ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 12, 2009

ZE RETURN OF MACHINGAZ


KATIKA KIPINDI HIKI TUNAPOELEKEA 2010 BAADHI YA SHERIA KAMA ZIMELEGEZWA VILE... SASA HIVI MGAMBO AKIKUKAMATA ETI HACHUKUI MZIGO WAKO BALI ANAKUELEKEZA SEHEMU UNAPOPASWA KUFANZA BIASHARA AU PENGINE ANAKUPA HI KISHA ANASEPA. HEHEHEIYA! PICHANI NI KANDOKANDO MWA BARABARA YA UWANJA WA SHEIK AMRI ABEID ARUSHA.

KAHAMA KUMEKUCHAEH BANA KUNA BONGE LA CLUB LINAFUNGULIWA EID MOSI HAPA MUJI YA DHAHABU (KAHAMA) CLUB INAITWA KAHAMA SOCIAL CLUB PANA VIEW YA HATARI KAUNTA ZAKITALII, DISCO LA NGUVU, MAKULAJI, MAVINYWAJI NA MAKILA KINGA FRENGWA. MB DOG ATASABABISHA MVUA YA MAUA MEKUNDU KWA MASONGI YA MALAVIDAVI, JAFARAH ATAKAMUA HIP HOP, UNAAMBIWA ABIRIA CHUNGA MZIGO KWANI- BONGO DAR ES SALAAM DUDE NAYE NDANI(ataiba kweli? maana kuna ulinzi wa baunsaz na screen). MAJD WAPYA WA VSS KUTAMBULISHWA. DJ SELE NA DJ SUMMER. DUNIA IMEZALIWA"

Friday, September 11, 2009

FLASH BACK PICTURE WIKI HII


KILA IJUMAA KUTANA NA FLASH BACK PICTURE WIKI HII NI PICHA YA MIAKA YA ZAMANI SANA AU ZAMANI YA KARIBU KATIKA UKURASA WA BLOG YAKO UIPENDAYO. MOIZ HUSEIN DOSAJ TOKA ARUSHA OMBI LAKO NIMELITIMIZA. PICHANI ALEX AKISNEP NA UNIQUE SISTERS NDANI YA FIESTA YA KWANZA ARUSHA SIKUMBUKI MWAKA. KAMA VIPI NTUMIE YAKO

KIITCHEN PARTY


SIKU HIZI KUNA MAUBUNIFU KTK UPAMBAJI, KWA UPAMBAJI WA AINA ZOTE MAMA RINGO IS THE BEST. "FASTA CHUKUA PICHA KISHA YABAADAYE HAYAHUUU!"

Thursday, September 10, 2009

QSS KIKAZI ZAIDI

EH BANA MDAFADA HUYU UNAYE MDEKSHIA ANAITWA SALMA NI BONGE LA EDITOR WA STILL PICTURE NA ANACHEZA NA GRAPHICS ILE LAANA ANAPATIKANA NYERERE ROAD QSS PHOTO STUDIO.

"COFUSION IN ROCK CITY" OF COZ in rock city.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MH. ABBAS KANDORO AKIZINDUA FILAMU YA CONFUSION IN ROCK CITY. UZINDUZI ULIOFANYIKA NYUMBANI HOTELS AND RESORTS NSSF JIJINI MWANZA. SHUKURANI KWA WADHAMINI AIR TANZANIA, NYUMBANI HOTEL, STONE CLUB, MH. L. MASHA, NAWE MWANAMWANZA.

MUHESHIMIWA IN DA HOUSE

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MBUNGE WA WILAYA YENYE KASI KTK MAENDELEO (SENGEREMA) MH. WILLIAM NGELEJA (mwenye t.shirt nyeupe) AKISHOW LOVE NA WADAU WA FILAMU YA CONFUSION YENYE WASHIRIKI WENYE MAJINA MAKUBWA NCHINI KAMA GADNA G. HABASH, SALAMA JABIR, MAUNDA ZORO NA WENGINE KIBAO.
FILAMU INA MAZINGIRA YA MIJI MIWILI MIKUBWA HAPA NCHINI DAR ES SALAAM NA MWANZA ILE HALI MWANZA IKICHUKUA ASILIMIA KUBWA KTK MATUKIO YA PICHA, MAZINGIRA NA WAIGIZAJI.

MWANZA NI WA KWANZA

NI WAKATI WA UTAMBULISHO:- KULIA (aliye nyoosha mkono) BW. RUGE MUTAHABA MBELE YA WANA MWANZA WENYE BAHATI KUALIKWA KUWA MASHUHUDA WA KWANZA WA MWONEKANO WA KWANZA WA FILAMU YA KWANZA YENYE UBORA LEVER ZA JUU KUREKODIWA MWANZA "COFUSION IN ROCK CITY" KUSHOTO NI DIRECTOR WA FILAMU MISS. KEMMY MUTAHABA SAMBAMBA NAYE PRODUCER SUMMER KATIKATI. SI MUDA MREFU ITAINGIA SOKONI....

Wednesday, September 9, 2009

SUPRISE!!

BINGWA WA SASA WA DUNIA MFUKUZA UPEPO MWANADADA CESTER SEMANYA TOKA SOUTH AFRICA ALIYEZUA GUMZO WIKI ZA HIVI KARIBUNI JUU YA JINSIA YAKE KUTOKANA NA MWONEKANO WAKE AMETOKEA KTK COVER LA YOU MAGAZINE LA AFRIKA KUSINI AKIWA AMEREMBESHWA NA WATAALAMU WA MAVAZI NA SURA KUWAZIMA WACHIMVI WALIOKUWA WAKICHONGA KUWA ETI MWANADADA HUYO NI MWANAUME. ZOEZI LILICHUKUWA WIKI NZIMA LIMEKAMILISHWA KWA SUPRISE YA MWONEKANO WAKE GAZETINI. WAKWARE WATAMIMINIKAJE?!

NYINGINE KTK STAGE

UNAMTAMBUA ZAIDI KWA JINA STL. JINA LAKE LA UBATIZO ANAITWA STELA NYAMBUI MWANGI NI MDAFADA TOKA NCHINI KENYA ANAYEPASUA ANGA LA MUZIKI NA MA AUDIO NA MAVIDEO FULL QUALITY OVA MAMTONI UMEIONA SHE GOT IT? MARA NYINGI INARUKA CHANEL O NA MTV AFRICA ICHEKISHIE.

HOTEL TILAPIA MWANZA


IKO UFUKWENI MWA ZIWA VICTORIA, ENEO LITAKALO KURUHUSU KUSHUHUDIA KWA MBALI BILA BUGUDHA SHUGHULI MBALIMBALI ZA UVUVI NA SAFARI ZOTE ZA KUELEKEA KISIWA CHA UTALII SAA NANE. EH BANA EEEH KAMA NI POZ LA MTOKO, KUOSHA AKILI ILI KUONDOSHA TAKATAKA ZA MAWAZO YAUMIZAYO AU PENGINE HONEY MOON TILAPIA NI ENEO MUAFAKA, PICHA YA KWANZA NILIPIGA ENEO LA TILAPIA NIKIWA MTUMBWINI YA PILI "USIDHANI MELI MJOMBA" NI MOJA YA VYUMBA KWA AJILI YAKO! TENA PRESIDENTIAL. SAMAKI CHOMA ,SAMAKI BANIKA TENA RUKSA KUVUA MWENYEWE HAPA NDIYO KAYA.

KAA TAYARI KWA MWONEKANO MPYA WA BLOG YAKO


JE UMEZIMIKA AU PENGINE UME FALL IN LOVE NA HII BLOG? HUTAKI KUACHA KUIDEKSHIA KILA DAY!! KAMA NDIYO - "WEITER!! MWONGEZE"!! TATIZO NI JE UNAUBAVU??Tuesday, September 8, 2009

MILA NA JICHO LANGU.HIVI MAJUZI MABINTI WA SWAZILAND ZAIDI YA ELFU KUMI WAKIWA NA MAVAZI YAO ASILI AMBAYO HUKU KWETU NA KWA WENGINE NI NUSU UCHI, WALIJIPITISHA MBELE YA MFALME MSWATI APATE CHAGUA MKE WA 14 (INGAWA JAMAA HAKUPICK).TEHE TEHE!! (nakumbuka yaliyotokea kati ya akudo na basata). HUMO MSAFARANI NAAMINI KUNA WENGI WASICHANA TOKA KTK FAMILIA ZA HALI DUNI, FAMILIA ZA KATI NA FUNGU LA WATOKAO FAMILIA BORA (TAJIRI) AMBAO WANASHIRIKI ZOEZI HILO WAKIPAMBWA NA VITO ASILI VILIVYO GHALI TOKA KWA WABUNIFU WAKUBWA NCHINI HUMO PENGINE HATA NJE! FIKRA ZINATUAMA KWA MSICHANA MASIKINI AMBAYE MILA NA DESTURI ZIMEMLAZIMISHA KUTEMBEA KTK GWARIDE HILO ILIKUTIMIZA JADI. NAVUTA PICHA KWA BINTI HUYO JINSI ANAVYOJIFICHA ATA ASIONEKANE KTK UPEO WA JICHO LA MFALME EITHER KUONA HASTAHILI KUWA HATA MJAKAZI WAKE AU PENGINE HOFU YA KIJINSIA. TERERE DHLAMINI BINTI WA MIAKA 16 BINGWA WA SHINDANO LA MWAKA KTK KUCHEZA NGOMA ASILI (UMHLANGA REED DANCE). AKIWA AMEVALIA SKETI TU'' YA ASILI ALINUKULIWA AKISEMA "I CAME HERE TO DANCE I WISH THE KING WOULD HAVE CHOSEN ME BECAUSE ITS NICE AT THE KING'S PLACE. THE WIVES LIVE A NICE LIFE"

"UKISIKIA USIKAE............."NIMELINASA MIDOMONI MWA WATU JE WEKETEREWE MWANA BOFOKOTORONGO MWENZAKATALANGU? AU UPO UPO TU KAMA GOGO LA MNAZI? (HATA KWA KUNI HALIFAI).
BUSTA RHYMES OHAAAA - OHAA!! "NDANI YA MZIKI MTIKISIKO UTASIKIA UTAONA LIVE LINI NA WAPI KAA TAYARI!"

Monday, September 7, 2009

AJALI KAZINI
NI ASUBUHI YA LEO WADAU WAKO KAZINI BAHATI NZURI HAKUNA ALIYEDHURIKA, SIJUI KILITOKEA NINI, MARA NGIDI-PWAAA!!