUKULA WILAYA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULINA KWA JINA LA RHODA JUMA MIAKA 30, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA KILABELA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI WA KUMFUNGIA NDANI YA NYUMBA KWA MUDA WA MIEZI MINNE NA KUMSHAMBULIA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE MTOTO MDOGO WA KIKE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU AITWAYE JULIANA KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MWANAMKE TAJWA HAPO JUU ALIKUWA AKIISHI NA MTOTO HUYO HAPO NYUMBANI KWAKE BAADA YA KULETEWA NA RAFIKI YAKE ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA RAHEL (RECHO) AMBAYE INADAIWA NDIO MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO, AIDHA INASEMEKANA REHEL (RECHO) ALIMUACHA MTOTO HAPO KWA RAFIKI YAKE MWEZI  JULAI 2016, NA KWENDA KUSIKO JULIKANA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA UHUDUMU WA BAA.

AIDHA INADAIWA KUWA KWA KIPINDI CHOTE CHA MIEZI MINNE MTOTO ALIKUWA AKIFUNGIWA NDANI NA KUSHAMBULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA RHODA JUMA AMBAYE NI MAMA ALIYEACHIWA MTOTO, HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUWA NA MAKOVU MENGI MWILINI NA KUDHOOFIKA KIAFYA, WATU MAJIRANI WALIMUONA MTOTO HUYO WAKATI MAMA MWENYE KAYA ALIPOKWENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE NA KUACHA MLANGO WAZI NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI NA KUSAIDIA MTUHUMIWA KUKAMATWA.

MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TAYARI AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO TAREHE 7.12.2016, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE, MTOTO AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA SENGEREMA AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA KUTENDA UKATILI WA AINA YEYOTE ILE KWA WATOTO AU WATU WAZIMA KWANI NI KOSA LA JINAI, ENDAPO IKIBAINIKA MTU ANATENDA UKATILI ATAKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, HIVYO ANAWASIHI WANANCHI WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI TUWEZE KUDHIBITI UKATILI KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

TAASISI YA AFRICAN RELIEF YAANZISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHUMBI.

Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Ndauka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mradi huo
 Vibarua akifyaka vichaka kusafisha shamba hilo
 Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) wakisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Samy  Mohammed Elazeb akisimamia maandalizi ya shamba hilo
 Ndauka na Samy  Mohammed Elazeb wakijadiliana jambo
 Mratibu wa Mradi huo, Peter Ambilikile (kushoto) akifafanua jambo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Samy  Mohammed Elazeb (kushoto),  na mwanakijiji wakiziba maji kwenye mabomba ya kisima kilitolewa msaada na taasisi hiyo kwa Kijiji cha Chumbi C

 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chumbi C, akikinga maji kwa mkono katika kisima hicho
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko, akionesha ukumbi wa Kijiji ambao umejengwa kwa msaada wa Taasisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akionesha jengo la ofisi za kijiji hicho, lililojengwa kwa msaada wa taasisi hiyo.
 Nyumba anayoishi Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho