TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA
HABARI LEO TAREHE 7.12.2016
·
MTU
MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI MTOTO
MDOGO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MIWILI WILAYANI SENGEREMA.
KWAMBA TAREHE 6.12.2016
MAJIRA YA SAA 14:00 KATIKA KIJIJI CHA KILABELA KATA YA NYATUKULA WILAYA
SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULINA KWA JINA LA RHODA JUMA
MIAKA 30, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA KILABELA, ANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI WA KUMFUNGIA NDANI YA NYUMBA KWA MUDA
WA MIEZI MINNE NA KUMSHAMBULIA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE MTOTO MDOGO WA
KIKE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU AITWAYE JULIANA KITENDO AMBACHO NI KOSA
LA JINAI.
INADAIWA KUWA MWANAMKE
TAJWA HAPO JUU ALIKUWA AKIISHI NA MTOTO HUYO HAPO NYUMBANI KWAKE BAADA YA
KULETEWA NA RAFIKI YAKE ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA RAHEL (RECHO) AMBAYE INADAIWA
NDIO MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO, AIDHA INASEMEKANA REHEL (RECHO) ALIMUACHA MTOTO
HAPO KWA RAFIKI YAKE MWEZI JULAI 2016, NA
KWENDA KUSIKO JULIKANA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA UHUDUMU WA BAA.
AIDHA INADAIWA KUWA KWA
KIPINDI CHOTE CHA MIEZI MINNE MTOTO ALIKUWA AKIFUNGIWA NDANI NA KUSHAMBULIWA
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA RHODA JUMA AMBAYE NI MAMA ALIYEACHIWA MTOTO,
HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUWA NA MAKOVU MENGI MWILINI NA KUDHOOFIKA KIAFYA, WATU
MAJIRANI WALIMUONA MTOTO HUYO WAKATI MAMA MWENYE KAYA ALIPOKWENDA KWENYE
SHUGHULI ZAKE NA KUACHA MLANGO WAZI NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI NA KUSAIDIA
MTUHUMIWA KUKAMATWA.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA
TAYARI AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO TAREHE 7.12.2016, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA
ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE, MTOTO AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA SENGEREMA
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI
NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA KUTENDA UKATILI WA AINA YEYOTE ILE KWA
WATOTO AU WATU WAZIMA KWANI NI KOSA LA JINAI, ENDAPO IKIBAINIKA MTU ANATENDA
UKATILI ATAKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, HIVYO ANAWASIHI
WANANCHI WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI TUWEZE KUDHIBITI UKATILI
KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.